Clatous CHama – Greensports Site: Habari za michezo na burudani Tanzania na Ulimwenguni. https://www.greensports.co.tz Michezo na burudani ni zaidi ya ajira Wed, 01 May 2024 20:05:48 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.7.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Clatous CHama – Greensports Site: Habari za michezo na burudani Tanzania na Ulimwenguni. https://www.greensports.co.tz 32 32 Chama afungiwa mechi tatu https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/chama-afungiwa-mechi-tatu/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/chama-afungiwa-mechi-tatu/#respond Wed, 01 May 2024 20:05:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10817

Na mwandishi wetu
Kiungo wa Simba, Clatous Chama amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kumkanyaga makusudi Nickson Kibabage wa Yanga wakati timu hizo zilipokutana Aprili 20, mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi cha Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi.
Mbali na Chama pia Simba imetozwa faini ya Sh milioni moja huku Yanga ikitozwa faini ya Sh milioni tano kwa makosa ya kuingia kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kupitia milango isiyo rasmi kuelekea katika mchezo huo ulioisha kwa Yanga kushinda mabao 2-1.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa baada ya kuwasili uwanjani, timu hizo hazikutumia mlango rasmi kuingia vyumbani, ikielezwa kuwa Yanga imetenda kosa hilo katika michezo zaidi ya minne.
Imeelezwa kuwa timu hiyo imekuwa ikifanya hivyo katika michezo inayozikutanisha klabu hiyo ndani ya misimu mitatu kuanzia msimu wa 2021-22, 2022-23 na 2023-24 ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kuhusiana na sakata la vyumbani, kamati hiyo inasubiri taarifa ya daktari wa mchezo huo ambaye alichukua sampuli ya hewa kutoka vyumba hivyo viwili kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi.
Inadaiwa kwamba wachezaji wa timu hizo wameshindwa kuingia kwenye vyumba hivyo kutokana na kuwemo kwa harufu isiyo ya kawaida.
Naye, mshambuliaji wa Azam FC, Abdul Selemani ‘Sopu’ ametozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kuchukua taulo na maji ya mlinda mlango wa klabu ya Mashujaa FC kisha kuvitupa mbali.
Klabu ya Mashujaa imetozwa faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Vitendo hivyo vinadaiwa kufanywa katika mchezo wao huo na Azam FC, wakati wakifanya mazoezi ya mwisho siku moja kabla ya mechi.
Imeainishwa kuwa wachezaji na viongozi wa klabu hiyo walionekana wakimwaga vitu vyenye asili ya unga kwenye viti vya mabenchi ya ufundi na kuweka chupa inayodaiwa kuwa na karatasi nyeupe ndani yake.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/chama-afungiwa-mechi-tatu/feed/ 0
Chama ajipa matumaini ya ubingwa https://www.greensports.co.tz/2024/02/16/chama-ajipa-matumaini-ya-ubingwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/16/chama-ajipa-matumaini-ya-ubingwa/#respond Fri, 16 Feb 2024 19:20:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9767

Na mwandishi wetu
Licha ya Simba kuachwa kwa tofauti ya pointi nne na mahasimu wao Yanga wanaoongoza Ligi Kuu NBC, kiungo wa timu hiyo, Clatous Chama amesema bado wako kwenye mbio za kuwania ubingwa msimu huu wa 2023-24.
Chama alisema hayo baada ya kufunga bao muhimu lililoisaidia timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 jana ugenini dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Kiungo huyo ambaye amefunga mabao mawili na kutoa ‘asisti’ mbili katika mechi nne za Simba tangu arejee baada ya kuitumikia Zambia kwenye Afcon, alisema mzunguko wa kwanza haukuwa mbaya.
Alifafanua kwamba walianza kwa kuchechemea na kufanya makosa madogo lakini bado wanaendelea kujitafuta na kurekebisha makosa ili waimarike na kutimiza malengo yao.
“Nafasi ya pili siyo mbaya, wanaoongoza wametuzidi pointi nne, tutapambana tuendelee kuona tutafika wapi lakini malengo yetu ni kushinda ubingwa wa ligi kuu.

“Hivi sasa siangalii sana ufungaji bora wa ligi kuu, muhimu ni timu kwanza ifanye vizuri halafu mimi. Kutakuwa hakuna umuhimu wa kuwa mfungaji bora halafu timu haijabeba ubingwa,” alisema Chama.


Simba iko nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 36 baada ya kushuka uwanjani mara 15 ikiwa imeshinda michezo 11, sare tatu na kufungwa mechi moja.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/16/chama-ajipa-matumaini-ya-ubingwa/feed/ 0
Chama aibua maswali baada ya kusimamishwa https://www.greensports.co.tz/2023/12/22/chama-aibua-maswali-baada-ya-kusimamishwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/22/chama-aibua-maswali-baada-ya-kusimamishwa/#respond Fri, 22 Dec 2023 16:36:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8983

Na Hassan Kingu
Uamuzi wa Simba kumsimamisha kiungo wake, Clatous Chota Chama umeacha maswali miongoni mwa mashabiki kuhusu hatma ya mchezaji huyo huku wengine wakikimbilia kumhusisha na Yanga.
Uongozi wa Simba jana Alhamisi ulitoa taarifa ya kusimamishwa kwa wachezaji wawili Chama pamoja na Nassor Kapama kwa kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu wa wachezaji hao.
Taarifa hiyo hata hivyo haikufafanua ni vitendo gani vya utovu wa nidhamu vilivyofanywa na wachezaji hao, badala yake ilisisitiza juu ya watumishi wa klabu ya Simba kuzingatia misingi ya maadili na nidhamu.
Baadhi ya mijadala inayoendelea kisikika hasa mitandaoni imekuwa ni kuhusu Chama pekee, hatma yake, nini hasa alichokifanya, kwa nini hakuvumiliwa na mengineyo.
Moja ya hoja ambayo imeendelea kujadiliwa ni kwamba uamuzi wa kumsimamisha Chama ni wa muda tu, ni kama vile klabu inatingisha kiberiti lakini mchezaji huyo atajadiliwa na kamati ya nidhamu kama ilivyoelezwa na suluhisho litafikiwa na mwishowe ataendelea kuitumikia Simba.
Pia ipo hoja kwamba mchezaji huyo amekuwa na tatizo la utovu wa nidhamu kwa muda mrefu na amekuwa akivumiliwa na makocha wake lakini kocha wa sasa, Abdelhak Benchikha ameshindwa kumvumilia.
Katika hali ya kawaida ni vigumu kwa Simba kuruhusu au kukubali kuachana na mchezaji wa hadhi ya Chama ambaye tayari amedhihirisha umuhimu wake kwenye Ligi Kuu NBC pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba inapigania kulibeba taji la Ligi Kuu NBC lakini pia inapambana na ipo katika hatua nzuri kwenye mbio za kuwania kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kote huko nafasi na mchango wa Chama unahitajika.
Ujasiri wa kuachana na mchezaji huyo katika mazingira yoyote yale bado hauwezi kuwa na nafasi na kama italazimika kufanya hivyo basi tatizo la utovu wa nidhamu analodaiwa kulifanya Chama linaweza kuwa kubwa na ambalo halivumiliki.
Matatizo ya utovu wa nidhamu wanayohusishwa nayo wachezaji mara nyingi yanakuwa ya kufanana kama vile nidhamu ya kutojali muda, kutofika mazoezini kwa wakati au kutofika kabisa na mara nyingi hutokea mara moja moja hivyo kamwe hayawezi kuwa sababu ya klabu kuachana na mchezaji tena mchezaji mwenyewe Chama.
Hadithi inayosikika mitandaoni ya kuharakia kumhusisha Chama na Yanga huenda imetengenezwa na Yanga kwa nia ya kuwavuruga Simba lakini bado si jambo rahisi kwa Simba kukubali kuachana na Chama au kuwa tayari kumuona Chama akielekea Yanga.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/22/chama-aibua-maswali-baada-ya-kusimamishwa/feed/ 0
Chama afunga bao bora Ligi ya Mabingwa https://www.greensports.co.tz/2023/03/22/chama-afunga-bao-bora-ligi-ya-mabingwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/22/chama-afunga-bao-bora-ligi-ya-mabingwa/#respond Wed, 22 Mar 2023 19:24:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5558

Na mwandishi wetu
Kiungo wa Simba, Clatous Chama ametangazwa mfungaji wa bao bora la mzunguko wa tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika huku mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele akiingia katika kinyang’anyiro cha kuwania bao bora la mzunguko wa tano wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Mayele aliyefunga bao lake la tatu msimu huu kwenye michuano hiyo ameingia kupitia bao alilofunga Jumapili iliyopita dhidi ya US Monastir waliposhinda mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Mabao mengine mawili yanayoshindanishwa ni la Ousmane Kamissoko wa Real Bamako dhidi ya TP Mazembe waliposhinda 2-0 na lingine la Mydo Nakouho wa DC Motema Pembe walipopoteza mbele ya Asec Mimosas kwa mabao 2-1.
Chama ametangazwa mshindi kupitia bao alilofunga kwa adhabu ndogo dakika ya 10 walipokuwa wakicheza na Horoya AC Jumamosi iliyopita katika ushindi wao mnono wa 7-0, Uwanja wa Mkapa.
Katika kinyang’anyiro hicho Chama ambaye amewaangusha Percy Tau wa Al Ahly, Zakaria Draoui (Zamalek), Soufiane Benjdida (Vipers) na Sadio Kanoute (Simba) kwenye bao bora, ameshindwa kwenye kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa wiki wa michuano hiyo na kutua kwa Mahmoud Kahraba wa Al Ahly.
Mbali na Kahraba na Chama wengine waliokuwa wakiwania mchezaji bora wa wiki ni Sadio Kanoute na Percy Tau. Al Ahly iliifunga Cotton mabao 4-0 wikiendi iliyopita.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/22/chama-afunga-bao-bora-ligi-ya-mabingwa/feed/ 0
Chama kidedea CAF https://www.greensports.co.tz/2023/03/15/chama-kidedea-caf/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/15/chama-kidedea-caf/#respond Wed, 15 Mar 2023 16:42:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5504

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama ameibuka kidedea na kuwa mchezaji bora wa wiki wa mechi ya nne ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ushindi huo wa Chama ulitangazwa usiku wa kuamkia leo Jumatano na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), akiwabwaga Walid Sabar wa Raja Casablanca, Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns na Ahmed Zizo wa Zamalek.
Chama raia wa Zambia alipata ushindi huo kutokana na kura zilizokuwa zikipigwa kwa takriban siku tatu mfululizo kwenye ukurasa rasmi wa michuano hiyo wa mtandao wa kijamii wa Twitter.
Kiungo huyo alishinda kwa kura asilimia 68.7, Shalulile akipata asilimia 14.9 wakati Sabbar akiokota kura 10.9% na Zizo akiambulia 5.6%.
Licha ya wachezaji wengine kuonesha kiwango kuzisaidia timu zao kupata ushindi kwenye mechi za wiki ya nne lakini Chama alielezwa kuonesha kiwango bora zaidi katika mchezo wao dhidi ya Vipers na kufunga bao pekee la ushindi kwenye mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Pia, Chama alijumuishwa kwenye mabao matano bora yaliyofungwa wiki hiyo, yumo kwenye kikosi bora cha wiki sanjari na beki wa kulia wa Wekundu hao, Shomari Kapombe.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/15/chama-kidedea-caf/feed/ 0