Tabora United - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 02 Apr 2025 18:47:17 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.7.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Tabora United - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Tabora yachezea kichapo kwa Yanga https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/tabora-yachezea-kichapo-kwa-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/tabora-yachezea-kichapo-kwa-yanga/#respond Wed, 02 Apr 2025 18:47:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13192 Na mwandishi wetuHatimaye Yanga leo Jumatano Aprili 2, 2025 imebeba pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu NBC baada ya kuilaza Tabora United mabao 3-0, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.Kwa matokeo hayo Yanga imejiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 61 baada ya kucheza mechi 23 ikifuatiwa na […]

The post Tabora yachezea kichapo kwa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hatimaye Yanga leo Jumatano Aprili 2, 2025 imebeba pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu NBC baada ya kuilaza Tabora United mabao 3-0, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Kwa matokeo hayo Yanga imejiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 61 baada ya kucheza mechi 23 ikifuatiwa na mahasimu wao Simba wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 22.
Yanga ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 16 mfungaji akiwa ni beki Israel Mwenda kwa mpira wa adhabu iliyotolewa baada ya beki wa Tabora, Banele Junior kumchezea rafu Prince Dube.
Tabora wakishangiliwa na mashabiki wao wa nyumbani walipambana kutaka kusawazisha huku Hiritier Makambo akionekana kuisumbua safu ya ulinzi ya Yanga ingawa hadi muda wa mapumziko unafika walikuwa ni Yanga waliotoka uwanjani na bao hilo pekee.
Kipindi cha pili kila timu iliendelea kuonesha nia ya kutaka bao lakini alikuwa ni Clement Mzize aliyewainua vitini mashabiki wa Yanga dakika 10 baada ya mapumziko akiitumia pasi ya Pacome Zouzoua.
Yanga walikamilisha karamu ya mabao dakika ya 67 kwa bao la Dube ambaye aliinasa pasi ya Pacome na kumzunguka beki wa Tabora kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Jan Noel.
Dalili za ushindi kwa Yanga zilianza kuonekana mapema dakika ya 11 baada ya Ibrahim Bacca kuunganisha kwa kichwa kona iliyochongwa na Pacome lakini mpira aliopiga uligonga mwamba.
Dakika tatu kabla ya shambulizi hilo, Mzize naye alimpora mpira beki wa Tabora na kugongeana vyema na wachezaji wenzake na mpira kumrudia kabla ya kufumua shuti ambalo lilipaa juu ya lango.
Ushindi wa leo umepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wa Yanga baada ya majibizano na majigambo yaliyotawala kabla ya mechi hiyo lakini zaidi ikikumbukwa Yanga ilivyolala kwa mabao 3-1 timu hizo zilipokutana Novemba mwaka jana.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho Alhamisi kwa mechi kati ya JKT Tanzania na Dodoma Jiji, Kagera Sugar na Coastal Union na Ken Gold dhidi ya Azam FC.

The post Tabora yachezea kichapo kwa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/tabora-yachezea-kichapo-kwa-yanga/feed/ 0
Simba yaiengua Yanga kileleni https://www.greensports.co.tz/2025/02/02/simba-yaiengua-yanga-kileleni/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/02/simba-yaiengua-yanga-kileleni/#respond Sun, 02 Feb 2025 19:26:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12965 Na mwandishi wetuSimba imeiengua Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Tabora United mabao 3-0 katika mechi ya ligi hiyo iliyochezwa leo Jumapili, Februari 2, 2025.Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 43 na kuizidi Yanga kwa tofauti ya pointi moja, baada ya Yanga kushika nafasi hiyo kwa takriban saa 24.Simba ilianza […]

The post Simba yaiengua Yanga kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imeiengua Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Tabora United mabao 3-0 katika mechi ya ligi hiyo iliyochezwa leo Jumapili, Februari 2, 2025.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 43 na kuizidi Yanga kwa tofauti ya pointi moja, baada ya Yanga kushika nafasi hiyo kwa takriban saa 24.
Simba ilianza kuzitikisa nyavu za Tabora katika dakika ya 12 kwa bao la Leonel Ateba aliyefumua shuti kali lililomshinda kipa wa Tabora, Jean Amonome.
Wenyeji Tabora wakiwa kwenye dimba lao la Ali Hassan Mwinyi walipambana kusawazisha bao hilo kabla ya kuvunjwa nguvu dakika ya 32 baada ya Simba kuandika bao la pili lililofungwa tena na Ateba.
Ateba alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa na mwamuzi Kefa Kayombo baada ya Faria Odongo kumchezea rafu Elly Mpanzu, rafu ambayo pia ilimfanya Odongo apewe kadi ya njano.
Juhudi za Ateba zilizalisha bao la tatu kwa Simba ambalo lilifungwa na beki Shomari Kapombe katika dakika ya 66.
Kwa matokeo hayo Tabora inabaki nafasi ya tano ikiwa na pointi 25, imetanguliwa na Singida Big inayoshika nafasi ya nne na pointi zake 33 wakati Azam FC inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36.

The post Simba yaiengua Yanga kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/02/simba-yaiengua-yanga-kileleni/feed/ 0
Rage ataka Tabora Utd wasikate tamaa https://www.greensports.co.tz/2024/06/06/rage-ataka-tabora-utd-wasikate-tamaa/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/06/rage-ataka-tabora-utd-wasikate-tamaa/#respond Thu, 06 Jun 2024 05:50:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11243 Na mwandishi wetuMwenyekiti wa zamani wa Simba na mdau wa Tabora United, Ismail Aden Rage ameitaka timu ya Tabora kutokata tamaa ya kusalia Ligi Kuu NBC kwani bado wana nafasi ya kufanya hivyo kama wataamka mapema.Rage ametoa rai hiyo baada ya Tabora kuchezea kipigo cha mabao 4-0 jana Jumanne dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja […]

The post Rage ataka Tabora Utd wasikate tamaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa zamani wa Simba na mdau wa Tabora United, Ismail Aden Rage ameitaka timu ya Tabora kutokata tamaa ya kusalia Ligi Kuu NBC kwani bado wana nafasi ya kufanya hivyo kama wataamka mapema.
Rage ametoa rai hiyo baada ya Tabora kuchezea kipigo cha mabao 4-0 jana Jumanne dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora katika mechi ya awali ya kuwania kubaki ligi kuu msimu ujao. Mechi ya marudiano ni Juni 8, mwaka huu.
“Niwaambie tu Tabora wasikate tamaa bado kuna nafasi ya mechi ya pili ya marudiano, hata kama itaonekana idadi ya mabao ni kubwa na bahati mbaya ikashindikana kupata matokeo mchezo wa pili basi kuna mchezo na Biashara United pia.

“Kwa hiyo bado kuna nafasi nyingine hata kama hii ikipotea, wanaweza kujipanga na kupambana upya na kusalia ligi kuu kupitia Biashara na pia nimezungumza na benchi la ufundi na kuwaeleza makosa machache ya ulinzi ndiyo yametugharimu,” alisema Rage mchezaji wa zamani wa Simba.


Mshindi wa jumla baina ya JKT na Tabora atasalia ligi kuu wakati aliyeshindwa atavaana na Biashara ya Championship kwa ajili ya mechi mbili za mwisho za kutafuta kushiriki ligi kuu msimu ujao wa 2024-25.

The post Rage ataka Tabora Utd wasikate tamaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/06/rage-ataka-tabora-utd-wasikate-tamaa/feed/ 0
Djuma akichambua kipigo cha 2-0 https://www.greensports.co.tz/2024/05/08/djuma-akichambua-kipigo-cha-2-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/08/djuma-akichambua-kipigo-cha-2-0/#respond Wed, 08 May 2024 06:21:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10889 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Tabora United, Masoud Djuma amesema kupoteza kwao mechi dhidi ya Simba kwa mabao 2-0, kumetokana na uwepo wa faida ya timu kubwa ya Simba na si vinginevyo.Akifafanua hilo Djuma alisema katika mabao waliyofunga Simba katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatatu hii kwenye dimba la Azam Complex, Dar es Salaam, hakukuwa na […]

The post Djuma akichambua kipigo cha 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Tabora United, Masoud Djuma amesema kupoteza kwao mechi dhidi ya Simba kwa mabao 2-0, kumetokana na uwepo wa faida ya timu kubwa ya Simba na si vinginevyo.
Akifafanua hilo Djuma alisema katika mabao waliyofunga Simba katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatatu hii kwenye dimba la Azam Complex, Dar es Salaam, hakukuwa na bao lolote lolote la kimbinu.
“Unapocheza na timu kubwa faida inakuwa kwao, kwanza wapo nyumbani, sisi tunataka matokeo na wao wanataka matokeo lakini faida wanaipa timu kubwa, tunaelewa huo ndiyo mpira acha tusahau hilo tuna mechi na Mtibwa (Sugar) na yaliyojiri tumeyasahau sababu unapocheza na timu kubwa haya yanatokea.
“Hatukufungwa kimbinu ilikua ni makosa yetu wenyewe, bao la kwanza ilipaswa kila mtu atembee na mtu sababu tunajua huwa Simba wana wachezaji wa kuruka vichwa lakini haikuwa hivyo.

“Goli la pili tumefunga sisi refa kaacha, wachezaji wamezembea wakitaka lile goli lililofungwa, wakapiga (Simba) ‘counter-attack’ wakafunga na hapo hakuna mbinu yoyote, lakini tunaelewa tumecheza na timu kubwa na ndiyo wakati wao huu na hatuna budi kuendelea na safari,” alisema Djuma.


Naye kaimu kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda alisema: “Ninashukuru wachezaji wangu kwa namna walivyojitoa mpaka tumepata alama tatu muhimu na kubwa zaidi ni mchezaji wangu wa 12, mashabiki waliojitokeza kuja kutusapoti na tumemaliza salama na sasa tunajipanga na Azam.
“Mechi na Azam ni mechi ngumu kama inavyofahamika, tunashindana kwa kufuatana katika msimamo. Ni mechi yenye taswira itakayoonesha nani atakuwa wapi na tunaenda kujipanga dhidi yao kuhakikisha tunapata matokeo yaliyo mazuri.”

The post Djuma akichambua kipigo cha 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/08/djuma-akichambua-kipigo-cha-2-0/feed/ 0
Simba yaitandika Tabora Utd 2-0 https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/simba-yaitandika-tabora-utd-2-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/simba-yaitandika-tabora-utd-2-0/#respond Tue, 07 May 2024 06:24:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10866 Na mwandishi wetuSimba imefanikiwa kunyakua pointi tatu baada ya kuichapa Tabora United mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa Jumatatu hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.Ushindi huo umeifanya Simba kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya mahasimu wao Yanga kutoka 15 za awali na sasa inakuwa imezidiwa na Yanga yenye […]

The post Simba yaitandika Tabora Utd 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imefanikiwa kunyakua pointi tatu baada ya kuichapa Tabora United mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa Jumatatu hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Ushindi huo umeifanya Simba kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya mahasimu wao Yanga kutoka 15 za awali na sasa inakuwa imezidiwa na Yanga yenye pointi 65 kwa tofauti ya pointi 12.
Simba hata hivyo pamoja na ushindi huo wanaendelea kubaki nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa wametanguliwa na Azam FC yenye pointi 57 ingawa Simba wamecheza mechi 24 dhidi ya 25 za Azam.
Mabao ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na Kanoute katika dakika ya 19 wakati bao la pili na la ushindi lilifungwa na Edwin Balua.
Kwa Tabora Utd, matokeo hayo yanazidi kuwaweka pagumu kwani hadi sasa wameweza kuvuna pointi 23 katika mechi 25 hivyo wana kazi ya kujinasua na janga la kushuka daraja katika ligi hiyo yenye timu 16.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa Jumatatu hii, Azam ilitoka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Mtibwa Sugar mabao ya washindi yakifungwa na Feisal Salum na Girbil Sillah wakati Coastal Union na Prisons zilitoka sare ya 0-0.

The post Simba yaitandika Tabora Utd 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/simba-yaitandika-tabora-utd-2-0/feed/ 0
Yanga, Coastal zatua nusu fainali FA https://www.greensports.co.tz/2024/05/02/yanga-coastal-zatua-nusu-fainali-fa/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/02/yanga-coastal-zatua-nusu-fainali-fa/#respond Thu, 02 May 2024 06:01:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10823 Na mwandishi wetuVinara wa Ligi Kuu NBC, Yanga wamefanikiwa kukata tiketi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) baada ya kuitandika Tabora United mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam, Complex jijini Dar es Salaam.Kwa ushindi huo Yanga inaungana na timu za Coastal Union na Ihefu FC ambazo pia zimejikatia tiketi ya […]

The post Yanga, Coastal zatua nusu fainali FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Vinara wa Ligi Kuu NBC, Yanga wamefanikiwa kukata tiketi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) baada ya kuitandika Tabora United mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam, Complex jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo Yanga inaungana na timu za Coastal Union na Ihefu FC ambazo pia zimejikatia tiketi ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo sasa inajulikana kwa jina la Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya benki ya CRDB kuwa mdhamini.
Katika mechi ya Yanga ambayo ilianza mapema Jumatano hii, vinara hao wa Ligi Kuu NBC waliandika bao la kwanza katika dakika ya 35 mfungaji akiwa ni Stephanie Aziz Ki.
Mabao mengine mawili ya Yanga yalifungwa na Kennedy Musonda dakika ya 66 na Joseph Guede dakika nane kabla ya kutimia dakika tisini za mchezo.
Kwa upande wa timu nyingine, Coastal imefuzu nusu fainali baada ya kuilaza bao 1-0 Geita Gold FC wakati Ihefu FC imefuzu kwa ushindi wa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0 na Mashujaa FC.
Katika mechi za nusu fainali Yanga inatarajia kuumana na Ihefu wakati Coastal wao wataoneshana ubabe na mshindi wa mechi kati ya Namungo FC dhidi ya Azam.

The post Yanga, Coastal zatua nusu fainali FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/02/yanga-coastal-zatua-nusu-fainali-fa/feed/ 0
Goran ahesabu siku Tabora United https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/goran-ahesabu-siku-tabora-united/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/goran-ahesabu-siku-tabora-united/#respond Thu, 21 Mar 2024 08:02:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10272 Na mwandishi wetuUongozi wa timu ya Tabora United upo katika hatua za mwisho kuachana na kocha wao mkuu, Goran Kopunovic kutokana na mwenendo mbaya uliokuwa nayo timu hiyo kwenye Ligi Kuu NBC.Mtendaji Mkuu wa Tabora United, Thabiti Kandoro alisema wameshakutana na kocha huyo na kumueleza namna wasivyoridhishwa na mwenendo wa timu yao na wapo katika […]

The post Goran ahesabu siku Tabora United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa timu ya Tabora United upo katika hatua za mwisho kuachana na kocha wao mkuu, Goran Kopunovic kutokana na mwenendo mbaya uliokuwa nayo timu hiyo kwenye Ligi Kuu NBC.
Mtendaji Mkuu wa Tabora United, Thabiti Kandoro alisema wameshakutana na kocha huyo na kumueleza namna wasivyoridhishwa na mwenendo wa timu yao na wapo katika hatua za mwisho kusitisha mkataba wake.

“Bado hatujaachana naye sababu kuna haki zake tunasubiri kumkamilishia lakini kama uongozi tupo katika mchakato wa kumsaka mbadala wake atakayeiongoza timu yetu katika mechi zilizobaki,” alisema Kandoro.


Mtendaji huyo alisema matokeo ambayo timu yao inayapata hayaendani na ubora wa kikosi walichokisajili msimu huu ndio maana wanataka kuachana na Mserbia huyo.
Tabora inayoshiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo ikiwa na pointi 21 na tayari imecheza idadi kama hiyo ya mechi na imebakiwa na mechi tisa kabla msimu kumalizika.

The post Goran ahesabu siku Tabora United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/goran-ahesabu-siku-tabora-united/feed/ 0
Ouma akiri mechi na Tabora ngumu https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/ouma-akiri-mechi-na-tabora-ngumu/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/ouma-akiri-mechi-na-tabora-ngumu/#respond Fri, 01 Mar 2024 08:06:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9948 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Coastal Union, David Ouma, (pichani) amesema mchezo wao dhidi ya Tabora United utakuwa mgumu lakini anakiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha wanapata ushindi.Mchezo huo umepangwa kuchezwa Machi 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora na mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu wameahidi kuibuka na ushindi katika mchezo […]

The post Ouma akiri mechi na Tabora ngumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Coastal Union, David Ouma, (pichani) amesema mchezo wao dhidi ya Tabora United utakuwa mgumu lakini anakiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha wanapata ushindi.
Mchezo huo umepangwa kuchezwa Machi 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora na mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu wameahidi kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
“Ni mchezo mgumu ukizingatia tutakuwa ugenini lakini malengo yetu ni ushindi na tutahakikisha tunacheza kwa juhudi kuhakikisha hatupotezi mchezo huu, ni mchezo muhimu, kila mmoja anajiandaa vya kutosha,” alisema Ouma raia wa Kenya.
Kocha huyo alisema wanataka kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao hivyo ni lazima wapambane ili kubaki kwenye nafasi za juu za kushiriki michuano hiyo mwisho wa msimu.
Wagosi wa Kaya hao wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC wakikusanya pointi 26 katika michezo 17 waliyocheza hadi sasa.

The post Ouma akiri mechi na Tabora ngumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/ouma-akiri-mechi-na-tabora-ngumu/feed/ 0
Matola ataja kilichoiponza Tabora Utd https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/matola-ataja-kilichoiponza-tabora-utd/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/matola-ataja-kilichoiponza-tabora-utd/#respond Thu, 08 Feb 2024 06:54:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9627 Na mwandishi wetuKocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola amesema siri ya ushindi wao dhidi ya Tabora United ilitokana na kuwasoma vyema wapinzani wao na kutumia udhaifu wao kufunga mabao.Matola alisema hayo baada ya mchezo wao huo wa Ligi Kuu NBC uliochezwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora juzi na Simba kushinda mabao 4-0.“Tuliwasoma Tabora […]

The post Matola ataja kilichoiponza Tabora Utd first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola amesema siri ya ushindi wao dhidi ya Tabora United ilitokana na kuwasoma vyema wapinzani wao na kutumia udhaifu wao kufunga mabao.
Matola alisema hayo baada ya mchezo wao huo wa Ligi Kuu NBC uliochezwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora juzi na Simba kushinda mabao 4-0.
“Tuliwasoma Tabora United na kugundua wanapenda kwenda mbele na kuacha nafasi za pembeni wazi na sisi tukazitumia na kupiga krosi tukafanikiwa,” alisema Matola.
Naye kocha wa Tabora United, Goran Kopunovic alikubali kupoteza mchezo lakini akilia na nyasi za uwanja pamoja na makosa binafsi ya wachezaji wake.

“Ni kweli tumefungwa mabao 4-0 lakini nyasi zimechangia kwa sababu zilikuwa ndefu zikafanya mpira usitembee. Tabora na Simba zimetofautiana kwa ubora lakini kuwakosa wachezaji muhimu nako kumechangia kupoteza,” alisema Kopunovic.


Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 29 katika nafasi ya tatu ikiwa nyuma kwa mchezo mmoja huku Tabora ikiendelea kusalia nafasi ya 12 kwa pointi 15.

The post Matola ataja kilichoiponza Tabora Utd first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/matola-ataja-kilichoiponza-tabora-utd/feed/ 0
Yanga yatamba, Simba yakwama https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/yanga-yatamba-simba-yakwama/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/yanga-yatamba-simba-yakwama/#respond Sun, 24 Dec 2023 11:29:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8994 Na mwandishi wetuSimba imepata pigo katika Ligi Kuu NBC baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na KMC wakati mahasimu wao Yanga wakitoka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Tabora United.Katika mechi hizo zilizochezwa Jumamosi hii, Simba ikiwa Azam Complex, ilishitushwa na KMC dakika ya 31 baada ya Waziri Junior kufunga bao na kuifanya […]

The post Yanga yatamba, Simba yakwama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imepata pigo katika Ligi Kuu NBC baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na KMC wakati mahasimu wao Yanga wakitoka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Tabora United.
Katika mechi hizo zilizochezwa Jumamosi hii, Simba ikiwa Azam Complex, ilishitushwa na KMC dakika ya 31 baada ya Waziri Junior kufunga bao na kuifanya KMC iende mapumziko ikiwa mbele.
Juhudi za Simba zilizaa matunda katika dakika ya 57 baada ya kupata bao la kusawazisha lililowekwa kimiani na Saido Ntibazonkiza kwa mkwaju wa penalti.
Dakika mbili baadaye Simba waliongeza bao la pili lililowekwa kimiani kwa kichwa na Jean Baleke baada ya kuinasa krosi ya Shomary Kapombe.
Matarajio ya Simba kutoka uwanjani na pointi zote tatu yalizimwa katika dakika ya 89 baada ya Waziri Junior kuipatia KMC bao la pili akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Tepsi Evans.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kubaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23 katika mechi 10 wakati KMC imefikisha pointi 17 ikiwa katika nafasi ya saba.
Kwa upande wa Yanga iliyokuwa ugenini mjini Dodoma kwenye dimba la Jamhuri, ilinufaika na bao pekee la Aziz Ki na kutoka na ushindi ambao umeiimarisha timu hiyo katika nafasi ya pili ya ligi hiyo.
Yanga sasa imekusanya pointi 30 tofauti ya pointi moja mbele ya Azam inayoshika usukani wa ligi hiyo wakati Tabora inabaki nafasi ya 12 na pointi zake 15.
Ligi hiyo kwa sasa imesimama kupisha mashindano ya kila mwaka ya Kombe la Mapinduzi pamoja na maandalizi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2024) zitakaofanyika mwakani nchini Ivory Coast.

The post Yanga yatamba, Simba yakwama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/yanga-yatamba-simba-yakwama/feed/ 0