Flick - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 29 May 2024 12:38:13 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.7.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Flick - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Rasmi, Flick kocha mkuu Barca https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/rasmi-flick-kocha-mkuu-barca/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/rasmi-flick-kocha-mkuu-barca/#respond Wed, 29 May 2024 12:38:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11159 Barcelona, HispaniaKlabu ya Barcelona au Barca hatimaye imemteua rasmi kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Hansi Flick kuwa kocha mkuu kwa mkataba wa miaka miwili.Flick ambaye pia amewahi kuwa kocha wa timu ya Bayern Munich pia ya Ujerumani, Septemba mwaka jana alitimuliwa timu ya taifa ya Ujeumani na sasa anachukua nafasi ya […]

The post Rasmi, Flick kocha mkuu Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Klabu ya Barcelona au Barca hatimaye imemteua rasmi kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Hansi Flick kuwa kocha mkuu kwa mkataba wa miaka miwili.
Flick ambaye pia amewahi kuwa kocha wa timu ya Bayern Munich pia ya Ujerumani, Septemba mwaka jana alitimuliwa timu ya taifa ya Ujeumani na sasa anachukua nafasi ya Xavi ambaye wiki iliyopita alitimuliwa Barca.
Hadi kuteuliwa kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani, Flick alipata mafanikio akiwa na Bayern hasa mwaka 2020 alipoiwezesha kubeba mataji matatu ‘treble’ ambayo ni Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji wa Barca, Robert Lewandowski, 35, anamjua vizuri Flick kwani walikuwa naye katika klabu ya Bayern Munich kwa misimu miwili iliyokuwa na mafanikio.
Mara baada ya kutimuliwa Barca, Xavi alinukuliwa akisema kwamba kocha atakayechukua nafasi yake atapata tabu sana kwa kuwa kazi ya kuinoa timu hiyo ni ngumu na ina mambo mengi.
Mafanikio pekee ambayo Xavi ameyapata akiwa na Barca ni kubeba taji la La Liga msimu uliopita ingawa msimu huu umekuwa mgumu kwake baada ya timu hiyo kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili nyuma ya mahasimu wao Real Madrid kwa tofauti ya pointi 10.

The post Rasmi, Flick kocha mkuu Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/rasmi-flick-kocha-mkuu-barca/feed/ 0
Hansi Flick awasili Barcelona https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/hansi-flick-awasili-barcelona/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/hansi-flick-awasili-barcelona/#respond Wed, 29 May 2024 06:22:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11148 Barcelona, HispaniaKocha mpya mtarajiwa wa Barca, Hansi Flick amewasili jijini Barcelona ili kusaini mkataba na kukabidhiwa rasmi majukumu ya kuinoa timu hiyo baada ya kutimuliwa kwa Xavi Hernandez.Flick, 59, amekuwa bila kazi tangu Septemba mwaka jana alipotimuliwa timu ya taifa ya Ujerumani na katika siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na Barca ili kumrithi Xavi.Kocha […]

The post Hansi Flick awasili Barcelona first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Kocha mpya mtarajiwa wa Barca, Hansi Flick amewasili jijini Barcelona ili kusaini mkataba na kukabidhiwa rasmi majukumu ya kuinoa timu hiyo baada ya kutimuliwa kwa Xavi Hernandez.
Flick, 59, amekuwa bila kazi tangu Septemba mwaka jana alipotimuliwa timu ya taifa ya Ujerumani na katika siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na Barca ili kumrithi Xavi.
Kocha huyo aliwasili Barcelona Jumanne akiwa na wakala wake Pini Zahavi ili kukamilisha taratibu za kimkataba kabla ya kuanza majukumu hayo mapya huku zikiwapo habari kuwa atasani mkataba wa miaka miwili.
Flick ambaye pia amewahi kuinoa Bayern Munich, habari za kujiunga kwake na Barca zilianza kusikika Januari mwaka huu baada ya Xavi kutangaza kwamba ataachana na timu hiyo baada ya msimu huu.
Aprili mwaka huu mambo yalibadilika baada ya Xavi kubadili uamuazi wa awli na kuamua kuwa angeendelea kuinoa timu hiyo hadi mkataba wake utakapofikia ukomo mwaka 2025.
Mambo hata hivyo yalibadilika kwa mara nyingine baada ya Rais wa Barca, Joan Laporta kuamua kumtimua Xavi sababu ikidaiwa kuwa ni kauli ya kocha huyo kwamba timu hiyo haitoweza kushindana na timu kubwa Ulaya kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi.
Baada ya hapo, Laporta alimgeukia Flick ambaye inadaiwa alikuwa akimpigia hesabu tangu mwaka 2021 ili achukue nafasi ya Ronald Koeman lakini Flick ambaye wakati huo alikuwa akiinoa Bayern tayari alikuwa na makubaliano na timu ya taifa ya Ujerumani.
Moja ya mafanikio ya kukumbukwa ya Flick ni yale ya mwaka 2020 akiwa Bayern alipoiwezesha timu hiyo kubeba mataji matatu makubwa, mawili ya Ujerumani pamoja na lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

The post Hansi Flick awasili Barcelona first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/hansi-flick-awasili-barcelona/feed/ 0