Antony - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 12 Jan 2024 19:22:02 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.7.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Antony - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 ‘Ya nje ya uwanja yanamtesa Antony’ https://www.greensports.co.tz/2024/01/12/ya-nje-ya-uwanja-yanamtesa-antony/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/12/ya-nje-ya-uwanja-yanamtesa-antony/#respond Fri, 12 Jan 2024 19:22:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9284 Manchester, EnglandWinga wa Man United, Antony amekuwa na wakati mgumu kurudi kwenye ubora wake jambo ambalo kocha wake, Erik ten Hag anasema limesababishwa na matatizo ya nje ya uwanja yanayomuandama mchezaji huyo.Septemba mwaka jana, Antony alilazimika kuwa nje ya klabu hiyo kwa kipindi cha wiki tatu baada ya kujikuta katika tuhuma za kumdhalilisha mwanamke.Polisi nchini […]

The post ‘Ya nje ya uwanja yanamtesa Antony’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Winga wa Man United, Antony amekuwa na wakati mgumu kurudi kwenye ubora wake jambo ambalo kocha wake, Erik ten Hag anasema limesababishwa na matatizo ya nje ya uwanja yanayomuandama mchezaji huyo.
Septemba mwaka jana, Antony alilazimika kuwa nje ya klabu hiyo kwa kipindi cha wiki tatu baada ya kujikuta katika tuhuma za kumdhalilisha mwanamke.
Polisi nchini Brazil pamoja na Uingereza wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo na Ten Hag anasema mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil kwa msimu huu hajafunga hata bao moja au kutoa asisti jambo ambalo anaamini linachangiwa na matatizo yake ya nje ya uwanja.
“Naweza kulielezea hilo na nafikiri ni jambo rahisi, mambo yake ya nje ya uwanja yanamzuia kucheza,” alisema Ten Hag mbele ya waandishi wa habari leo Ijumaa.
“Mwaka wake wa kwanza ulikuwa sawa, kwenye maandalizi ya msimu alikuwa sawa, mechi nne za kwanza alikuwa vizuri lakini tangu awe nje ya timu na hadi anarudi hakuwa na kiwango ambacho ungekitarajia kutoka kwake na ana uwezo wa kufanya vizuri zaidi,” alisema Ten Hag.

“Haya mambo yamemuathiri na hakika yamekuwa na matokeo mabaya kwake, ni lazima akabiliane nayo, ayamalize lakini pia ana wajibu wa kucheza vizuri,” alisema Ten Hag.


Katika hatua nyingine Ten Hag amemtakia heri winga wake wa zamani Jadon Sancho baada ya kuhamia kwa mkopo Borussia Dortmund ingawa hakutaka kusema kama mchezaji huyo ana nafasi katika klabu hiyo kwa siku zijazo.

The post ‘Ya nje ya uwanja yanamtesa Antony’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/12/ya-nje-ya-uwanja-yanamtesa-antony/feed/ 0
Antony apigiwa hesabu kuivaa Galatasaray https://www.greensports.co.tz/2023/10/03/antony-apigiwa-hesabu-kuivaa-galatasaray/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/03/antony-apigiwa-hesabu-kuivaa-galatasaray/#respond Tue, 03 Oct 2023 13:13:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7930 Manchester, EnglandWinga wa Man United, Antony anayetuhumiwa kwa kosa la kumdhalilisha mpenzi wake, huenda leo akaichezea timu yake katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray ya Uturuki.Antony alionekana kwa mara ya mwisho akiiwakilisha Man United, Septemba 3 katika mechi dhidi ya Arsenal na baada ya hapo alilazimika kujiweka kando baada ya aliyekuwa […]

The post Antony apigiwa hesabu kuivaa Galatasaray first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Winga wa Man United, Antony anayetuhumiwa kwa kosa la kumdhalilisha mpenzi wake, huenda leo akaichezea timu yake katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray ya Uturuki.
Antony alionekana kwa mara ya mwisho akiiwakilisha Man United, Septemba 3 katika mechi dhidi ya Arsenal na baada ya hapo alilazimika kujiweka kando baada ya aliyekuwa rafiki yake wa kike Gabriela Cavallin kuibuka na tuhuma hizo.
Katika kipindi hicho hicho, Antony pia aliachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kilichokuwa kikijiandaa kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Antony hata hivyo alirejea mazoezini kwenye kikosi cha Man United kwa mara ya kwanza Jumapili, hiyo ni baada ya kuripoti polisi na kuhojiwa kabla ya kuachiwa bila kufunguliwa kesi katika tuhuma zinazomkabili.
Kocha wa Man United, Erik ten Hag alisema kwamba mchezaji huyo alishiriki kikamilifu kwenye mazoezi ya timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu ajikute katika tuhuma za udhalilishaji.

“Ametoa ushirikiano kikamilifu, Antony anaweza akacheza lakini Jumapili ilikuwa siku yake ya kwanza kwenye mazoezi ya timu, kuna mazoezi ya mwisho Jumatatu na baada ya hapo tutaamua, yupo katika hesabu zetu,” alisema Ten Hag.


Wasichana wanaodai kudhalilishwa na Antony mbali na Gabriela wengine ni Rayssa de Freitas na Lana ambao wote waliwasilisha tuhuma hizo kwenye chombo kimoja cha habari nchini Brazil ingawa mchezaji huyo amekana tuhuma zote hizo.
Antony anasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Man United leo Jumanne ili acheze mechi yake ya kwanza tangu kuibuka kwa tuhuma hizo.
Mechi za leo Jumanne Ligi ya Mabingwa Ulaya
Kundi A
FC Copenhagen v Bayern Munich
Man United v Galatasaray
Kundi B
Lens v Arsenal
PSV Eindhoven v Sevilla
Kundi C
Union Berlin v Sporting Braga
Napoli v Real Madrid
Kundi D
FC Red Bull v Real Sociedad
Inter Milan v Benfica

Mechi za kesho Jumatano Ligi ya Mabingwa Ulaya
Kundi E
Atlético Madrid v Feyenoord
Celtic v Lazio
Kundi F
Borussia Dortmund v AC Milan
Newcastle v PSG
Kundi G
Red Star Belgrade v Young Boys
RB Leipzig v Man City
Kundi H
Royal Antwerp v Shakhtar Donetsk
FC Porto v Barcelona

The post Antony apigiwa hesabu kuivaa Galatasaray first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/03/antony-apigiwa-hesabu-kuivaa-galatasaray/feed/ 0
Antony kurejea mazoezini Man United https://www.greensports.co.tz/2023/09/29/antony-kuanza-mazoezini-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/29/antony-kuanza-mazoezini-man-united/#respond Fri, 29 Sep 2023 12:40:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7885 Manchester, EnglandKlabu ya Manchester United imethibitisha kuwa winga wake, Antony anatarajia kurudi mazoezini ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu ahusishwe na tuhuma za udhalilishaji kijinsia.Antony, 23, ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil, jana Alhamisi aliripoti kituo cha polisi jijini Manchester na baada ya kuhojiwa hakuwekewa vikwazo vyovyote na hajakamatwa au kushitakiwa […]

The post Antony kurejea mazoezini Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Manchester United imethibitisha kuwa winga wake, Antony anatarajia kurudi mazoezini ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu ahusishwe na tuhuma za udhalilishaji kijinsia.
Antony, 23, ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil, jana Alhamisi aliripoti kituo cha polisi jijini Manchester na baada ya kuhojiwa hakuwekewa vikwazo vyovyote na hajakamatwa au kushitakiwa Uingereza au Brazil.
Taarifa ya Man United iliyopatikana leo Ijumaa ilieleza, “Antony ni mwajiriwa wa Manchester United na imeamriwa ataendelea na mazoezi na anaweza kucheza mechi wakati uchunguzi wa polisi ukiendelea. Hili litakuwa likifanyiwa mapitio wakati taratibu nyingine zikiendelea.”
Hata hivyo haitarajiwi mchezaji huyo kuanza mazoezi leo Ijumaa au kupata nafasi ya kucheza mechi ya kesho Jumamosi ya Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace itakayopigwa Old Trafford.
Hadi sasa Antony ameshakosa mechi nne za Man United tangu apewe likizo inayoandamana na malipo kutokana na tuhuma zilizotolewa dhidi yake na wanawake watatu akiwamo rafiki na mpenzi wake wa zamani, Gabriela Cavallin.
Septemba 4 mwaka huu chanzo kimoja cha habari nchini Brazil kiliripoti tuhuma zilizotolewa na Gabriella akilalamika kupigwa kichwa na Antony katika hoteli moja mjini Manchester, tukio analodaiwa kulifanya Januari 15 mwaka huu.
Mwanadada huyo pia alidai kwamba Antony alimpiga ngumi kifuani na kumsababishia maumivu makubwa.
Tuhuma nyingine dhidi ya Antony ziliwasilishwa na wasichana wengine wawili, Rayssa de Freitas na Ingrid Lana kila mmoja akidai kwamba mwaka 2022 alipigwa na Antony ingawa mchezaji huyo ambaye pia aliondolewa katika kikosi cha Brazil, amekana tuhuma zote hizo.

The post Antony kurejea mazoezini Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/29/antony-kuanza-mazoezini-man-united/feed/ 0
Antony ajisalimisha polisi Manchester https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/antony-ajisalimisha-polisi-manchester/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/antony-ajisalimisha-polisi-manchester/#respond Wed, 27 Sep 2023 19:34:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7873 Manchester, EnglandWinga wa Man United, Antony amerudi England akitokea Brazil na amekubali kukutana na polisi wa Manchester ili kujibu maswali kuhusu tuhuma za udhalilishaji zilizowasilishwa dhidi yake.Inadaiwa kwamba winga huyo mwenye umri wa miaka 23 sasa, amekubali kuwakabidhi polisi wa Manchester simu yake ili kuwasaidia katika uchunguzi wanaoufanya dhidi yake.Mwanadada, Gabriela Cavallin ambaye ni rafiki […]

The post Antony ajisalimisha polisi Manchester first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Winga wa Man United, Antony amerudi England akitokea Brazil na amekubali kukutana na polisi wa Manchester ili kujibu maswali kuhusu tuhuma za udhalilishaji zilizowasilishwa dhidi yake.
Inadaiwa kwamba winga huyo mwenye umri wa miaka 23 sasa, amekubali kuwakabidhi polisi wa Manchester simu yake ili kuwasaidia katika uchunguzi wanaoufanya dhidi yake.
Mwanadada, Gabriela Cavallin ambaye ni rafiki wa zamani wa kike wa Antony alinukuliwa na chanzo kimoja cha habari akiwasilisha tuhuma za kufanyiwa udhalilishaji na mchezaji huyo.
Tuhuma nyingine za udhalilishaji dhidi ya Antony ziliwasilishwa na wasichana wengine wawili, Rayssa de Freitas na Lana ingawa mchezaji huyo amekana tuhuma zote hizo.
Wakati yote hayo yakiendelea, klabu ya Man United, imetangaza kuzipa uzito unaostahili tuhuma hizo na wamempa Antony likizo ili kukabiliana na tuhuma hizo ingawa atakuwa akilipwa mshahara wake kama kawaida.
Antony alikuwa akiwajibika kwenye timu yake ya taifa ya Brazil wakati tuhuma hizo zilipotolewa na kujikuta akiondolewa katika kikosi cha timu hiyo mara tu baada ya kuibuka kwa tuhuma hizo kwa mara ya kwanza Septemba 4 mwaka huu.
Mmoja wa wasichana hao, Cavallin katika madai yake alidai kwamba Antony aliwahi kumpiga kichwa wakiwa katika chumba cha hoteli moja mjini Manchester na kumchana kichwani hadi kupatiwa matibabu na daktari.
Msichana huyo pia alidai kuumizwa kifuani baada ya kupigwa ngumi na Antony wakati Lana ambaye ni mtumishi wa benki alidai kusukumwa na mchezaji huyo hadi kujigonga ukutani, tuhuma ambazo pia Antony amezikana.

The post Antony ajisalimisha polisi Manchester first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/antony-ajisalimisha-polisi-manchester/feed/ 0
Antony atua Man Utd kwa pesa ndefu https://www.greensports.co.tz/2022/08/29/antony-atua-man-utd-kwa-pesa-ndefu/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/29/antony-atua-man-utd-kwa-pesa-ndefu/#respond Mon, 29 Aug 2022 10:42:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2607 Manchester, EnglandManchester United imekubali kulipa Pauni 80.75 milioni ili kumsajili winga wa Ajax, Antony ambaye sasa anakuwa mmoja wa wachezaji waliosajiliwa kwa bei mbaya.Baada ya Paul Pogba ambaye alisajiliwa kwa ada ya Pauni 89 milioni na ndiye anayeshikilia rekodi ya mchezaji aliyenunuliwa na Man United kwa bei mbaya, Antony naye sasa anaingia katika orodha hiyo […]

The post Antony atua Man Utd kwa pesa ndefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Manchester United imekubali kulipa Pauni 80.75 milioni ili kumsajili winga wa Ajax, Antony ambaye sasa anakuwa mmoja wa wachezaji waliosajiliwa kwa bei mbaya.
Baada ya Paul Pogba ambaye alisajiliwa kwa ada ya Pauni 89 milioni na ndiye anayeshikilia rekodi ya mchezaji aliyenunuliwa na Man United kwa bei mbaya, Antony naye sasa anaingia katika orodha hiyo ya wachezaji wa bei mbaya.
Antony anabebwa na mafanikio ambayo ameyapata akiwa Ajax kwa kufunga mabao 25 na asisti 82 tangu ajiunge na timu hiyo mwaka 2020 akitokea Sao Pulo ya Brazil lakini kubwa zaidi ni kwamba kocha wa sasa wa Man Utd, Erik ten Hag anamjua vizuri mchezaji huyo uwezo wake kwani amewahi kuwa naye wakati huo akiwa kocha Ajax.
Akiwa ndio kwanza ana miaka 22, Antony alianza kuichezea timu ya Taifa ya Brazil, Oktoba 2021 na tayari ana mabao mawili katika mechi tisa alizoichezea timu hiyo wakati akiwa na Ajax hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao saba katika mechi 11 za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Haijaweza kueleweka mara moja iwapo Antony anayetumia vizuri zaidi mguu wa kushoto kama atavaa jezi ya Man Utd, Alhamisi hii siku ambayo timu hiyo itaumana na Leicester City katika mechi ya Ligi Kuu England kwa kuwa suala hilo pia linahusisha upatikanaji wa kibali cha kufanyia kazi Uingereza.
Anatony anakuwa mchezaji wa tano wa Man Utd kusajiliwa katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi baada ya mchezaji mwenzake wa Ajax, beki Lisandro Martinez, kiungo Casemiro kutoka Real Madrid, beki Tyrell Malacia kutoka Feyernoord na kiungo mchezeshaji Christian Eriksen.
Usajili wa Antony pia unazidisha uvumi kuhusu majaliwa ya Cristiano Ronaldo katika klabu hiyo hasa baada ya kuwapo habari za muda mrefu kwamba mchezaji huyo alikuwa akitaka kuihama timu hiyo.

The post Antony atua Man Utd kwa pesa ndefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/29/antony-atua-man-utd-kwa-pesa-ndefu/feed/ 0