Katwila - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 08 Dec 2023 18:40:59 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Katwila - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Katwila aomba fungu la kuiokoa Mtibwa https://www.greensports.co.tz/2023/12/08/katwila-aomba-fungu-la-kuiokoa-mtibwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/08/katwila-aomba-fungu-la-kuiokoa-mtibwa/#respond Fri, 08 Dec 2023 18:40:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8788 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila ameuomba uongozi wa timu hiyo kutenga kiasi kikubwa cha pesa ili kufanya usajili wa nguvu kwenye dirisha dogo.Dirisha dogo linatarajiwa kufunguliwa Desemba 16 na litafungwa Januari 15, mwakani ambapo kocha huyo amesisitiza kuwa maingizo mapya ndio tiba pekee itakayoinusuru timu hiyo na janga la kushuka daraja […]

The post Katwila aomba fungu la kuiokoa Mtibwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila ameuomba uongozi wa timu hiyo kutenga kiasi kikubwa cha pesa ili kufanya usajili wa nguvu kwenye dirisha dogo.
Dirisha dogo linatarajiwa kufunguliwa Desemba 16 na litafungwa Januari 15, mwakani ambapo kocha huyo amesisitiza kuwa maingizo mapya ndio tiba pekee itakayoinusuru timu hiyo na janga la kushuka daraja mwishoni mwa msimu huu.
Katwila alisema kinachoisumbua timu yake ni idadi kubwa ya wachezaji wake kukosa uzoefu hivyo kushindwa kuhimili ushindani uliopo kwenye ligi.
“Bado tunayo nafasi ya kurekebisha makosa yetu lakini tunahitaji kuboresha kikosi chetu kwa kusajili wachezaji wenye uzoefu na ligi ambao kwa sasa tunawakosa,” alisema Katwila.
Kocha huyo alisema ukiacha uzoefu, wachezaji wengi kwenye timu hiyo wana uwezo mkubwa wa kucheza mpira na ndio maana pamoja na kupoteza idadi kubwa ya mechi lakini wamekuwa wakionesha kiwango bora katika mechi zao nyingi.
Alisema yeye bado ana imani kuwa timu hiyo itafanya vizuri na kubaki kwenye ligi kuu, lakini hilo linaweza kutimia endapo watakiboresha kikosi chao katika dirisha dogo.
Mtibwa Sugar inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi tano katika michezo 12 ya Ligi Kuu NBC iliyocheza mpaka sasa.

The post Katwila aomba fungu la kuiokoa Mtibwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/08/katwila-aomba-fungu-la-kuiokoa-mtibwa/feed/ 0
Katwila asikilizia ofa mpya https://www.greensports.co.tz/2023/10/19/katwila-asikilizia-ofa-mpya/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/19/katwila-asikilizia-ofa-mpya/#respond Thu, 19 Oct 2023 09:33:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8160 Na mwandishi wetuSiku chache baada ya kufutwa kazi na klabu ya Ihefu, kocha Zuberi Katwila (pichani) ameweka wazi kuwa hana muda wa kupumzika na anasikiliza ofa kutoka timu yoyote yenye maono mazuri ya kisoka.Kocha huyo amezungumza hayo na GreenSports ikiwa takriban siku sita zimepita tangu aondolewe kuinoa Ihefu baada ya kuiongoza katika mechi tano pekee […]

The post Katwila asikilizia ofa mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Siku chache baada ya kufutwa kazi na klabu ya Ihefu, kocha Zuberi Katwila (pichani) ameweka wazi kuwa hana muda wa kupumzika na anasikiliza ofa kutoka timu yoyote yenye maono mazuri ya kisoka.
Kocha huyo amezungumza hayo na GreenSports ikiwa takriban siku sita zimepita tangu aondolewe kuinoa Ihefu baada ya kuiongoza katika mechi tano pekee msimu huu akishinda mbili na kufungwa tatu.
“Siwezi kusema kwamba kuna timu fulani naisubiria au ni lazima nifundishe timu za ligi kuu peke yake, zipo timu nyingi zina mipango mizuri ya kisoka zipo madaraja ya chini, hivyo cha msingi ni sehemu yenye maono ya soka na ushindani nafikiri ndio nitaipa kipaumbele zaidi,” alisema Katwila.
Katwila aliyewahi kuinoa Mtibwa Sugar ya Morogoro alisema angeweza kupumzika kwa sasa lakini anahisi bado anahitaji kufanya vingi katika ukocha kwa sasa kuliko kupumzika kwa muda na kuwa nje ya mchezo.

“Naweza kupumzika lakini kwa sasa nahisi si muda sahihi sana wa kufanya hivyo sababu nina vitu vingi nahitaji kuvifanya kwenye soka na muda wa kupumzika ukifika nitapumzika kidogo kama kujipa likizo tu lakini kwa sasa bado kwanza,” alisema Katwila.


The post Katwila asikilizia ofa mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/19/katwila-asikilizia-ofa-mpya/feed/ 0
Ihefu mguu sawa kuivaa Simba https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/ihefu-mguu-sawa-kuivaa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/ihefu-mguu-sawa-kuivaa-simba/#respond Sun, 19 Mar 2023 11:22:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5530 Na mwandishi wetuTimu ya Ihefu imeeleza kuwa inajipanga vilivyo kuhakikisha inavaana na Simba kwenye mechi mbili mfululizo za michuano tofauti na kuibukia kidedea dhidi ya Wekundu hao.Ihefu ambayo ilikuwa na mapumziko ya siku tano, imerejea mazoezini jana kuanza rasmi mawindo yao hayo ya mechi ya robo fainali ya Kombe la FA na ile ya ligi, […]

The post Ihefu mguu sawa kuivaa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Ihefu imeeleza kuwa inajipanga vilivyo kuhakikisha inavaana na Simba kwenye mechi mbili mfululizo za michuano tofauti na kuibukia kidedea dhidi ya Wekundu hao.
Ihefu ambayo ilikuwa na mapumziko ya siku tano, imerejea mazoezini jana kuanza rasmi mawindo yao hayo ya mechi ya robo fainali ya Kombe la FA na ile ya ligi, zote dhidi ya Simba zinazotarajiwa kupigwa Aprili, mwaka huu.
Kocha Msaidizi wa Ihefu, Zuberi Katwila ameiambia GreenSports kuwa wanafahamu kibarua hicho dhidi ya Wekundu hao na kwa kuwa ni mechi mbili zenye hadhi tofauti basi wanafahamu tofauti ya namna ya kujipanga nazo ili zote wapate matokeo.
“Tuko kwenye kujiandaa dhidi ya Simba, ni mechi mbili tofauti, hivyo maandalizi ya Kombe la FA yatakuwa ni ya dakika 90 na ligi yatakuwa namna ya kutafuta pointi, yaani tunajipanga kwa namna mechi husika inavyotaka na lengo ni kupata ushindi mechi zote.

“Lengo letu ni kuvuka kwanza hapa tulipo kwa maana ya kusonga nusu fainali ya Kombe la FA, tutakayekutana naye mbele naye tutajua namna ya kufanya, ni hatua moja baada ya nyingine na tunajipanga kwa ajili ya kufanya vizuri,” alisema Katwila.


Licha ya kuteka hisia za wengi kwa timu hizo kukutana mara mbili mfululizo kwenye michuano tofauti lakini pia kiwango ilichonacho Ihefu hivi karibuni kimekuwa gumzo zaidi.
Ihefu ambayo ilianza vibaya ligi, imeshinda mechi nne na sare moja katika mechi zake tano zilizopita huku pia ikisifika kuwaadhibu vigogo kila wanapokuwa uwanja wao wa nyumbani.
Iliichapa Azam bao 1-0 kwenye mechi ya mwisho na ndiyo timu pekee iliyoifunga Yanga msimu huu kwa ushindi wa mabao 2-1.

The post Ihefu mguu sawa kuivaa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/ihefu-mguu-sawa-kuivaa-simba/feed/ 0