Augustine Okrah - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 02 Jan 2024 15:28:21 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Augustine Okrah - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Gamondi amtaka Okrah adhihirishe ubora https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/gamondi-amtaka-okrah-adhihirishe-ubora/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/gamondi-amtaka-okrah-adhihirishe-ubora/#respond Tue, 02 Jan 2024 15:28:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9112 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amemtaka mchezaji mpya wa timu hiyo Augustine Okrah kuonesha kwa vitendo imani ambayo viongozi na mashabiki wa timu hiyo wanayo juu yake.Okrah aliyeitumikia Simba msimu uliopita amejiunga na Yanga hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili akitokea timu ya Bencham United ya kwao Ghana.Gamondi raia wa Argentina […]

The post Gamondi amtaka Okrah adhihirishe ubora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amemtaka mchezaji mpya wa timu hiyo Augustine Okrah kuonesha kwa vitendo imani ambayo viongozi na mashabiki wa timu hiyo wanayo juu yake.
Okrah aliyeitumikia Simba msimu uliopita amejiunga na Yanga hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili akitokea timu ya Bencham United ya kwao Ghana.
Gamondi raia wa Argentina alisema timu yake ilihitaji kiungo mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa kulingana na ugumu wa mashindano wanayoshiriki na ukubwa wa Yanga hivyo Okrah anapaswa kujituma na kuonesha kwa vitendo kwamba anastahili kucheza timu hiyo.

“Sihitaji kuzungumza mambo mengi kuhusu yeye, kama kocha nitampa nafasi aonyeshe kwa vitendo ubora wake utakaompa nafasi ya kucheza zaidi endapo atashindwa kufanya kile tunachokitarajia kutoka kwake atawapisha wengine wacheze,” alisema Gamondi.


Kocha huyo alisema kwa ukubwa na malengo ya Yanga, hivi sasa hawahitaji kumpa muda mchezaji kulingana na aina ya mashindano lakini pia uhitaji wa matokeo kuwa mkubwa katika kila mechi.
Alisema kwenye kikosi chake ana wachezaji wenye uwezo na rekodi nzuri huko walikotoka lakini wameshindwa kuingia mapema kwenye mfumo wa Yanga na yeye ameshindwa kuwatumia sababu ya uhitaji wa matokeo.
Malengo ya Yanga msimu huu ni kufika robo fainali kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutetea mataji yote ya ndani ambayo ni Ligi Kuu NBC na Kombe la ASFC (FA).

The post Gamondi amtaka Okrah adhihirishe ubora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/gamondi-amtaka-okrah-adhihirishe-ubora/feed/ 0
Hadithi ya Okrah Yanga yapamba moto https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/hadithi-ya-okrah-yanga-yapamba-moto/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/hadithi-ya-okrah-yanga-yapamba-moto/#respond Fri, 29 Dec 2023 18:39:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9070 Na mwandishi wetuMabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC, Yanga wameendelea kuimarisha kikosi chao kwenye dirisha hili la usajili baada ya kudaiwa kuinasa saini ya winga wa Ghana, Augustine Okrah kwa mkataba wa miaka miwili.Mchezaji huyo ambaye makabrasha yake yanaonesha ana umri wa miaka 30, amejiunga na Yanga akiwa kinara kwenye kiwango bora katika chati ya […]

The post Hadithi ya Okrah Yanga yapamba moto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC, Yanga wameendelea kuimarisha kikosi chao kwenye dirisha hili la usajili baada ya kudaiwa kuinasa saini ya winga wa Ghana, Augustine Okrah kwa mkataba wa miaka miwili.
Mchezaji huyo ambaye makabrasha yake yanaonesha ana umri wa miaka 30, amejiunga na Yanga akiwa kinara kwenye kiwango bora katika chati ya wafungaji wa Ligi Kuu Ghana akiwa amefunga mabao manane.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka nchini Ghana, inadaiwa nyota huyo kutoka klabu ya Bechem United amesaini Jangwani kwa dau la Dola za Kimarekani 150,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 375.
Inaelezwa kuwa Okrah aliyewahi kukipiga Simba alitua nchini tangu jana Alhamisi kukamilisha taratibu za kuichezea timu hiyo inayovaa jezi ya kijani na njano na tangu wakati huo amekuwa akijadiliwa kama kweli amejiunga na Yanga au la.
Huu unakuwa usajili wa pili kwa Yanga kwenye kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili baada ya kuinasa saini ya kiungo Shekhan Ibrahim Khamis kutoka JKU ya Zanzibar kwa mkataba wa miaka mitatu.
Akizungumza leo Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema kifaa kipya ni ‘mgeni’ mwenyeji aliyetakiwa kutambulishwa leo Ijumaa lakini Rais wa klabu hiyo, Hersi Said ameagiza wakamtambulishe visiwani Zanzibar.
“Huyu mchezaji ni mgeni lakini mwenyeji tunatarajia kumtambulisha katika mchezo wetu wa kwanza, utambulisho wake utafunika ile shoo ya msanii Diamond (Platnumz) aliyoifanya pale Uwanja wa Amaan Complex.
“Usajili ambao unafanywa ni kulingana na mapendekezo ya kocha Gamondi (Miguel) kuhakikisha tunaimarisha kikosi chetu na kuwa imara zaidi,” alisema Kamwe.
Aliongeza kuwa timu inaondoka leo kuelekea Zanzibar huku wakiwa na dhamira ya kutwaa Kombe la Mapinduzi na kwenda na kikosi cha wachezaji wote isipokuwa wale walioko katika timu za taifa.
Nyota wengine wanaotajwa kusajiliwa na Yanga ni Simon Msuva na mshambuliaji kutoka klabu ya Dynamo Dougla ya Cameroon, Leonel Ateba.

The post Hadithi ya Okrah Yanga yapamba moto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/hadithi-ya-okrah-yanga-yapamba-moto/feed/ 0
Okrah aanza mazoezi Simba https://www.greensports.co.tz/2023/04/05/okrah-aanza-mazoezi-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/05/okrah-aanza-mazoezi-simba/#respond Wed, 05 Apr 2023 18:44:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5698 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Simba, Augustine Okrah amerejea kwenye maozezi ya kikosi hicho baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takriban miezi miwili akisumbuliwa na jeraha la kidole.Mchezaji huyo raia wa Ghana amerejea kwenye mazoezi ya kwanza ya timu hiyo tangu irejee nchini ikitoka Morocco ilikokwenda kucheza mechi yao ya mwisho ya hatua ya […]

The post Okrah aanza mazoezi Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Augustine Okrah amerejea kwenye maozezi ya kikosi hicho baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takriban miezi miwili akisumbuliwa na jeraha la kidole.
Mchezaji huyo raia wa Ghana amerejea kwenye mazoezi ya kwanza ya timu hiyo tangu irejee nchini ikitoka Morocco ilikokwenda kucheza mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca na kupewa mapumziko ya siku mbili.
Okrah ambaye alipata jeraha hilo kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan mnamo Februari 5, mwaka huu, imemlazimu kukosa mechi za hatua ya makundi za Ligi ya Mabingwa.
Okrah hata hivyo anaweza kuukosa mchezo wa Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Ihefu lakini inawezekana akawemo kwenye mechi ya Kariakoo Derby inayotarajia kupigwa Aprili 16, mwaka huu.

The post Okrah aanza mazoezi Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/05/okrah-aanza-mazoezi-simba/feed/ 0