Jenni Hermoso - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 26 Feb 2025 20:10:03 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.7.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Jenni Hermoso - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Aliyepigwa busu mdomoni ataka adhabu iwe fundisho https://www.greensports.co.tz/2025/02/24/aliyepigwa-busu-mdomoni-ataka-adhabu-iwe-fundisho/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/24/aliyepigwa-busu-mdomoni-ataka-adhabu-iwe-fundisho/#respond Mon, 24 Feb 2025 18:46:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13048 Madrid, HispaniaMchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso aliyepigwa busu la mdomoni amesema adhabu iliyotolewa kwa Luis Rubiales aliyempiga busu ibaki kuwa somo.Wakati wa utoaji tuzo kwa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni alipigwa busu la mdomoni na Rubiales wakati huo akiwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, tukio ambalo lilizua […]

The post Aliyepigwa busu mdomoni ataka adhabu iwe fundisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso aliyepigwa busu la mdomoni amesema adhabu iliyotolewa kwa Luis Rubiales aliyempiga busu ibaki kuwa somo.
Wakati wa utoaji tuzo kwa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni alipigwa busu la mdomoni na Rubiales wakati huo akiwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, tukio ambalo lilizua mjadala mkubwa duniani kote.
Hivi karibuni Mahakama Kuu Hispania ilimpa Rubiales adhabu ya faini ya Dola 10,700 kwa kosa la udhalilishaji kijinsia pamoja na marufuku ya kumsogelea Jenni kwa umbali usiozidi mita 200 na kutofanya mazungumzo naye kwa mwaka mmoja.
Rubiales, 47, ambaye alilazimika kujiuzulu nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Hispania, hata hivyo alifutiwa tuhuma za kutumia nguvu na kumlazimisha Jenni aseme kwamba busu hilo alipigwa kwa makubaliano.
Akizungumzia sakata hilo na uamuzi wa mahakama kwa mara ya kwanza, Jenni alitumia mtandao wa Instagram na kusisitiza kwamba uamuzi wa mahakama ni hatua muhimu.
Jenni hata hivyo aliongeza kwa kusema kwamba kwa mazingira yanayowazunguka katika jamii bado kuna mengi yanatakiwa kufanywa.

“Moyo wangu upo kamili pamoja na kila mtu ambaye amekuwa na ataendelea kuwa pamoja nami katika mapambano haya, na sasa yamefikia mwisho,” alisema Jenni.


Ijumaa iliyopita, Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) iliitupa rufaa iliyowasilishwa na Rubiales ya kupinga adhabu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka mitatu aliyopewa na Fifa.

The post Aliyepigwa busu mdomoni ataka adhabu iwe fundisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/24/aliyepigwa-busu-mdomoni-ataka-adhabu-iwe-fundisho/feed/ 0
Aliyembusu mchezaji mdomoni akutwa na hatia https://www.greensports.co.tz/2025/02/20/aliyembusu-mchezaji-mdomoni-akutwa-na-hatia/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/20/aliyembusu-mchezaji-mdomoni-akutwa-na-hatia/#respond Thu, 20 Feb 2025 19:32:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13034 Madrid, HispaniaRais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales amekutwa na hatia katika kesi ya udhalilishaji kijinsia baada ya kumpiga busu la mdomoni mchezaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso.Rubiales alimpiga mchezaji huyo busu lililozua taharuki wakati wa utoaji tuzo mara baada ya Hispania kuibuka mshindi wa fainali za Kombe la […]

The post Aliyembusu mchezaji mdomoni akutwa na hatia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales amekutwa na hatia katika kesi ya udhalilishaji kijinsia baada ya kumpiga busu la mdomoni mchezaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso.
Rubiales alimpiga mchezaji huyo busu lililozua taharuki wakati wa utoaji tuzo mara baada ya Hispania kuibuka mshindi wa fainali za Kombe la Dunia la Wanawake mwaka 2023.
Mahakama Kuu Hispania baada ya kumkuta na hatia katika kosa hilo imetaja adhabu ya faini ya Dola 10,400 kwa kosa hilo lakini imemfutia kosa la kutoa vitisho au ubabe.
Rubiales mara baada ya kutajiwa hukumu hiyo alisema kwamba anajipanga kukata rufaa akiahidi kuendeleza mapambano.
Awali waendesha mashtaka walitaka Rubiales afungwe jela kwa tukio hilo ambalo liliibua mijadala ya udhalilishaji jinsia na haki za wanawake ingawa mwenyewe alidai kwamba Jenni alikubali kupigwa busu.
Jaji mmoja wa mahakama hiyo alisema anauamini ushahidi uliotolewa na Jenni kwa kudai kwamba hakukuwa na makubaliano kati yake na Rubiales kwenye tukio zima la kupigwa busu mdomoni.
Jaji huyo hata hivyo alipinga suala la ubabe au vitisho vya aina yoyote kutumika katika tukio hilo na hivyo hakuona uhalali wowote wa kumpa Rubiales adhabu ya kifungo cha jela.
Rubiales pia ametakiwa kutomsegelea Jenni kwa umbali wa mita 200, pamoja na kutozungumza naye kwa mwaka mmoja.


Wakati kesi ikiendelea, Jenni alisema busu alilopigwa bila ridhaa yake lilimfanya akose raha katika siku ambayo ilikuwa ya furaha ya maisha yake wakati wachezaji wenzake walisema kwamba mwenzao alilia na kujiona mnyonge kwa saa na siku kadhaa.
Katika hatua nyingine Watuhumiwa wengine watatu waliodaiwa kuhusika kwa kutoa vitisho na ushawishi ili suala hilo lisifike mbali wote wamefutiwa mashtaka na kuachiwa huru.
Watuhumiwa hao ni aliyekuwa kocha timu ya wanawake ya Hispania, Jorge Vilda, mkurugenzi wa michezo wa timu ya soka ya wanaume ya Hispania, Albert Luque na mkurugenzi wa masoko wa Shirikisho la Soka Hispania, Ruben Rivera.
Baada ya hukumu kutolewa Chama cha Wanasoka Hispania (AFE) kimesema kwamba hukumu hiyo ni hatua muhimu katika kulinda haki za wanawake na kupigania michezo ambayo haitokuwa na unyanyasaji na ubaguzi.

The post Aliyembusu mchezaji mdomoni akutwa na hatia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/20/aliyembusu-mchezaji-mdomoni-akutwa-na-hatia/feed/ 0
Aliyempiga busu mchezaji adai aliomba kabla https://www.greensports.co.tz/2025/02/11/aliyempiga-busu-mchezaji-adai-aliomba-kabla/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/11/aliyempiga-busu-mchezaji-adai-aliomba-kabla/#respond Tue, 11 Feb 2025 19:13:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13007 Madrid, HispaniaAliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales ameiambia mahakama moja ya Hispania kuwa alimuomba kumpiga busu mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso kabla ya kufanya tendo hilo.Rubiales aliingia matatani kwa kumpiga busu mdomoni Jenni katika shamrashamra za kutoa tuzo kwa wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania […]

The post Aliyempiga busu mchezaji adai aliomba kabla first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales ameiambia mahakama moja ya Hispania kuwa alimuomba kumpiga busu mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso kabla ya kufanya tendo hilo.
Rubiales aliingia matatani kwa kumpiga busu mdomoni Jenni katika shamrashamra za kutoa tuzo kwa wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 2023.
Sakata hilo lilikuwa mahakamani leo Jumanne ambapo mbali na Rubiales, viongozi wengine watatu wanatuhumiwa kwa kosa la kutaka busu ambalo Rubiales alimpiga Jenni lionekane ni tukio la kawaida na kupuuzwa.
Katika sakata hilo, Rubiales pia anatuhumiwa kwa udhalilishaji wa kijinsia pamoja na wenzake watatu wanaodaiwa kumshawishi, Jenni amtetee Rubiales.
Watuhumiwa hao watatu ni kocha wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake Hispania, Jorge Vilda, mkurugenzi wa zamani wa michezo wa timu ya taifa ya wanaume ya Hispania, Albert Luque na mkurugenzi wa masoko wa Shirikisho la Soka Hispania, Ruben Rivera.
“Nina hakika alinipa ruhusa, kwa wakati ule lilikuwa jambo ambalo ni la kawaida,” alisema Rubiales kuiambia mahakama.
Alipoulizwa kama ana kawaida ya kuwabusu watu kwenye midomo, Rubiales alisema kwamba kwa tukio lilivyokuwa na kutokana na ukweli kwamba amekuwa akimjua Jenni kwa muda mrefu ilimhalalishia kufanya alichokifanya.
Rubiales pia alifafanua kwamba Kombe la Dunia huwa hawashindi kila siku na angeweza kufanya hivyo hata kwa mchezaji wa kiume au hata kwa mmoja wa watoto wake.
Kwa upande wake Jenni alisema hakutoa ruhusa kwa Rubiales kumpiga busu mdomoni wakati Rubiales amekana kufanya kosa lolote na kusisitiza kwamba alichokifanya kilikuwa na ridhaa ya Jenni.
Baada ya tukio la busu hilo, Rubiales alijikuta akisakamwa hadi akalazimika kujiuzulu nafasi ya urais kwenye shirikisho la soka na kufungiwa na Fifa kwa miaka mitatu.
Katika hoja zake za awali, Jenni alisema baada ya kupigwa busu alijiona aliyedharauliwa na kwamba busu hilo lilimtoa katika tukio la furaha ya maisha yake baada ya Hispania kushinda Kombe la Dunia.
Waendesha mashtaka katika shauri hilo wanataka Rubiales afungwe jela kwa miaka miwili na nusu na kutozwa faini ya Dola 51,000 pamoja na kupigwa marufusu kujihusisha na shughuli za michezo.
Kuhusu watuhumiwa wengine watatu, waendesha mashtaka hao wanataka wafungwe jela kwa mwaka mmoja na nusu kwa kila mmoja.

The post Aliyempiga busu mchezaji adai aliomba kabla first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/11/aliyempiga-busu-mchezaji-adai-aliomba-kabla/feed/ 0
Jaji ataka aliyembusu mchezaji ashitakiwe https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/jaji-ataka-aliyembusu-mchezaji-ashitakiwe/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/jaji-ataka-aliyembusu-mchezaji-ashitakiwe/#respond Fri, 26 Jan 2024 20:29:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9461 Madrid, HispaniaJaji mmoja wa Mahakama Kuu ya Hispania ametaka aliyekuwa kiongozi wa soka nchini humo, Luis Rubiales ashitakiwe kwa kitendo cha kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso.Rubiales alimshika shingoni Jenni na kumpiga busu la mdomoni wakati wa utoaji tuzo baada ya Hispania kuibwaga England na kubeba Kombe […]

The post Jaji ataka aliyembusu mchezaji ashitakiwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Jaji mmoja wa Mahakama Kuu ya Hispania ametaka aliyekuwa kiongozi wa soka nchini humo, Luis Rubiales ashitakiwe kwa kitendo cha kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso.
Rubiales alimshika shingoni Jenni na kumpiga busu la mdomoni wakati wa utoaji tuzo baada ya Hispania kuibwaga England na kubeba Kombe la Dunia la Wanawake Agosti mwaka jana katika mechi ya fainali iliyopigwa mjini Sydney, Australia.
Kwa mujibu wa jaji huyo, upo ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi hiyo huku akitaja kitendo hicho kuwa hakikuwa na maridhiano baina ya Jenni na Rubiales.
Awali waendesha mashitaka walimshitaki Rubiales kwa kosa la udhalilishaji kijinsia na ubabe ambapo adhabu yake inaweza kuwa ni faini au kifungo cha jela miaka minne.
Tukio hilo pia limewaingiza matatizoni vingozi wengine watatu wa timu ya soka ya wanawake ya Hispania kuanzia aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Jorge Vilda, meneja masoko, Ruben Rivera na mkurugenzi wa michezo wa timu ya wanaume ya Hispania, Albert Luque.


Watatu hao kwa pamoja wanatuhumiwa kwa kumshawishi Jenni kuueleza umma kuwa busu alilopigwa lilitokana na ridhaa yake na kwa mujibu wa jaji huyo, watu hao watatu nao wanapaswa kushitakiwa.
Rubiales aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania awali alisimamishwa na Fifa kwa siku 90 licha ya kukana kufanya kosa lolote akidai Jenni aliridhia kupigwa busu hilo, baadaye alilazmika kujiuzulu uongozi baada ya kusakamwa kila kona.
Jenni ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji nyota wa timu ya Hispania, alinukuliwa akisema kwamba kitendo alichofanyiwa na Rubiales hakikubaliki na kuahidi kuitafuta haki.

The post Jaji ataka aliyembusu mchezaji ashitakiwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/jaji-ataka-aliyembusu-mchezaji-ashitakiwe/feed/ 0
Aliyepigwa busu aachwa timu ya taifa https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/aliyepigwa-busu-aachwa-timu-ya-taifa/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/aliyepigwa-busu-aachwa-timu-ya-taifa/#respond Wed, 20 Sep 2023 08:52:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7801 Madrid, HispaniaMshambuliaji wa timu ya taifa ya Hispania aliyepigwa busu mdomoni, Jenni Hermoso hayumo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichotajwa hivi karibuni ingawa kocha mpya wa timu hiyo, Montse Tome amesema wako pamoja na mchezaji huyo.Jenni alipigwa busu na aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales baada ya Hispania kubeba Kombe la […]

The post Aliyepigwa busu aachwa timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Hispania aliyepigwa busu mdomoni, Jenni Hermoso hayumo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichotajwa hivi karibuni ingawa kocha mpya wa timu hiyo, Montse Tome amesema wako pamoja na mchezaji huyo.
Jenni alipigwa busu na aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales baada ya Hispania kubeba Kombe la Dunia kwa kuichapa England bao 1-0 katika mechi iliyopigwa Agosti 20 mwaka huu.
Mchezaji huyo ameachwa katika timu hiyo ingawa wachezaji 21 kati ya 23 waliokuwa na timu ya Hispania iliyobeba Kombe la Dunia wamo katika kikosi hicho kipya.
Sakata la mchezaji huyo kupigwa busu lilimfanya Rubiales ajiuzulu licha ya awali kugoma kwa madai kwamba alimpiga busu mchezaji huyo baada ya kuwa na furaha isiyo kifani lakini baadaye alibadili uamuzi na kuamua kujiuzulu.
Kikosi hicho kilitangazwa Ijumaa iliyopita na kocha mpya wa timu hiyo, Montse Tome ambaye ni kocha wa kwanza mwanamke wa timu hiyo akichukua nafasi ya Jorge Vilda anayetajwa kuwa mshirika wa karibu wa Rubiales.

“Tuko pamoja na Jenni, tunaamini namna bora zaidi ya kumlinda ni kwa kufanya hivyo, Jenni ni mwenzetu, tunamtegemea,” alisema Tome.


Uteuzi wa timu hiyo umekuja huku kukiwa na mgomo wa wachezaji waliotangaza kutokuwa tayari kuichezea timu hiyo wakitaka Rubiales ajiuzulu pamoja na kufanyika mabadiliko ya ndani kwenye idara mbalimbali za REEF.
Baadaye REEF ilitoa taarifa ya kuwataka wachezaji hao kufuta mgomo huo na kuendelea kuichezea timu ya taifa watakapotakiwa kufanya hivyo.
Wachezaji wengine wanawake wa timu hiyo, Mapi Leon na Patri Guijarro wanaoichezea Barcelona ambao hawakuwamo katika kikosi cha Hispania kilichoshiriki fainali za Kombe la Dunia baada ya kuandika barua ya wazi ya kutotaka kufanya kazi chini ya kocha wa awali, Vilda nao wamo katika kikosi kipya.
Akizungumzia uamuzi wa kuwaita wachezaji hao, Tome alisema, “Ni mwanzo wa awamu mpya, muda unaenda mbele, hakuna kilicho nyuma yetu na hakika tunataka kuungana na wachezaji hawa.”
Hispania katika mechi za Nations Ligi itaumana na timu ya Sweden katika mechi itakayopigwa Septemba 22 na kufuatiwa na mechi nyingine dhidi ya Switzerland itakayopigwa Septemba 26.

The post Aliyepigwa busu aachwa timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/aliyepigwa-busu-aachwa-timu-ya-taifa/feed/ 0