Mancini - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 28 Aug 2023 18:37:11 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mancini - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mancini kocha mkuu Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2023/08/28/mancini-kocha-mkuu-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/28/mancini-kocha-mkuu-saudi-arabia/#respond Mon, 28 Aug 2023 18:37:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7555 Riyadh, Saudi ArabiaAliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya Italia, Roberto Mancini ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Saudi Arabia ikiwa ni takriban wiki mbili baada ya kujiuzulu kuinoa timu ya Italia.Mancini ameiongoza vyema Italia katika fainali za Kombe la Ulaya 2020 ‘Euro 2020’ na kuiwezesha kubeba taji hilo kwa kuwabwaga […]

The post Mancini kocha mkuu Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya Italia, Roberto Mancini ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Saudi Arabia ikiwa ni takriban wiki mbili baada ya kujiuzulu kuinoa timu ya Italia.
Mancini ameiongoza vyema Italia katika fainali za Kombe la Ulaya 2020 ‘Euro 2020’ na kuiwezesha kubeba taji hilo kwa kuwabwaga wenyeji England kwa penalti katika mechi iliyopigwa kwenye dimba la Wembley.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 ambaye pia amewahi kuinoa Man City, akiwa na timu ya Italia amejiwekea rekodi ya kuiongoza katika mechi 37 bila kupoteza hata moja hadi kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2022 zilizofanyika Qatar, Novemba hadi Desemba mwaka jana.
Mancini amesaini mkataba wa kuinoa timu ya Saudi Arabia hadi mwaka 2027 na mtihani wake wa kwanza utakuwa Septemba 8 katika mechi ya kirafiki na Costa Rica itakayopigwa St James’ Park, Newcastle.

“Naamini hii ni fursa kubwa kwangu, kupata uzoefu wa soka katika nchi mpya hususan kutokana na kukuwa kwa umaarufu wa soka katika bara la Asia,” alisema Mancini.


Mancini ambaye ndiye aliyeipa Man City taji la kwanza la Ligi Kuu England, pia amewahi kuzinoa timu za Inter Milan, Lazio, Fiorentina, Galatasaray na Zenit St Petersburg.
Katika fainali za Kombe la Dunia mwaka jana, timu ya Saudi Arabia ikiwa chini ya kocha Mfaransa, Herve Renard iliushtua ulimwengu kwa kuilaza mabao 2-1 Argentina ambayo baadaye ndiyo iliyobeba taji hilo ingawa pamoja na ushindi huo, timu hiyo haikuweza kuvuka hatua ya makundi.

The post Mancini kocha mkuu Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/28/mancini-kocha-mkuu-saudi-arabia/feed/ 0
Spalletti amrithi Mancini Italia https://www.greensports.co.tz/2023/08/19/spalletti-amrithi-mancini-italia/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/19/spalletti-amrithi-mancini-italia/#respond Sat, 19 Aug 2023 19:06:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7455 Milan, ItaliaKocha wa zamani wa Napoli, Luciano Spalletti (pichani) ametangazwa na Shirikisho la Soka Italia kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Taifa akichukua nafasi ya Roberto Mancini ambaye Agosti 13 alijiuzulu.Spalletti alijipatia heshima msimu uliopita wa 2022-23 kwa kuiwezesha Napoli kutwaa taji la Serie A kwa mara ya kwanza baada ya miaka 33 lakini […]

The post Spalletti amrithi Mancini Italia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Milan, Italia
Kocha wa zamani wa Napoli, Luciano Spalletti (pichani) ametangazwa na Shirikisho la Soka Italia kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Taifa akichukua nafasi ya Roberto Mancini ambaye Agosti 13 alijiuzulu.
Spalletti alijipatia heshima msimu uliopita wa 2022-23 kwa kuiwezesha Napoli kutwaa taji la Serie A kwa mara ya kwanza baada ya miaka 33 lakini pia amewahi kuzinoa AS Roma, Inter Milan na Zenit St Petersburg ya Urusi.
Spalletti mwenye umri wa miaka 64, baada ya kuipa mafanikio Napoli, aliomba likizo ndefu mwezi Mei mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na kocha Rudi Garcia kutoka Ufaransa.
Katika taarifa ya Shirikisho la Soka Italia lilielezwa kwamba kocha huyo mpya ataanza kazi rasmi Septemba Mosi na shirikisho linaamini Spalletti ni mtu sahihi wa kukabiliana na changamoto zilizo mbele yake.

“Timu ya taifa inahitaji kocha mwenye hadhi, na nina furaha Spalletti amekubali, shauku na uzoefu wake ni vitu muhimu katika kukabiliana na changamoto zinazoisubiri Italia miezi michache ijayo,” alisema rais wa shirikisho hilo, Gabriele Gravina.


Na ingawa taarifa ya shirikisho hilo haijaweka wazi mkataba wa kocha huyo ni wa muda gani lakini zipo habari kwamba atainoa timu hiyo hadi mwaka 2026 wakati wa fainali za Kombe la Dunia.
Mechi ya kwanza ya Spalletti na timu ya Taifa ya Italia itakuwa Septemba 9, timu hiyo itakapoumana na North Macedonia kuwania kufuzu fainali za Euro 2024 na siku tatu baadaye itaumana na Ukraine.
Katika kuwania kufuzu Euro 2024, Italia ipo Kundi C ambalo pia lina timu ya England inayoshika usukani ikiwa na pointi 12 katika mechi nne wakati Italia ni ya tatu na Ukraine ya pili.

The post Spalletti amrithi Mancini Italia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/19/spalletti-amrithi-mancini-italia/feed/ 0