Ten Hag - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 02 Nov 2024 18:14:22 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.7.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ten Hag - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ten Hag awashukuru mashabiki https://www.greensports.co.tz/2024/11/02/ten-hag-awashukuru-mashabiki/ https://www.greensports.co.tz/2024/11/02/ten-hag-awashukuru-mashabiki/#respond Sat, 02 Nov 2024 16:20:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12228 Manchester, EnglandKocha Erik ten Hag aliyetimuliwa katika kikosi cha Man United, ameibuka kwa mara ya kwanza tangu kutimuliwa kwake na kuwashukuru mashabiki kwa namna walivyomuunga mkono.Ten Hag alitimuliwa Jumatatu iliyopita wakati timu hiyo ikishika nafasi ya 14 kwenye Ligi Kuu England (EPL) ikiwa na rekodi isiyovutia ya kupoteza mechi nne kati ya tisa za mwanzo […]

The post Ten Hag awashukuru mashabiki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchester, England
Kocha Erik ten Hag aliyetimuliwa katika kikosi cha Man United, ameibuka kwa mara ya kwanza tangu kutimuliwa kwake na kuwashukuru mashabiki kwa namna walivyomuunga mkono.
Ten Hag alitimuliwa Jumatatu iliyopita wakati timu hiyo ikishika nafasi ya 14 kwenye Ligi Kuu England (EPL) ikiwa na rekodi isiyovutia ya kupoteza mechi nne kati ya tisa za mwanzo za ligi hiyo msimu huu wa 2024-25.
Nafasi ya Ten Hag imechukuliwa na kocha kutoka Ureno, RĂºben Amorim ambaye hapo kabla alikuwa akiinoa Sporting Lisbon na anatarajia kuanza rasmi kazi hiyo mpya Novemba 11 mwaka huu.
“Nianze kwa kuwashukuru, asanteni kwa wakati wote kuwa karibu na klabu, iwe kwa mechi ya nyumbani au ugenini au mechi ngumu kwenye dimba la Old Trafford, hamkuwahi kuyumba katika kutuunga mkono,” alisema Ten Hag.
Kocha huyo pia aliwashukuru maofisa wa klabu hiyo katika kila idara mbalimbali kwa namna ambavyo walikuwa naye pamoja katika wakati mzuri na hata alipokuwa katika kipindi kigumu.

“Tumeshinda mataji mawili, mafanikio ambayo yataendelea kunifariji katika maisha yangu yote, ni kweli kwamba ndoto zangu zilikuwa ni kuipa klabu hii mataji mengi, bahati mbaya ndoto hiyo haikutimia,” alisema Ten Hag.


Man United ilitangaza rasmi jana Ijumaa uamuzi wa kumkabidhi Amorim majukumu ya Ten Hag ambapo kocha huyo mpya amesaini mkataba utakaofikia ukomo Juni 2027 kukiwa na kipengele kinachotoa nafasi ya kuongeza mwaka mmoja zaidi.

The post Ten Hag awashukuru mashabiki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/11/02/ten-hag-awashukuru-mashabiki/feed/ 0
Man Utd yamtimua Ten Hag https://www.greensports.co.tz/2024/10/28/man-utd-yamtimua-ten-hag/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/28/man-utd-yamtimua-ten-hag/#respond Mon, 28 Oct 2024 18:29:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12100 Manchester, EnglandHatimaye klabu ya Manchester United, leo Jumatatu imetangaza kumfuta kazi kocha Erik ten Hag kutokana na mwenendo usiovutia wa timu hiyo tangu kuanza kwa msimu huu wa 2024-25.Baada ya uamuzi huo, nafasi ya Ten Hag kwa sasa itakaimiwa na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Ruud van Nistelrooy ambaye alikuwa msaidizi wake.Kutokana na mwenendo […]

The post Man Utd yamtimua Ten Hag first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchester, England
Hatimaye klabu ya Manchester United, leo Jumatatu imetangaza kumfuta kazi kocha Erik ten Hag kutokana na mwenendo usiovutia wa timu hiyo tangu kuanza kwa msimu huu wa 2024-25.
Baada ya uamuzi huo, nafasi ya Ten Hag kwa sasa itakaimiwa na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Ruud van Nistelrooy ambaye alikuwa msaidizi wake.
Kutokana na mwenendo mbaya wa Man Utd, habari ya Ten Hag kutimuliwa ilipamba moto siku za karibuni na kutimia kwake ni kama kukamilika kwa tukio ambalo lilikuwa likisubiri siku.
Ten Hag alikuwa uwanjani mara ya mwisho jana Jumapili katika mechi na West Ham, mechi ambayo Man Utd ililala kwa mabao 2-1 na kwa sasa timu hiyo inashika nafasi ya 14 kwenye Ligi Kuu England ikiwa imecheza mechi tisa na kushinda tatu tu.
Taarifa ya klabu hiyo ilieleza kwamba Van Nistelrooy atasimamia masuala ya timu hiyo wakati mchakato wa kumpata kocha mpya wa kudumu ukiendelea huku tayari majina kadhaa yakianza kutajwa likiwamo la aliyekuwa kocha wa Barcelona, Xavi Hernandez.
Uamuzi wa kumtimua Ten Hag ulifikiwa leo asubuhi baada ya kikao cha ana kwa ana kati ya kocha huyo na ofisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Omar Berrada pamoja na Dan Ashworth ambaye ni mkurugenzi wa michezo na kocha huyo alielezwa wazi wazi juu ya uamuzi huo.
Baada ya uamuzi huo kufikiwa mchezaji wa kwanza kumtakia kila la heri Ten Hag katika mambo yake ya baadaye ni nahodha wa timu hiyo, Bruno Fernandes ambaye pia alimshukuru kwa kila kitu ikiwamo kwa muda wote ambao wamekuwa pamoja.

The post Man Utd yamtimua Ten Hag first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/28/man-utd-yamtimua-ten-hag/feed/ 0
Xavi, Amorim watajwa Man United https://www.greensports.co.tz/2024/10/26/xavi-amorim-watajwa-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/26/xavi-amorim-watajwa-man-united/#respond Sat, 26 Oct 2024 10:45:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12080 Manchester, EnglandNafasi ya kocha Erik ten Hag katika kikosi cha Man United imeendelea kujadiliwa huku makocha Xavi Hernandez na Ruben Amorim (pichani chini) wa Sporting Lisbon wakianza kutajwa.Hii si mara ya kwanza kwa Xavi aliyeachana na Barcelona msimu uliopita kutajwa akihusishwa na nafasi hiyo lakini kwa Amorin hii ni mara yake ya kwanza kuingizwa katika […]

The post Xavi, Amorim watajwa Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Nafasi ya kocha Erik ten Hag katika kikosi cha Man United imeendelea kujadiliwa huku makocha Xavi Hernandez na Ruben Amorim (pichani chini) wa Sporting Lisbon wakianza kutajwa.
Hii si mara ya kwanza kwa Xavi aliyeachana na Barcelona msimu uliopita kutajwa akihusishwa na nafasi hiyo lakini kwa Amorin hii ni mara yake ya kwanza kuingizwa katika mbio hizo.
Habari za ndani zilizopatikana kwenye vyanzo mbalimbali vya habari hii leo Jumamosi vimeeleza kuwapo kwa mpango huo ingawa makocha hao hawajasema lolote kuhusu kuhusishwa kwao.
Kilichopo wazi kwa Ten Hag ni kwamba mwenendo wa Man United si wa kuvutia katika Ligi Kuu England (EPL) hivyo mjadala kuhusu hatma ya kocha huyo ni jambo linalotarajiwa.


Mara baada ya msimu uliopita wa 2023-24 kumalizika ilitarajiwa ingekuwa mwisho wa Ten Hag kuinoa Man United lakini ubingwa wa Kombe la FA inasemekana ulimbeba na kuwafanya vigogo wa timu hiyo kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja.
Katika EPL hadi sasa Man United inashika nafasi ya 12 ikiwa imecheza mechi nane, imepoteza tatu na kushinda mitatu na kutoka sare mara mbili.
Na ingawa kocha huyo amekuwa akijifariji mara kwa mara kutokana na janga la wachezaji majeruhi kwenye kikosi chake lakini kiujumla hali halisi hairidhishi na haishangazi kuona nafasi yake ikizidi kugeuzwa mjadala.

The post Xavi, Amorim watajwa Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/26/xavi-amorim-watajwa-man-united/feed/ 0
Ten Hag: Tuache kupaniki https://www.greensports.co.tz/2024/10/03/ten-hag-tuache-kupaniki/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/03/ten-hag-tuache-kupaniki/#respond Thu, 03 Oct 2024 07:21:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11975 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Erik ten Hag amesema licha ya timu yake kuanza vibaya msimu huu kwa kupoteza mechi nne na kushinda mbili tu za Ligi Kuu England (EPL) bado hakuna sababu ya kupaniki.Kocha huyo Mholanzi ametoa kauli hiyo baada ya timu yake kulala kwa mabao 3-0 mbele ya Tottenham Hotspur katika mechi ya […]

The post Ten Hag: Tuache kupaniki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Erik ten Hag amesema licha ya timu yake kuanza vibaya msimu huu kwa kupoteza mechi nne na kushinda mbili tu za Ligi Kuu England (EPL) bado hakuna sababu ya kupaniki.
Kocha huyo Mholanzi ametoa kauli hiyo baada ya timu yake kulala kwa mabao 3-0 mbele ya Tottenham Hotspur katika mechi ya mwisho ya EPL Jumapili iliyopita hali ambayo imeibua hofu.
Mwenendo mzima wa timu hiyo inayoshika nafasi ya 13 katika EPL unaonekana kukiweka pabaya kibarua cha kocha huyo ambaye takriban miezi minne iliyopita aliongezewa mkataba.

“Tutakuwa wenye mafanikio msimu huu, hakuna jambo rahisi lakini yanayotokea hayana sababu ya kunifanya nipaniki, tunaweza kulimaliza tatizo, hii timu inaweza kuyamaliza mambo haya,” alisema Ten Hag.


Ten Hag pia alisisitiza kwamba hana hofu ya usalama wa kibarua chake licha ya kupoteza mechi dhidi ya Spurs huku akikabiliwa na mechi ya Europa dhidi ya Porto pamoja na mechi ya EPL dhidi ya Aston Villa.
Kocha huyo badala yake alisisitiza kwamba hafikirii chochote na wala hana hofu, akifafanua kwamba walijenga mazingira ya umoja kati ya wamiliki na viongozi na wote wanayalinda mambo hayo.
“Tuna makubaliano ambayo wote tupo nyuma ya makubaliano hayo, tunajua kwamba mbinu yetu ni kuwaandaa wachezaji vijana ambao wapo katika kipindi cha mpito,” alisema Ten Hag.

The post Ten Hag: Tuache kupaniki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/03/ten-hag-tuache-kupaniki/feed/ 0
Ten Hag amtaka Rashford atupie kwa wingi https://www.greensports.co.tz/2024/09/15/ten-hag-ampa-neno-rashford-2/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/15/ten-hag-ampa-neno-rashford-2/#respond Sun, 15 Sep 2024 12:09:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11912 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Erik ten Hag amemtaka mshambuliaji wake, Marcus Rashford kuhakikisha anafunga mabao mengi msimu huu baada ya kuandamwa na ukame wa mabao kwa miezi sita.Rashford jana Jumamosi alifunga bao dhidi ya Southampton katika ushindi wa 3-0, bao ambalo limekuja baada ya mchezaji huyo kutoka uwanjani bila kufunga katika mechi 13 za […]

The post Ten Hag amtaka Rashford atupie kwa wingi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Erik ten Hag amemtaka mshambuliaji wake, Marcus Rashford kuhakikisha anafunga mabao mengi msimu huu baada ya kuandamwa na ukame wa mabao kwa miezi sita.
Rashford jana Jumamosi alifunga bao dhidi ya Southampton katika ushindi wa 3-0, bao ambalo limekuja baada ya mchezaji huyo kutoka uwanjani bila kufunga katika mechi 13 za Man United.
Mara ya mwisho, Rashford kuifungia bao Man United ilikuwa Machi 9 mwaka huu katika mechi dhidi ya Everton, mechi ambayo timu hiyo ilitoka na ushindi wa mabao 2-0.
Kutokana na ukame wa mabao ambao umekuwa ukimuandama Rashford, 26, kuna wakati alijikuta akishambuliwa vikali na mashabiki wa Man United wengi wao wakimshutumu kwa kutojituma.
Kabla ya mechi na Sothampton Ten Hag aliulizwa ni kwa nini alimpanga Rashford kikosi cha kwanza ambapo kocha huyo alisema kwamba mshambuliaji huyo alihitaji kufunga bao moja au kutoa asisti ili arudi katika kasi yake ya mabao.
Matumaini ya Ten Hag ni kwamba mshambuliaji huyo kwa sasa ni kama amefungua njia baada ya rekodi mbaya ya mabao manane tu kwa mashindano yote ya msimu uliopita wa 2023-24, hiyo ni baada ya kuwa na rekodi ya kuvutia ya mabao 30 kwa msimu wa 2022-23.
“Hilo ni jambo muhimu kwa kila mshambuliaji, wanachohitaji ni kuwa katika orodha ya waliofunga, baada tu ya bao la kwanza mengine mengi yanafuata,” alisema Ten Hag.

The post Ten Hag amtaka Rashford atupie kwa wingi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/15/ten-hag-ampa-neno-rashford-2/feed/ 0
Ten Hag akiri Man United bado https://www.greensports.co.tz/2024/08/16/ten-hag-akiri-man-united-bado/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/16/ten-hag-akiri-man-united-bado/#respond Fri, 16 Aug 2024 07:31:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11785 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Erik ten Hag ameonesha kuwa na wasiwasi na timu yake kama ipo tayari kwa mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2024-25 dhidi ya Fulham, leo Ijumaa.Man United itakuwa nyumbani katika mechi hiyo ya kwanza ambapo wachezaji wake wapya Noussair Mazraoui na Matthijs de Ligt watakuwa […]

The post Ten Hag akiri Man United bado first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Erik ten Hag ameonesha kuwa na wasiwasi na timu yake kama ipo tayari kwa mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2024-25 dhidi ya Fulham, leo Ijumaa.
Man United itakuwa nyumbani katika mechi hiyo ya kwanza ambapo wachezaji wake wapya Noussair Mazraoui na Matthijs de Ligt watakuwa kwenye kikosi cha timu hiyo wakiwa ndio kwanza wamewasili Alhamisi na hivyo kumuweka njia panda Ten Hag kuhusu kuwapa nafasi au la.
Sambamba na hilo Ten Hag ana janga la majeruhi kuanzia kwa Luke Shaw, beki mpya Leny Yoro na mshambuliaji Rasmus Hojlund ambao kila mmoja ana matatizo yake ambapo kwa Yoro imebainika atakuwa nje kwa miezi mitatu.
Katika usajili wa wachezaji wapya Man United imemwaga kitita cha Pauni 60 ili kuwanasa Mazraoui na De Ligt kutoka Bayern lakini uhakika wa kuwatumia katika mechi ya leo ni jambo linalomtatiza Ten Hag.

“Timu hii haijawa tayari lakini ligi ndio inaanza, ni dhahiri kuna makocha wengine wengi wenye tatizo kama hili lakini ni lazima tuanze, hatuwezi kujificha katika hilo, hatuwezi kulikimbia, ni lazima tukabiliane nalo,” alisema Ten Hag.


Eneo la beki wa kushoto ni tatizo jingine litakalomuweka njia panda Ten Hag katika kuamua nani wa kumpanga kwa kuwa Shaw hayuko fiti wakati Tyrell Malacia naye ni majeruhi na atakuwa nje kwa miezi miwili akijiuguza hoti.

The post Ten Hag akiri Man United bado first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/16/ten-hag-akiri-man-united-bado/feed/ 0
Ten Hag aongezewa mkataba https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/ten-hag-aongezewa-mkataba/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/ten-hag-aongezewa-mkataba/#respond Thu, 04 Jul 2024 19:58:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11525 Manchester, EnglandKlabu ya Manchester United imemuongezea mkataba kocha Erik ten Hag ambao sasa utamfanya aendelee kuwa na klabu hiyo hadi mwaka 2026 ikiwa ni mwaka mmoja zaidi ya mkataba wa sasa unaoishia 2025.Sambamba na hilo, klabu hiyo inaendelea kufanya maboresho ya maofisa wake wakiwamo wa benchi la ufundi huku kukiwa na habari kuwa Ruud van […]

The post Ten Hag aongezewa mkataba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Manchester United imemuongezea mkataba kocha Erik ten Hag ambao sasa utamfanya aendelee kuwa na klabu hiyo hadi mwaka 2026 ikiwa ni mwaka mmoja zaidi ya mkataba wa sasa unaoishia 2025.
Sambamba na hilo, klabu hiyo inaendelea kufanya maboresho ya maofisa wake wakiwamo wa benchi la ufundi huku kukiwa na habari kuwa Ruud van Nistelrooy na Rene Heke wapo mbioni kujiunga na klabu hiyo.
Ten Hag alisema kwamba ana furaha kwa kufikia makubaliano na uongozi wa klabu hiyo kwa lengo la kuendelea kufanya kazi pamoja.

“Tukiangalia miaka miwili iliyopita tunaweza kutafakari tukiwa wenye kujivunia mataji mawili na mifano mingi ya hatua za mafanikio kutoka pale ambapo tulikuwa wakati najiunga na klabu hii,” alisema Ten Hag.


Ten Hag hata hivyo aliweka wazi kuwa pamoja na mafanikio hayo ni lazima wawe wazi kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kufikia kiwango kinachotarajiwa katika klabu hiyo ambacho ni kupigania mataji ya England na Ulaya.
Alisema kwamba katika mazungumzo yake na uongozi wa klabu hiyo wamekuwa wamoja katika dira yao ya kuhakikisha wanafikia malengo hayo na wako pamoja na imara katika kuhakikisha safari hiyo inakuwa ya pamoja.
Ten Hag alijiunga na Man United mwaka 2022 akitokea Ajax ya Uholanzi na kusaini mkataba ambao ulitarajiwa kufikia ukomo mwaka 2025 kabla ya kuongezwa hii leo Alhamisi na sasa utafikia ukomo ifikapo Juni 2026.

The post Ten Hag aongezewa mkataba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/ten-hag-aongezewa-mkataba/feed/ 0
Man United wamfuata Ten Hag akiwa mapumzikoni https://www.greensports.co.tz/2024/06/17/man-united-wamfuata-ten-hag-akiwa-mapumzikoni/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/17/man-united-wamfuata-ten-hag-akiwa-mapumzikoni/#respond Mon, 17 Jun 2024 16:34:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11353 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Erik ten Hag amesema akiwa katika mapumziko yake kwenye fukwe za Ibiza ghafla mabosi wa klabu hiyo walimfuata na kumwambia wanataka aendelee kuwa kocha wa timu hiyo.Majaliwa ya Ten Hag katika kikosi cha Man United yamekuwa njia panda kabla na hata baada ya Man United kucheza mechi ya fainali ya […]

The post Man United wamfuata Ten Hag akiwa mapumzikoni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Erik ten Hag amesema akiwa katika mapumziko yake kwenye fukwe za Ibiza ghafla mabosi wa klabu hiyo walimfuata na kumwambia wanataka aendelee kuwa kocha wa timu hiyo.
Majaliwa ya Ten Hag katika kikosi cha Man United yamekuwa njia panda kabla na hata baada ya Man United kucheza mechi ya fainali ya Kombe la FA Mei 25 dhidi ya Man City na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Akizungumzia alivyofuatwa, Ten Hag alisema mabosi wa klabu hiyo walimfuata akiwa mapumzikoni Ibiza na hapo hapo baada ya kukutana naye wakamwambia wanataka aendelee na kazi akiwa na timu hiyo.
Man United imemaliza msimu wa 2023-24 wa Ligi Kuu England (EPL) ikiwa nafasi ya nane, nafasi ambayo ni ya chini mno katika kipindi cha miaka takriban 20 na hivyo habari za kutimuliwa kwa Ten Hag zikavuma kwa kasi kwenye vyombo vya habari.
Kabla ya kufuta mpango wa kumtimua, Ten Hag, mmiliki mwenza wa klabu hiyo, Sir Jim Ratcliffe alishafanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Thomas Tuchel ili akabidhiwe mikoba ya Ten Hag.

“Manchester United wameniambia kwamba walizungumza na Tuchel lakini mwishowe wakafikia hitimisho la kwamba tayari wana kocha bora,” alisema Ten Hag.


Alisema kwamba mabosi wa Ineos ambayo ni kampuni ya Sir Jim ni watu wapya katika soka kwa hiyo ilikuwa kawaida kwao kufanya tathmini ya msimu na si siri kwamba walifanya mazungumzo na makocha kadhaa.
Ten Hag hata hivyo alisema kwamba bado hajakaa na mabosi hao wa Man United kwa ajili ya kusaini mkataba mpya na kwamba jambo hilo watapata wasaa wa kulijadili.

The post Man United wamfuata Ten Hag akiwa mapumzikoni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/17/man-united-wamfuata-ten-hag-akiwa-mapumzikoni/feed/ 0
Ten Hag haondoki Man United https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/ten-hag-haondoki-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/ten-hag-haondoki-man-united/#respond Wed, 12 Jun 2024 07:05:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11309 Manchester, EnglandUtata kuhusu hatma ya kocha Erik Ten Hag wa Man United umekwisha na habari mpya ni kwamba baada ya kufanya tathmini kwa mapana vigogo wa bodi ya klabu hiyo wameamua kocha huyo asiondoke.Vigogo hao ambao wamekuwa katika zoezi la kumfanyia tathmini Ten Hag na mwenendo wa timu kwa msimu uliopita wa 2023-24, wameama waanze […]

The post Ten Hag haondoki Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Utata kuhusu hatma ya kocha Erik Ten Hag wa Man United umekwisha na habari mpya ni kwamba baada ya kufanya tathmini kwa mapana vigogo wa bodi ya klabu hiyo wameamua kocha huyo asiondoke.
Vigogo hao ambao wamekuwa katika zoezi la kumfanyia tathmini Ten Hag na mwenendo wa timu kwa msimu uliopita wa 2023-24, wameama waanze mazungumzo ya kumuongezea mkataba kocha huyo.
Tathmini ya kocha huyo ilianza mara baada ya mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Man City iliyopigwa Mei 25 na Man United kuibuka na ushindi na tayari zilikuwapo habari kwamba kocha huyo angetimuliwa mara tu baada ya mechi hiyo.
Mambo hata hivyo yalibadilika na habari zaidi kudai kwamba ushindi wa mabao 2-1 ambao Man United iliupata katika mechi hiyo na hatimaye kubeba taji huenda ndio uliobadili upepo.
Inadaiwa baada ya tathmini ya kina na mazungumzo yaliyomshirikisha Ten Hag hatimaye muafaka umefikiwa wa kocha huyo Mholanzi mwenye umri wa miaka 54 kuendelea na kibarua chake katika timu hiyo.
Ten Hag bila shaka ataupokea vizuri uamuzi huo hasa baada ya kuwa njia panda kwa muda mrefu akiwa hajui hatma yake kama ataendelea na kibarua chake au angetimuliwa.
Makocha kadhaa tayari walianza kutajwa kuchukua nafasi yake wakiwamo Roberto de Zerbi, Graham Potter, Thomas Frank pamoja na kocha wa sasa wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate.
Ten Hag, alianza kuinoa Man United majira ya kiangazi mwaka 2022 akitokea Ajax, katika msimu wake wa kwanza aliiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England (EPL) pamoja na fainali ya Kombe la FA.
Februari 23, Ten Hag alishinda taji lake la kwanza Man United ambalo ni EFL na msimu huu ingawa amebeba taji la FA lakini mambo hayakuwa mazuri kwenye EPL

The post Ten Hag haondoki Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/ten-hag-haondoki-man-united/feed/ 0
Tuchel akataa kumrithi Ten Hag https://www.greensports.co.tz/2024/06/10/tuchel-akataa-kumrithi-ten-hag/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/10/tuchel-akataa-kumrithi-ten-hag/#respond Mon, 10 Jun 2024 07:30:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11284 Munich, UjerumaniKocha wa zamani wa Bayern Munich na Chelsea, Thomas Tuchel ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na Man United amejiweka kando na kazi hiyo kwa alichodai kuwamba kwa sasa anataka kupumzika.Tuchel, 50, ni kati ya makocha ambao katika siku za karibuni wamekuwa wakipewa nafasi kubwa ya kumrithi Erik Ten Hag ambaye kwa muda […]

The post Tuchel akataa kumrithi Ten Hag first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Kocha wa zamani wa Bayern Munich na Chelsea, Thomas Tuchel ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na Man United amejiweka kando na kazi hiyo kwa alichodai kuwamba kwa sasa anataka kupumzika.
Tuchel, 50, ni kati ya makocha ambao katika siku za karibuni wamekuwa wakipewa nafasi kubwa ya kumrithi Erik Ten Hag ambaye kwa muda mrefu sasa hatma yake Man United ipo njia panda.
Kwa sasa vigogo wa Man United wanafanya tathmini ya mwenendo wa timu yao kwa msimu mzima wa 2023-24 na bado hawajatoa hitimisho la nini kitafanyika kuelekea msimu ujao na hata Ten Hag hajawa na uhakika kama ataendelea kuinoa timu hiyo au la.
Wakati hayo yakiendelea zipo habari kwamba Tuchel aliwahi kukutana na mmiliki mwenza wa Man United Sir Jim Ratcliffe nchini Ufaransa ingawa undani wa mazungumzo ya wawili hao haukuwahi kuwekwa wazi.
Kwa upande wake, Tuchel ambaye pia amewahi kuzinoa klabu za PSG na Borussia Dortmund hata hivyo amedai kwamba kwa sasa anataka kupumzika baada ya kuachana na Bayern mwishoni mwa msimu.
Makocha wengine ambao wamekuwa wakitajwa kuchukua nafasi ya Ten Hag Man United ni pamoja na Graham Potter, Thomas Frank pamoja na kocha wa England, Gareth Southgate.

The post Tuchel akataa kumrithi Ten Hag first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/10/tuchel-akataa-kumrithi-ten-hag/feed/ 0