Minziiro - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 04 Oct 2023 05:52:51 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Minziiro - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Minziro awaita mashabiki Sokoine https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/minziro-awaita-mashabiki-sokoine/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/minziro-awaita-mashabiki-sokoine/#respond Wed, 04 Oct 2023 05:49:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7933 Na mwandishi wetuKocha wa Tanzania Prisons, Fred Minziro amewataka mashabiki wa timu hiyo na wakazi wa Mbeya kwenda kuushuhudia ushindi wa kwanza kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Simba SC.Minziro (pichani juu) ameyaeleza hayo leo Jumanne wakiwa katika maandalizi ya mwisho ya mchezo wao huo wa kwanza msimu huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya […]

The post Minziro awaita mashabiki Sokoine first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa Tanzania Prisons, Fred Minziro amewataka mashabiki wa timu hiyo na wakazi wa Mbeya kwenda kuushuhudia ushindi wa kwanza kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Simba SC.
Minziro (pichani juu) ameyaeleza hayo leo Jumanne wakiwa katika maandalizi ya mwisho ya mchezo wao huo wa kwanza msimu huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya utakaopigwa keshokutwa.
Prisons inayoburuza mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC kwa pointi moja, imecheza mechi tatu ugenini mpaka sasa ambapo imetoa sare mechi moja na kufungwa mara mbili.

“Maandalizi yamekwenda vizuri, tumejaribu kufanya masahihisho ya hapa na pale kutokana na mechi zilizopita. Siwezi kusema naahidi nini lakini tunakutana na mchezo mgumu ila mashabiki wa Prisons na wananchi wa Mbeya waje kwa wingi kusapoti kuhakikisha tunapata matokeo kwenye mechi yetu ya kwanza hapa nyumbani,” alisema Minziro.


Wakati hali ikiwa hivyo Prisons, Simba yenyewe imeshinda michezo yake mitatu ya ligi ya awali ikiwa inashika nafasi ya pili kwa pointi tisa, sawa na vinara Yanga ambao wako juu kwa idadi ya mabao ya kufunga.

The post Minziro awaita mashabiki Sokoine first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/minziro-awaita-mashabiki-sokoine/feed/ 0
Minziro: Sijui hatma yangu Geita Gold https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/minziro-sijui-hatma-yangu-geita-gold/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/minziro-sijui-hatma-yangu-geita-gold/#respond Fri, 26 May 2023 19:26:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6300 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro amesema bado hafahamu hatma yake ya kuendelea kuinoa timu hiyo kutokana na kufika ukingoni kwa mkataba wake.Kocha huyo ameiambia GreenSports leo Ijumaa kuwa mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, ingawa amepata ofa za timu nyingine tayari lakini anasikiliza kwanza mazungumzo ya mabosi wake hao […]

The post Minziro: Sijui hatma yangu Geita Gold first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro amesema bado hafahamu hatma yake ya kuendelea kuinoa timu hiyo kutokana na kufika ukingoni kwa mkataba wake.
Kocha huyo ameiambia GreenSports leo Ijumaa kuwa mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, ingawa amepata ofa za timu nyingine tayari lakini anasikiliza kwanza mazungumzo ya mabosi wake hao wa sasa.
Amesema ingawa anatarajia kukutana na uongozi wa timu hiyo hivi karibuni kufahamu kama anaendelea au la lakini kutokuwa na uhakika kwa sasa kunamkwamisha kuanza harakati za mapema za kufanya usajili wa wachezaji wa msimu ujao.
“Ni kweli namaliza mkataba mwisho wa msimu huu, zimesalia siku chache mno lakini bado hakuna mazungumzo na uongozi kuhusiana na hilo japokuwa natarajia kukutana nao kabla ya kucheza mechi mbili zilizosalia za ligi.

“Kama inavyoonekana kweli tunaelekea kipindi cha usajili, kuisuka vizuri zaidi timu kwa ajili ya msimu ujao lakini huwezi kufanya hivyo kwa sasa sababu bado haijafahamika itakuwaje siku za usoni kuhusu kuendelea kubaki Geita,” alisema Minziro.


Minziro beki wa zamani wa Yanga, amekuwa na Geita tangu alipoipandisha timu hiyo daraja kucheza ligi kuu msimu wa 2021-22 na kisha kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Hiyo ni baada ya kumaliza kwenye nne bora ya msimamo wa ligi kuu katika msimu wao wa kwanza. Msimu huu Geita ipo nafasi ya sita ikipambana kumaliza kwenye tano bora.

The post Minziro: Sijui hatma yangu Geita Gold first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/minziro-sijui-hatma-yangu-geita-gold/feed/ 0