Aziz Ki - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 11 Jul 2024 08:19:20 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.7.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Aziz Ki - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Aziz Ki amaliza utata https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/aziz-ki-amaliza-utata/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/aziz-ki-amaliza-utata/#respond Thu, 11 Jul 2024 08:19:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11584 Na mwandishi wetuStephanie Aziz Ki hatimaye amemaliza utata baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga na hivyo kumaliza mijadala na vijembe miongoni mwa mashabiki wa soka nchini.Mashabiki wa Yanga na Simba katika siku za karibuni wamekuwa wakilumbana na kucharurana kuhusu hatma ya mchezaji huyo kama angeendelea kuichezea Yanga au angeachana na timu […]

The post Aziz Ki amaliza utata first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Stephanie Aziz Ki hatimaye amemaliza utata baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga na hivyo kumaliza mijadala na vijembe miongoni mwa mashabiki wa soka nchini.
Mashabiki wa Yanga na Simba katika siku za karibuni wamekuwa wakilumbana na kucharurana kuhusu hatma ya mchezaji huyo kama angeendelea kuichezea Yanga au angeachana na timu hiyo.
Mjadala huo ulizidi kuwa mkubwa baada ya mwenyekiti wa Yanga, Hersi Said kuweka wazi siku chache zilizopita kuwa mchezaji huyo hakuwa amesaini mkataba mpya baada ya ule wa awali kufikia ukomo.
Ukimya wa Aziz Ki na kauli ya Hersi kwa pamoja vilizidisha mijadala mitandaoni na vijiweni huku mashabiki wa Yanga wakionekana kushambuliwa kwa kupigwa vijembe lakini kwa sasa yote hayo yamekwisha.
Aziz Ki ambaye amemaliza msimu uliopita w 2023-24 akiwa mfungaji bora, zilikuwapo habari kwamba alikuwa akitakiwa na klabu kadhaa za Afrika hapo hapo ikadaiwa Simba nao walikuwa wakifuatilia kwa karibu maendeleo yake ili wamchukue kama angaitema Yanga.
Yote hayo yamekwisha na kwa sasa mashabiki wa Yanga wanajiona washindi wakitembea vifua mbele baada ya kushinda vita ya mitandaoni na vijiweni kuhusu hatma ya Aziz Ki.
Vyanzo vya habari vya klabu ya Yanga Jumatano hii vilitawaliwa na habari ya kiungo huyo mshambuliaji kwa kuuhakikishia umma kwamba msimu ujao huduma ya mchezaji huyo itaendelea kuonekana mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam yalipo makao makuu ya klabu ya Yanga.
“Nimeamua kuendelea kubaki Yanga ili kukamilisha majukumu katika klabu hii,” ilisomeka taarifa ya mchezaji huyo huku akisisitiza shauku yake ya kuuanza msimu ujao wa 2024-25.

The post Aziz Ki amaliza utata first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/aziz-ki-amaliza-utata/feed/ 0
Aziz Ki aibua sintofahamu https://www.greensports.co.tz/2024/06/05/aziz-ki-aibua-sintofahamu/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/05/aziz-ki-aibua-sintofahamu/#respond Wed, 05 Jun 2024 18:10:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11239 Na mwandishi wetuKinara wa mabao Ligi Kuu NBC, Stephane Aziz Ki ameibua sintofahamu mitandaoni baada ya kuwashukuru mashabiki, wachezaji wenzake na wadau wengine wa timu hiyo.Aziz Ki ameshukuru kwa muda wote wa msimu huu kwa namna walivyopambana na kuaminiana ingawa salamu hizo baadhi ya mashabiki wamezipa tafsiri ya kuwa mchezaji huyo anawaaga.Kiungo huyo mshambuliaji raia […]

The post Aziz Ki aibua sintofahamu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kinara wa mabao Ligi Kuu NBC, Stephane Aziz Ki ameibua sintofahamu mitandaoni baada ya kuwashukuru mashabiki, wachezaji wenzake na wadau wengine wa timu hiyo.
Aziz Ki ameshukuru kwa muda wote wa msimu huu kwa namna walivyopambana na kuaminiana ingawa salamu hizo baadhi ya mashabiki wamezipa tafsiri ya kuwa mchezaji huyo anawaaga.
Kiungo huyo mshambuliaji raia wa Burkina Faso ameeleza hayo leo Jumatano katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na kufafanua hisia zake katika kufanikisha ndoto zake.
“Kila kitu kiliwezekana, shukrani kwenu wachezaji wenzangu, wafanyakazi, kamati ya rais na hasa nyinyi mashabiki, wapendwa wangu, familia na pia kwa baraka za Mungu mwema kwa mara nyingine tena asante kwa uaminifu wako, msaada wako, imani yako, umenipa mengi katika msimu wote,” aliandika Aziz aliyefunga mabao 21.
Hata hivyo, andiko hilo kidogo liliibua sintofahamu kwa baadhi ya mashabiki wakihoji namna anavyotoa asante ni kama anataka kuihama timu hiyo.
Punde, Aziz alijibu ‘comment’ hizo na kufafanua: “Nawashukuru kwa sababu ni jambo dogo sana ninaloweza kufanya kuwashukuru nyinyi ambao mnanisaidia kila siku, haimaanishi kwaheri, niko hapa msijali.”

The post Aziz Ki aibua sintofahamu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/05/aziz-ki-aibua-sintofahamu/feed/ 0
Aziz Ki aikumbuka hat trick ya Azam https://www.greensports.co.tz/2024/06/02/aziz-ki-aikumbuka-hat-trick-ya-azam/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/02/aziz-ki-aikumbuka-hat-trick-ya-azam/#respond Sun, 02 Jun 2024 12:39:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11200 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki ameeleza kuwa ‘hat-trick’ (mabao matatu) aliyofunga dhidi ya Azam FC ni bora zaidi kuliko aliyowafunga Prisons kwenye mechi ya mwisho ya kufunga pazia la Ligi Kuu NBC.Mfungaji huyo bora wa ligi kuu msimu huu aliyepachika mabao 21 ameeleza kuwa hat trick ya Azam ilikuwa bora sababu […]

The post Aziz Ki aikumbuka hat trick ya Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki ameeleza kuwa ‘hat-trick’ (mabao matatu) aliyofunga dhidi ya Azam FC ni bora zaidi kuliko aliyowafunga Prisons kwenye mechi ya mwisho ya kufunga pazia la Ligi Kuu NBC.
Mfungaji huyo bora wa ligi kuu msimu huu aliyepachika mabao 21 ameeleza kuwa hat trick ya Azam ilikuwa bora sababu alihitimisha hat-trick hiyo kwa bao la ushindi katika mechi iliyoisha kwa Yanga kutakata kwa mabao 3-2.
“Kwangu bora zaidi ilikuwa dhidi ya Azam sababu tulitangulia kufunga wakachomoa bao, wakaongeza kisha nikafunga tena na kisha nikafunga tena na kupata ushindi, kwangu ushindi ni muhimu zaidi.
“Maana ile ya Prisons ilikuwa ushindi 4-1 na mpaka nafunga bao la mwisho tulikuwa na uhakika wa ushindi, ni tofauti na ile ya Azam maana baada ya wao kufunga bao la pili ilikuwa bado hatuna uhakika lakini nilipofunga la tatu iliibuka furaha kubwa ya uhakika wa pointi tatu,” alifafanua Aziz Ki.
Aziz Ki ambaye ni raia wa Burkina Faso pia amesema hata bao lake bora msimu huu ni bao la tatu alilowafunga Azam kwani sababu kubwa ilikuwa ni namna mashabiki na wadau wao walivyofurahi baada ya mechi ngumu dhidi yao muda wote.

The post Aziz Ki aikumbuka hat trick ya Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/02/aziz-ki-aikumbuka-hat-trick-ya-azam/feed/ 0
Fei ampongeza Aziz Ki https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/fei-ampongeza-aziz-ki/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/fei-ampongeza-aziz-ki/#respond Wed, 29 May 2024 12:36:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11157 Na mwandishi wetuBaada ya kushindwa kunyakua kiatu cha ufungaji bora, kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amempongeza kinara wa mabao Stephane Aziz Ki wa Yanga japo na yeye anafurahia timu yao kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika.Fei Toto aliyemaliza Ligi Kuu NBC akiwa na mabao 19, amempongeza kiungo wa Yanga Aziz Ki aliyefunga mabao […]

The post Fei ampongeza Aziz Ki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya kushindwa kunyakua kiatu cha ufungaji bora, kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amempongeza kinara wa mabao Stephane Aziz Ki wa Yanga japo na yeye anafurahia timu yao kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika.
Fei Toto aliyemaliza Ligi Kuu NBC akiwa na mabao 19, amempongeza kiungo wa Yanga Aziz Ki aliyefunga mabao 21 ambapo Fei pia amekiri kuwa mchezaji huyo alistahili kwa namna ambavyo alipambana.
“Hata kama nimekosa kiatu lakini najisikia vizuri tu, unajua jambo la kwanza ni timu na mengine baadaye. Kwa hiyo nampongeza sana (Aziz Ki) kwa kuwa mfungaji bora na pia tuna furaha tumefuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kama timu.
“Maana jambo la kwanza lilikuwa kufuzu na mengine baadaye, tuangalie hayo baadaye,” alisema Fei aliyejiunga na Azam msimu huu akitokea Yanga.
Fei ambaye pia ametoa pasi za mabao saba, akizidiwa mbili na Kipre Junior (Azam) mwenye tisa ameeleza kuwa anaamini huu ndio msimu wake bora zaidi tangu aanze kucheza Ligi Kuu NBC alipotua Yanga msimu wa 2018-19.

“Niseme kweli, ni wazi huu ndio msimu wangu bora tangu nianze kucheza Ligi ya Tanzania Bara kwa hiyo namshukuru Mungu kwa kumaliza msimu salama salmini bila ya majeraha na najiskia furaha,” alisema Fei.


Fei aliongeza kwamba kwake yeye hiyo ni historia kubwa na la muhimu zaidi ni kujitunza, kufanya mazoezi kwa bidii, kumsikiliza kocha na mambo mengine yataaenda vizuri.

The post Fei ampongeza Aziz Ki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/fei-ampongeza-aziz-ki/feed/ 0
Aziz Ki amfunika Fei Toto https://www.greensports.co.tz/2024/05/28/aziz-ki-amfunika-fei-toto/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/28/aziz-ki-amfunika-fei-toto/#respond Tue, 28 May 2024 19:41:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11142 Na mwandishi wetuKiungo wa Yanga, Stephanie Aziz Ki ameibuka kinara wa mabao Ligi Kuu NBC akimfunika kiungo wa Azam FC, Feisal Salum wakati ndoto za Simba kushika nafasi ya pili katika ligi hiyo zikiota mbawa.Aziz Ki na Feisal au Fei Toto wamekuwa katika mpambano wa kusaka kiatu cha mfungaji bora na kabla ya mechi za […]

The post Aziz Ki amfunika Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo wa Yanga, Stephanie Aziz Ki ameibuka kinara wa mabao Ligi Kuu NBC akimfunika kiungo wa Azam FC, Feisal Salum wakati ndoto za Simba kushika nafasi ya pili katika ligi hiyo zikiota mbawa.
Aziz Ki na Feisal au Fei Toto wamekuwa katika mpambano wa kusaka kiatu cha mfungaji bora na kabla ya mechi za leo Jumanne za kufunga pazia la ligi hiyo, kila mmoja alikuwa na mabao 18.
Mabao ya mechi za leo ndiyo yaliyombeba Aziz Ki na kumfanya amalize ligi hiyo akiwa na mabao 21 baada ya Yanga kuinyuka Prisons mabao 4-1 wakati Fei amefikisha mabao 19 baada ya kufunga bao moja dhidi ya Geita Gold.
Aziz Ki leo amefunga mabao matatu peke yake na hivyo kuondoka na mpira hali ambayo si tu imedhihirisha uwezo wake katika kuzifumania nyavu bali pia amewanyamazisha waliokuwa na fikra kwamba Fei leo angeweza kumpiku kwa mabao.
Fei ambaye amewahi kucheza pamoja na Aziz Ki katika kikosi cha Yanga hata hivyo naye ana kila sababu ya kujivunia mabao aliyofunga msimu huu kwani ndiyo yaliyoiwezesha Azam kushika nafasi ya pili.
Kwa kushika nafasi ya pili, Azam itaungana na Yanga katika ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Simba iliyoangukia nafasi ya tatu itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho pamoja na Coastal Union.
Yanga iliyotwaa taji hilo imemaliza ligi na pointi 80, Simba na Azam zimemaliza kila moja ikiwa na pointi 69, Simba imezipata pointi hizo baada ya kuifunga JKT Tanzania mabao 2-0 na Azam imeilaza Geita Gold mabao 2-0.
Azam imeshika nafasi ya pili kutokana na wastani mzuri wa mabao, imefunga mabao 63 dhidi ya 53 ya Simba wakati Azam pia imefungwa mabao 21, Simba imefungwa mabao 29.
Wakati hali ikiwa hivyo katika nafasi nne za juu, mambo si mazuri kwa Mtibwa Sugar ambayo tayari imeshuka daraja ikiungana na Geita Gold katika mkumbo huo wa kuelekea ligi ya Championship.
Matokeo ya mechi za mwisho za ligi hiyo…
Simba 2-0 JKT Tanzania
Coastal Union 0-0 KMC
Mashujaa FC 3-0 Dodoma Jiji
Ihefu 5-1 Mtibwa Sugar
Yanga 4-1 Prisons
Namungo FC 3-2 Tabora United
Geita Gold 0-2 Azam FC
Singida FG 2-3 Kagera Sugar

The post Aziz Ki amfunika Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/28/aziz-ki-amfunika-fei-toto/feed/ 0
Aziz Ki haondoki Yanga hadi abebe taji Ligi ya Mabingwa https://www.greensports.co.tz/2024/05/27/aziz-ki-haondoki-hadi-abebe-taji-ligi-ya-mabingwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/27/aziz-ki-haondoki-hadi-abebe-taji-ligi-ya-mabingwa/#respond Mon, 27 May 2024 18:46:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11139 Na mwandishi wetuKiungo Mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuihama timu hiyo mpaka atakapohakikisha anatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa Jangwani.Mchezaji huyo raia wa Burkina Faso ameieleza GreenSports kuwa licha ya taarifa za kuhitajika na timu nyingine lakini ifahamike kuwa hawezi kuhama Yanga mpaka atimize ndoto alizonazo […]

The post Aziz Ki haondoki Yanga hadi abebe taji Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuihama timu hiyo mpaka atakapohakikisha anatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa Jangwani.
Mchezaji huyo raia wa Burkina Faso ameieleza GreenSports kuwa licha ya taarifa za kuhitajika na timu nyingine lakini ifahamike kuwa hawezi kuhama Yanga mpaka atimize ndoto alizonazo juu ya timu hiyo.
“Mpaka sasa ni mchezaji wa Yanga, najua kuna timu zinanisubiri, wananihitaji lakini muda wote nawapa nafasi Yanga kwanza na nilikuja hapa kwa sababu tunahitaji kuwa juu Afrika, sasa bado tupo kwenye hiyo ‘project’, kwa hiyo mpaka tutakapoikamilisha.
“Ni mpaka tutakapocheza fainali ya Ligi ya Mabingwa hapa Kwa Mkapa (Uwanja wa Benjamin) kisha nitamfuata Rais (Hersi Said) kuulizia baraka zake za kuondoka. Nachopaswa ni kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa na kushinda ubingwa na Yanga, hii ndio ndoto yangu na ndio misheni yangu, nitashinda hili kombe kabla ya kuondoka naamini hilo,” alihitimisha Aziz Ki.
Nyota huyo aliyejiunga na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast ameonesha kiwango kikubwa mpaka sasa akiwa anaongoza kwenye orodha ya mabao Ligi Kuu NBC akifunga mara 18, akifungana kileleni na kiungo wa Azam FC, Feisal Salum.
Aziz Ki ambaye pia anashika namba mbili kwenye orodha ya waliotoa pasi za mabao akiwa nazo nane baada ya Kipre Junior (Azam) mwenye tisa.
Katika siku za hivi karibuni, Aziz Ki amekuwa akitajwa kuwindwa na vigogo wa Afrika wakiwemo Mamelodi Sundowns, Kaizer Chiefs, Al Ahly na Pyramids ikielezwa wako tayari kutoa kitita kunasa saini ya mchezaji huyo.

The post Aziz Ki haondoki Yanga hadi abebe taji Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/27/aziz-ki-haondoki-hadi-abebe-taji-ligi-ya-mabingwa/feed/ 0
Rais CAF ahalalisha bao la Aziz Ki https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/rais-caf-ahalalisha-bao-la-aziz-ki/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/rais-caf-ahalalisha-bao-la-aziz-ki/#respond Fri, 24 May 2024 19:05:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11110 Na mwandishi wetuRais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe amesema bao la kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini lilikuwa halali.Motsepe amezungumza hayo leo Ijumaa na waandishi wa habari mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar alipokwenda kuhudhuria fainali […]

The post Rais CAF ahalalisha bao la Aziz Ki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe amesema bao la kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini lilikuwa halali.
Motsepe amezungumza hayo leo Ijumaa na waandishi wa habari mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar alipokwenda kuhudhuria fainali za African Schools Football Championship (ASFC) 2024.
“Ngoja niwaambie kitu, nikiwa kama Rais wa Caf ninaipenda klabu iliyopo Africa na nilisema kitu kwa Rais Wallace (Karia, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), tulipokutana baada ya mechi ya Yanga na Mamelodi nilisema nadhani lile ni goli,” alisema Motsepe aliyewahi kuwa Rais wa Mamelodi.

“Ingawa Rais wa Caf hapaswi kutoa maoni kuhusu maamuzi ya waamuzi lakini kwangu binafsi nilivyorudia kuangalia lilikuwa ni goli halali lakini naheshimu sana taratibu zote za maamuzi na tuna jukumu la kutakiwa kulinda na kuheshimu maamuzi ya waamuzi, VAR, mechi kamishna wa michezo kwa afya ya soka letu,” alifafanua Motsepe.


Bao hilo la Aziz Ki lilizusha utata mkubwa wakati Yanga ikicheza mechi yake ya mkondo wa pili wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi uliopigwa Aprili 5, mwaka huu jijini Pretoria.
Baada ya bao hilo ambalo Aziz aliupiga mpira nje ya 18 na kugonga mwamba wa juu na mpira huo kudunda ndani ya mstari wa goli kabla ya kurejea uwanjani, mwamuzi Beida Dahane kutoka nchini Mauritania alikubaliana na maamuzi ya waamuzi wa chumba cha VAR kuwa si bao ambapo mashabiki wengi waliona hayakuwa maamuzi sahihi.
Motsepe pia ameendelea kuzipongeza klabu za Simba na Yanga kwa kuendelea kuonesha mfano mzuri wa mashabiki wanaoenda kuujaza uwanja kwa kusapoti timu zao zinapocheza.

The post Rais CAF ahalalisha bao la Aziz Ki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/rais-caf-ahalalisha-bao-la-aziz-ki/feed/ 0
Kumbe kweli Aziz Ki hajasaini Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/aziz-ki-hajasaini-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/aziz-ki-hajasaini-yanga/#respond Wed, 22 May 2024 20:19:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11081 Na mwandishi wetuHatimaye meneja habari na mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema bado hawajafanikiwa kumuongezea mkataba kiungo wao mshambuliaji, Stephane Aziz Ki.Kamwe pia alisema kwamba kuwa jukumu la mchezaji huyo kuendelea kukipiga Jangwani lipo mikononi mwa mashabiki na wanachama wao.Akizungumzia umuhimu wa mashabiki na wanachama wa Yanga hii leo Jumatano jijini Dar es Salaam, Kamwe […]

The post Kumbe kweli Aziz Ki hajasaini Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hatimaye meneja habari na mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema bado hawajafanikiwa kumuongezea mkataba kiungo wao mshambuliaji, Stephane Aziz Ki.
Kamwe pia alisema kwamba kuwa jukumu la mchezaji huyo kuendelea kukipiga Jangwani lipo mikononi mwa mashabiki na wanachama wao.
Akizungumzia umuhimu wa mashabiki na wanachama wa Yanga hii leo Jumatano jijini Dar es Salaam, Kamwe alisema mashabiki na wanachama Yanga wana wajibu wa kulipa ada ya usajili wa uanachama ili kumudu baadhi ya mambo ya klabu ikiwemo kuendelea kuwa na wachezaji mahiri kama Aziz Ki.
“Mashabiki wengi wananipigia simu kuhusu Aziz Ki. Sasa niwaambie kama wewe ni shabiki wa Yanga na hulipi kadi ya uanachama basi ujue wataondoka wachezaji wengi tu.
“Ili Aziz Ki abaki lazima klabu iwe na hela na hela zinatoka kwetu sisi. Tumewapa fursa ya kulipa ada kupitia mataw ya NBC. Je wachezaji wanabaki vipi ikiwa wewe hulipi ada?
“Hili nimesema nilizungumze hapahapa na niliweke wazi kabisa, mambo mnayoyasikia yakizungumzwa ndiyo maana hata sisi hatutaki kuyaongelea, kwa sababu tunajua hamna timu hapa Tanzania Aziz Ki anaweza kwenda kucheza zaidi ya Yanga, ila tunajua watu wanaomtaka Aziz wako vizuri kweli kipesa.

“Hiyo ni kweli sina hata haja ya kuanza kufanya propaganda, ningekuwa mtu wa propaganda ningewaambia kwamba tayari Aziz yupo lakini hayupo, bado na ni jukumu langu mimi na wewe mwanachama wa Yanga kuhakikisha tunajisajili na Aziz anabakia, huo ndiyo uhalisia wenyewe hakuna siasa hapa, tusipeane moyo wakati uhalisia tunaukimbia,” alisema Kamwe.


Hivi karibuni kumeibuka tetesi lukuki juu ya nyota huyo raia wa Burkinafaso kuwaniwa na vigogo wa Afrika wakiwemo Kaizer Chiefs, Orlando Pirates na Mamelodi Sundowns za Afrika Kusini pamoja na Al Ahly na Pyramids za Misri.
Aziz ambaye amejiunga na Yanga msimu wa 2022-23 akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast ameonesha kiwango kikubwa mpaka sasa akiwa amefunga mabao 15 msimu huu kabla ya mechi yao ya leo dhidi ya Dodoma Jiji akiwa amezidiwa bao moja na kinara Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam aliyefunga mara 16 mpaka sasa.

The post Kumbe kweli Aziz Ki hajasaini Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/aziz-ki-hajasaini-yanga/feed/ 0
Chirwa: Fei ni zaidi ya Aziz Ki https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/chirwa-fei-ni-zaidi-ya-aziz-ki/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/chirwa-fei-ni-zaidi-ya-aziz-ki/#respond Fri, 10 May 2024 07:59:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10912 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Kagera Sugar, Obrey Chirwa amesema anaamini kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni mchezaji mzuri zaidi ya Stephanie Aziz Ki wa Yanga, isipokuwa Fei anashushwa chini kutokana na uhalisia wa nchi yake, Tanzania.Chirwa ambaye anatokea nchini Zambia amezungumza hayo na kufafanua kwamba amekuwa akiiona hali ya wachezaji wa Kitanzania […]

The post Chirwa: Fei ni zaidi ya Aziz Ki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Obrey Chirwa amesema anaamini kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni mchezaji mzuri zaidi ya Stephanie Aziz Ki wa Yanga, isipokuwa Fei anashushwa chini kutokana na uhalisia wa nchi yake, Tanzania.
Chirwa ambaye anatokea nchini Zambia amezungumza hayo na kufafanua kwamba amekuwa akiiona hali ya wachezaji wa Kitanzania kutokukubalika nchini na badala yake wadau huvutiwa zaidi na wanaotoka nje.
Alisema hali hiyo huwakuta wachezaji hao hata kama wana viwango vya kawaida lakini yeye binafsi anaamini ni nchi yenye wachezaji wenye viwango vikubwa mno tofauti na watu wanavyodhani.
“Ukiachana na Diarra (Djigui wa Yanga), nilishakutana na makipa wengi wakali wa Tanzania kama Aishi Manula au Beno Kakolanya, wale wana hatari ujue ila shida ni kwamba Watanzania mnawadharau wenzenu, mnapenda vipya lakini Watanzania wana uwezo mkubwa kushinda ‘maforena’,” alisema Chirwa ambaye timu yake ilifungwa bao 1-0 na Yanga.


“Mnaona mabeki wa kati wa Yanga, wale ni Watanzania lakini watu wanawadharau wanawaona wa kawaida tu. Mfano viungo yaani ina wale kina Mudathir (Yahya), Feisal ni hatari wale siwezi kusema sana lakini mambo yanaelweka.

“Hata Fei na Aziz, Fei yupo juu lakini sababu ni Mtanzania watu wanamchukulia poa mbele ya wageni,” alisema Chirwa ambaye pia aliwahi kukipiga Yanga.


Chirwa aliyewahi pia kukipiga Nogoom FC ya nchini Misri ameongelea ushindani wa Fei na Aziz Ki kwa kuwa pia wanachuana msimu huu msimu huu.


Wachezaji hao ambao walikuwa na ushirikiano mzuri wakati wakiwa Yanga kabla ya Fei kutimkia Azam kwa sasa wamefungana kileleni kwa mabao 15 huku Aziz akiwa juu kwa kutoa pasi za mabao nane na Fei akitoa pasi saba mpaka sasa (kabla ya mechi ya Simba na Azam).

The post Chirwa: Fei ni zaidi ya Aziz Ki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/chirwa-fei-ni-zaidi-ya-aziz-ki/feed/ 0
Aziz Ki, Bruno wang’ara mwezi Machi https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/aziz-ki-bruno-wangara-mwezi-machi/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/aziz-ki-bruno-wangara-mwezi-machi/#respond Tue, 02 Apr 2024 14:12:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10479 Na mwandishi wetuNyota wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi akiwabwaga Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam na Clatous Chama wa Simba SC.Aziz Ki raia wa Burkina Faso ametangazwa leo Jumanne na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuisaidia timu yake kupata ushindi katika […]

The post Aziz Ki, Bruno wang’ara mwezi Machi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Nyota wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi akiwabwaga Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam na Clatous Chama wa Simba SC.
Aziz Ki raia wa Burkina Faso ametangazwa leo Jumanne na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuisaidia timu yake kupata ushindi katika mechi tatu kati ya nne ilizocheza katika mwezi huo.
Kwenye mechi hizo Aziz Ki alifunga mabao matatu na asisti nne na Yanga kuzoa pointi tisa ikisalia kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Hii inakuwa mara ya pili msimu huu kwa Aziz Ki kuchukua tuzo ya mchezaji bora ambapo awali aliibeba mwezi Oktoba, mwaka jana.
Upande wa pili, kocha mkuu wa Azam FC, Bruno Ferry ametangazwa kuwa kocha bora wa mwezi Machi akiwashinda Miguel Gamondi wa Yanga na Zuberi Katwila wa Mtibwa Sugar alioingia nao fainali.
Kwenye mwezi huo Bruno aliiongoza Azam kushinda michezo miwili kati ya mitatu iliyocheza na kuendelea kusalia nafasi ya pili kwenye msimamo.
Bruno anatwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu msimu huu. Aliwahi kutwaa pia mwezi Novemba na Desemba, mwaka jana.

The post Aziz Ki, Bruno wang’ara mwezi Machi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/aziz-ki-bruno-wangara-mwezi-machi/feed/ 0