Morrison - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 09 Sep 2023 12:17:49 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.7.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Morrison - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Morrison apewa jezi namba 5 https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/morrison-apewa-jezi-namba-5/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/morrison-apewa-jezi-namba-5/#respond Sat, 09 Sep 2023 12:17:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7718 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa zamani wa Yanga, Bernard Morrison amepewa jezi namba tano katika timu yake mpya ya AS FAR ya Morocco.Morrison ameweka wazi juu ya hilo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii akiwa na jezi hiyo akionesha kufurahishwa na uteuzi wa namba ya jezi hiyo.Taarifa mbalimbali zimefafanua kuwa Morisson amepewa mkataba wa mwaka […]

The post Morrison apewa jezi namba 5 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Bernard Morrison amepewa jezi namba tano katika timu yake mpya ya AS FAR ya Morocco.
Morrison ameweka wazi juu ya hilo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii akiwa na jezi hiyo akionesha kufurahishwa na uteuzi wa namba ya jezi hiyo.
Taarifa mbalimbali zimefafanua kuwa Morisson amepewa mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo inayonolewa na kocha Nasreddine Nabi anayeelezwa kumuhitaji mchezaji huyo wa Ghana baada ya kufanya naye kazi Yanga kabla ya wote kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita.
Awali, Morrison aliyeondoka Yanga akiwa huru baada ya kumaliza mkataba wake alikuwa akionekana akifanya mazoezi na sehemu ya kikosi hicho kabla ya hivi karibuni kuelezwa amekamilisha dili lake hilo.
Mbali na Yanga, Morrison pia aliwahi kuitumikia Simba kwa nyakati mbili tofauti pia amewahi kukipiga DC Motema Pembe na AS Vita za DR Congo, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na sasa anaanza maisha mapya Afrika ya Kaskazini.

The post Morrison apewa jezi namba 5 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/morrison-apewa-jezi-namba-5/feed/ 0
Morrison shabiki namba moja wa Skudu https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/morrison-shabiki-namba-moja-wa-skudu/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/morrison-shabiki-namba-moja-wa-skudu/#respond Sat, 22 Jul 2023 09:44:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7069 Na mwandishi wetuAliyekuwa winga wa Yanga, Bernard Morrison amesema yeye ni shabiki namba moja wa winga mpya wa Yanga, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ na anasubiri kwa hamu kuona Skudu atakavyowaonesha Watanzania vitu vya mpira ambavyo hata yeye alifundishwa na winga huyo.Skudu aliyesajiliwa na Yanga kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini amewahi kucheza na Morrison wakiwa Orlando […]

The post Morrison shabiki namba moja wa Skudu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Aliyekuwa winga wa Yanga, Bernard Morrison amesema yeye ni shabiki namba moja wa winga mpya wa Yanga, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ na anasubiri kwa hamu kuona Skudu atakavyowaonesha Watanzania vitu vya mpira ambavyo hata yeye alifundishwa na winga huyo.
Skudu aliyesajiliwa na Yanga kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini amewahi kucheza na Morrison wakiwa Orlando Pirates, lakini pia wakishabihiana aina ya uchezaji, wote wakitumika kama washambuliaji wa pembeni wakiwa na chenga za maudhi na mbwembwe nyingi.
Morrison ameeleza kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwamba anajivunia kuhusika kumleta Skudu katika timu hiyo bila kufafanua namna alivyohusika.
“Namna furaha inavyoonekana, sihitaji kuzunguma sana kwa sasa. Nitazungumza baadaye jinsi gani ninajivunia kukuleta hapa, nenda kaioneshe Tanzania vyote uliyowahi kunifundisha. Mimi shabiki yako namba moja, nakupenda kijana wangu,” aliandika Morrison.
Morrison kuonesha kuwa amevutiwa mno na Skudu kutua Yanga, aliibuka kwenye mazoezi ya kwanza ya mchezaji huyo na Yanga akiwa amevalia jezi namba sita yenye jina Skudu akimkumbatia na kufurahi kwa kumuona.
Yanga iliachana na Morrison baada ya kumalizika kwa msimu wa 2022-23 na sasa duru mbalimbali za michezo zinafafanua kuwa raia huyo wa Ghana anatarajia kutambulishwa na Singida Fountain Gate hivi karibuni.

The post Morrison shabiki namba moja wa Skudu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/morrison-shabiki-namba-moja-wa-skudu/feed/ 0
Simba yaachana na Morrison https://www.greensports.co.tz/2022/05/13/simba-yaachana-na-morrison/ https://www.greensports.co.tz/2022/05/13/simba-yaachana-na-morrison/#respond Fri, 13 May 2022 14:23:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=722 Na mwandishi wetuBaada ya tetesi za hapa na pale hatimaye habari mbili zimeibuka kuhusu mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison. Moja ni ya kupumzishwa hadi mwishoni mwa msimu wakati mkataba wakeutakapofikia mwisho.Habari hiyo inabebwa na habari ya pili ambayo inaonekana kuwa na nguvu zaidi kuwa Simba imeamua inaachana na mchezaji huyo na ilichofanya ni kuchelewesha tu […]

The post Simba yaachana na Morrison first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Morrison wakati akisaini mkataba Simba

Na mwandishi wetu
Baada ya tetesi za hapa na pale hatimaye habari mbili zimeibuka kuhusu mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison. Moja ni ya kupumzishwa hadi mwishoni mwa msimu wakati mkataba wakeutakapofikia mwisho.
Habari hiyo inabebwa na habari ya pili ambayo inaonekana kuwa na nguvu zaidi kuwa Simba imeamua inaachana na mchezaji huyo na ilichofanya ni kuchelewesha tu jambo hilo hadi baada ya kumalizika mkataba Hiyo maana yake ni kwamba akimaliza mapumziko na mkataba umekwisha. Ni kama vile ameachwa kiaina ili suala hilo limalizike kimya kimya bila makeke hasa kwa kuwa zipo habari kwamba anaelekea kwa mahasimu wao Yanga.
Na ingawa bado haijathibitishwa lakini vyanzo mbalimbali vimekuwa vikieleza kuwa Simba imeamua kuachana na mchezaji huyo kutokana na vitendo vyake vya utovu wa nidhamu lakini pia inadaiwa ni baada ya kumalizana na Yanga kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao.
Kabla ya taarifa hiyo iliyotolewa leo kupitia mitandao ya kijamii ya Simba, tayari kuliibuka sintofahamu kuhusu hatma ya mchezaji huyo ambaye mara ya mwisho alionekana akiitumikia Simba kwenye mchezo dhidi ya Yanga ulioisha kwa suluhu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Simba kupitia taarifa yake ilieleza kuwa inamshukuru Morrison raia wa Ghana kwa mchango wake katika kipindi cha miaka miwili aliyoitumikia timu hiyo ikiwemo kuwapa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Kombe la Mapinduzi, Kombe la Shirikisho la Azam na Kombe la Mapinduzi.
“Klabu yetu imempa mapumziko ya hadi mwisho wa msimu mchezaji Bernard Morrison. Simba imefikia maamuzi hayo baada ya pande zote mbili kukubalina kwa lengo la kumpa nafasi Morrison kupumzika na kushughulikia mambo yake binafsi.
“Simba inamshukuru Morrison kwa mchango wake kwa kipindi chote alichohudumu ndani ya klabu yetu. Kwa mchango na mafanikio hayo klabu inamshukuru mchezaji huyo kipenzi cha Wanasimba kwa kujitoa kwake kuipigania klabu yake.
“Simba inamtakia kila la heri Morrison katika mapumziko yake na safari yake ya soka hapo baadaye,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Habari ya Morisson imekuja wakati jana kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa na video iliyomuonyesha mchezaji huyo akiwa na kipa Aishi Manula ambapo kwenye video hiyo, Morrison alikuwa akisema, ‘bado nipo sana,’ alikuwa akifundishwa kutamka maneno hayo na Manula.
Taarifa nyingine ya Morisson iliyopatakana kwenye mitandao leo, inamnukuu mchezaji huyo akisema kwamba atakosekana katika klabu hiyo kwa kipindi cha msimu kilichobaki kwa sababu ya matatizo ya kifamilia ambayo yataathiri uwajibikaji wake katika timu iwapo ataendelea kuitumikia katika mechi zilizobaki.
Katika taarifa hiyo Morrison ameitakia kila lakheri Simba kwa michezo iliyobaki huku akiomba amalize matatizo yanayomkabili ili aweze kurudi na kuitumikia Simba kwa mechi zilizobaki.
Morrison alitua nchini mara ya kwanza mwaka 2020 na kusaini Yanga alikodumu kwa miezi sita kabla ya baadaye kutimkia Simba ambako amehudumu kwa miaka miwili, mkataba wake ukitarajiwa kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

The post Simba yaachana na Morrison first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/05/13/simba-yaachana-na-morrison/feed/ 0