Ahoua – Greensports Site: Habari za michezo na burudani Tanzania na Ulimwenguni. https://www.greensports.co.tz Michezo na burudani ni zaidi ya ajira Mon, 02 Sep 2024 20:47:06 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.7.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ahoua – Greensports Site: Habari za michezo na burudani Tanzania na Ulimwenguni. https://www.greensports.co.tz 32 32 Fadlu, Ahoua wang’ara Agosti https://www.greensports.co.tz/2024/09/02/fadlu-ahoua-wangara-agosti/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/02/fadlu-ahoua-wangara-agosti/#respond Mon, 02 Sep 2024 20:47:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11852

Na mwandishi wetu
Kocha wa Simba, Davids Fadlu na kiungo wa timu hiyo, Jean Ahoua wameibuka vinara wa tuzo za soka za Ligi Kuu NBC kwa mwezi wa Agosti kwa kutwaa tuzo ya kocha na mchezaji bora.
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania iliyopatikana leo Jumatatu, Fadlu na Ahoua wamebeba tuzo hizo kutokana na mafanikio ya Simba katika mechi mbili za ligi hiyo zilizochezwa mwezi Agosti.
Katika mechi hizo Ahoua aliifungia Simba bao moja na kuhusika katika mengine matatu wakati Simba ikiichapa Tabora United mabao 3-0 na kuichapa Fountain Gate mabao 4-0.
Naye Fadlu ametwaa tuzo ya kocha bora akiwashinda Patrick Aussems wa Singida Black Stars na Abdallah Hussein wa Mashujaa ambao aliingia nao katika fainali ya kinyang’anyiro hicho.
Kocha Fadlu ambaye huu ni msimu wake wa kwanza na Simba, aliiongoza timu yake kutopoteza mchezo hata mmoja na kukusanya pointi sita na mabao saba ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Naye Ashraf Omar ambaye ni meneja wa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo ameshinda tuzo ya meneja bora wa mwezi kwa kufanya vizuri katika usimamizi wa matukio na miundombinu ya uwanja huo.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/02/fadlu-ahoua-wangara-agosti/feed/ 0
Simba yajivunia usajili wa kitaalam https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/simba-furahieni-usajili-wa-kitaalam/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/simba-furahieni-usajili-wa-kitaalam/#respond Sun, 07 Jul 2024 19:50:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11551

Na mwandishi wetu
Simba imewaeleza wazi mashabiki wake kuwa wanapaswa kufurahi kutokana na usajili unaoendelea kufanyika katika kikosi hicho kwani ni usajili wa kitaalam mno.
Mpaka leo Jumapili Simba imetambulisha jumla ya wachezaji tisa wapya kwa ajili ya msimu mpya wa 2023-24.
Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amefafanua kuwa timu hiyo iliendelea na usajili mkubwa hata kabla ya kuwa na kocha mkuu kutokana na matunda ya timu kubwa ya skauti na wachambuzi wa kikosi chao.
Kutokana na hilo Kajula amewataka wapenzi wa Simba kutokuwa na wasiwasi kwani maskauti hao ndio waliomshusha mchezaji bra wa Ligi Kuu Ivory Coast, Ahoua Charles kwa ajili ya manufaa ya Simba msimu ujao.
“Niwaeleze tu kwamba timu kubwa iliyopo ya wachambuzi wa kikosi, mchezaji, mahitaji ya timu ndio imekuja na ripoti ya kueleza timu inataka nini kulingana na msimu uliopita.
“Kisha sasa maskauti wanaingia mbali zaidi kutazama mahitaji ya timu na wachezaji wanaohitajika huku pia ukitazama mikataba ya wanaomaliza na unafanyaje ili kuendana na ripoti ya kujenga timu,” alifafanua Kajula.
Alisema kwa jinsi Simba inavyosukwa na timu nyingine zinavyotengeneza timu zao ni dhahiri inaonesha ubora mkubwa wa Ligi Kuu Bara, akiwataka si tu Wanasimba kujivunia hilo bali Tanzania kwa ujumla.
Ukiachana na Clatous Chama aliyetimkia Yanga, Simba imewapa mkono wa kwaheri aliyekuwa nahodha wao, John Bocco, Kennedy Juma, Saido Ntibazonkiza, Henock Inonga, Shaban Chilunda na Luis Miquissone.
Wachezaji wapya ni Lameck Lawi, Joshua Mutale, Steven Mukwala, Abdulrazack Hamza, Valentino Mashaka, Augustine Okajepha, Debora Mavambo, Omari Omari na Ahoua.


Timu hiyo ipo kwenye mchakato mkubwa wa kusuka kikosi kitakachorejesha makali yao baada ya kulikosa taji la ligi kuu kwa misimu mitatu sasa wakilishuhudia taji hilo likitua Yanga.
Juzi Simba imemtangaza pia mrithi wa Abdelhak Benchika, Fadlu Davis raia wa Afrika Kusini aliyetua na jopo lake la benchi la ufundi, tayari kuipeleka Simba katika nchi ya ahadi.
Msimu ujao timu hiyo itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika ambako itahitaji kuonesha ubabe wake kutokana na kiwango ilichokuwa ikionesha kwenye Ligi ya Mabingwa kwa misimu minne mfululizo, hivyo inajipanga kuhakikisha hilo linatimia.
Agosti 3, mwaka huu Simba itafanya tamasha lake la kila mwaka la Simba Day kuonesha vifaa vyao vipya walivyosajili kwa ajili ya michuano mbalimbali watakayoshiriki msimu ujao.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/simba-furahieni-usajili-wa-kitaalam/feed/ 0