Fred Minziro – Greensports Site: Habari za michezo na burudani Tanzania na Ulimwenguni. https://www.greensports.co.tz Michezo na burudani ni zaidi ya ajira Tue, 21 Nov 2023 16:17:34 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.5.5 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Fred Minziro – Greensports Site: Habari za michezo na burudani Tanzania na Ulimwenguni. https://www.greensports.co.tz 32 32 Minziro akubali kuondoka Prisons lakini… https://www.greensports.co.tz/2023/11/21/minziro-akubali-kuondoka-prisons-lakini/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/21/minziro-akubali-kuondoka-prisons-lakini/#respond Tue, 21 Nov 2023 16:11:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8563

Na mwandishi wetu
Aliyekuwa kocha mkuu wa Tanzania Prisons, Fred Minziro amesema amekubaliana na uamuzi wa kumuondoa katika kikosi hicho ingawa amekiri kuondolewa kwenye kipindi ambacho si sahihi.
Minziro ameieleza hayo GreenSports baada ya leo Jumanne uongozi wa Tanzania Prisons kuweka wazi kusitisha mkataba wa mwaka mmoja walioingia na kocha huyo mwanzoni mwa msimu huu kwa manufaa makubwa ya timu hiyo.
“Nimepewa barua jana ya kusitisha mkataba wetu na sasa naelekea nyumbani Dar es Salaam lakini kuna vitu kama maslahi yangu ya kuvunja mkataba bado sijamalizana nao kwa hiyo tutakapimalizana kwenye stahiki zangu hapo ndio tutakuwa tumekamilisha taratibu za kuachana kabisa.

“Ila pia kabla ya kunipa barua ya kusitisha mkataba, nilikutana na uongozi kuwaeleza juu ya maendeleo ya timu kwa ujumla na niliwaeleza kwamba kuna mchakato wa mabadiliko unakamilika muda si mrefu maana timu inaonekana inavyobadilika lakini ndio hivyo nafikiri wameamua wanachoona sahihi,” alisema Minziro.


Kocha huyo ambaye msimu uliopita alikuwa akiinoa Geita Gold amesema kwa sasa hahitaji kuzungumza mengi zaidi anahitaji kupumzika na kuangalia anamalizana vipi kimaslahi na uongozi wa timu hiyo inayoshika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 7 baada ya mechi tisa.
Msimu huu Prisons inakuwa timu ya saba kuachana na kocha wake baada ya Simba, Namungo, Mtibwa Sugar, Ihefu, Singida Fountain Gate na Coastal Union kabla hata ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/21/minziro-akubali-kuondoka-prisons-lakini/feed/ 0
Minziro aipania Polisi Tanzania https://www.greensports.co.tz/2023/01/18/minziro-aipania-polisi-tanzania/ https://www.greensports.co.tz/2023/01/18/minziro-aipania-polisi-tanzania/#respond Wed, 18 Jan 2023 20:45:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4802

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro ameeleza amejiandaa vilivyo kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mechi ya keshokutwa dhidi ya Polisi Tanzania ili kuendelea kupigania ndoto za timu hiyo katika mechi zilizobaki za ligi.
Geita inatarajia kuwa mwenyeji katika mchezo huo unaotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Nyankumbu, Geita.
Akizungumza na GreenSports, Minziro alisema anahitaji kuendelea kupata ushindi kama ilivyokuwa kwenye mechi yao ya mwisho walipoifunga Dodoma Jiji mabao 2-0 ingawa anaamini mechi ya Polisi itakuwa ngumu zaidi.
“Mechi ni ngumu na ligi ni ngumu pia lakini tunaendelea kujiweka sawa na tuko tayari kwa ajili ya Polisi, hakuna timu inayotaka kupoteza katika kipindi hiki ndiyo maana nasema ligi ni ngumu na tunafahamu hilo.

“Mara ya mwisho tulipata ushindi dhidi ya Dodoma, tunahitaji kuendelea na wimbi la ushindi japo sio kitu rahisi lakini kwa kuwa tunahitaji kupigania ndoto za Geita msimu huu inatupasa kuendelea kupambana kupata pointi tatu katika kila mechi,” alisema Minziro.


Geita inakutana na Polisi iliyo chini ya Mwinyi Zahera ikiwa nafasi ya tano na pointi 27 wakati Polisi ikiburuza mkia kwenye nafasi ya 16 na pointi zake 14.
Kocha wa Polisi, Mwinyi Zahera amenukuliwa hivi karibuni akijiaminisha kuwa timu hiyo haitoshuka daraja licha ya kuwa katika nafasi mbaya wakati ligi ikielekea ukingoni.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/01/18/minziro-aipania-polisi-tanzania/feed/ 0