Senegal – Greensports Site: Habari za michezo na burudani Tanzania na Ulimwenguni. https://www.greensports.co.tz Michezo na burudani ni zaidi ya ajira Sun, 04 Jun 2023 07:29:08 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.6.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Senegal – Greensports Site: Habari za michezo na burudani Tanzania na Ulimwenguni. https://www.greensports.co.tz 32 32 Pape Sakho aitwa timu ya Taifa https://www.greensports.co.tz/2023/06/04/pape-sakho-aitwa-timu-ya-taifa/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/04/pape-sakho-aitwa-timu-ya-taifa/#respond Sun, 04 Jun 2023 07:28:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6432

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Sakho ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Senegal kinachojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Afcon 2023 dhidi ya Benin.
Sakho (pichani) ameitwa kwenye kikosi hicho na kocha mkuu wa timu hiyo, Aliou Cisse kwa mara ya pili baada ya awali kuitwa Machi mwaka huu walipokuwa wakijiandaa kuuamana na timu ya taifa ya Msumbiji.
Senegal iliyoita jumla ya wachezaji 26 itavaana na Benin ikiwa ugenini Juni 17 mjini Cotonou kabla ya kucheza mechi ya kirafiki na Brazil Juni 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa José Alvalade mjini Lisbon, Ureno.
Cisse hata hivyo amewatema mshambuliaji wa Lorient, Bamba Dieng na kipa wa Chelsea, Edouard Mendy katika kikosi hicho na kuwajumuisha winga Ismail Jacobs wa AS Monaco, kiungo Pape Gueye (Sevilla) na Cheikhou Kouyate (Nottingham Forest) aliyerejea kikosini baada ya awali kukosekana kutokana na majeraha.
Baadhi ya nyota wengine walioitwa kwenye kikosi cha mabingwa hao watetezi wa Afcon ni Sadio Mane wa Bayern Munich, Kalidou Koulibaly (Chelsea), Gana Gueye (Everton), Ismaila Sarr (Watford) na Abdou Diallo (RB Leipzig).
Senegal inaongoza Kundi L ikiwa na pointi 10, ikifuatiwa na Msumbiji yenye pointi nne, Rwanda ya tatu ikiwa na pointi tatu huku Benin ikiburuza mkia kwa pointi mbili baada ya timu zote kucheza mechi nne.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/04/pape-sakho-aitwa-timu-ya-taifa/feed/ 0
Sakho aitwa timu ya Taifa Senegal https://www.greensports.co.tz/2023/03/17/sakho-aitwa-timu-ya-taifa-senegal/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/17/sakho-aitwa-timu-ya-taifa-senegal/#respond Fri, 17 Mar 2023 19:28:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5518

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Sakho ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Senegal kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Afcon 2023 dhidi ya Msumbiji.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuitwa kwenye timu ya taifa tangu alipojiunga na miamba hiyo ya Tanzania mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Teungueth ya nyumbani kwao Senegal.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Senegal, vinaeleza kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Aliou Cisse amemjumuisha Sakho baada ya kuvutiwa na kiwango chake anachokionesha akiwa na Simba kwenye michuano ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Ni mchezaji mwenye kipaji cha juu ukitaka kuthibitisha hilo msimu uliopita aliibuka mshindi wa bao bora kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, naamini anaweza kutusaidia kufikia malengo yetu dhidi ya Msumbuji,” alisema Cisse.
Katika orodha ya wachezaji 24, Sakho ataungana na baadhi ya nyota wengine wa timu hiyo wakiwemo mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane, Gana Gueye anayekipiga Everton, Bamba Dieng anayecheza Lorient ya Ufaransa, Kalidou Coulibally wa Chelsea.
Sakho anaungana na wachezaji wengine wa Simba Henock Inonga (DR Congo), Clatous Chama (Zambia), Aishi Manula, Mzamiru Yassin, Beno Kakolanya ambao wameitwa kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya kuwania kufuzu fainali za Afcon zinazotarajiwa kufanyika Ivory Coast.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/17/sakho-aitwa-timu-ya-taifa-senegal/feed/ 0