Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya ngumi za ridhaa inatarajia kuondoka nchini Machi 9, mwaka huu kuelekea Ghana kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Afrika.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Makore Mashaga ameiambia GreenSports kuwa maandalizi yao kuelekea mashindano hayo yanakwenda vizuri na matarajio ya kurudi na medali ni makubwa.
“Timu ya ngumi itaondoka Machi 9, tutakuwa na mabondia 11, ambapo kati yao wa kiume ni wanane na watatu wanawake, maandalizi yetu yanakwenda vizuri na matarajio ya kufanya vizuri ni makubwa kwa kweli,” alisema Mashaga.
Alisema mabondia wao wote wa kike na kiume wamepania kufanya vizuri ili kujitangaza na kuipigania nchi yao ili kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.
Mashaga pia ameendelea kuipongeza serikali kwa sapoti iliyoitoa kwa timu hiyo ikiwepo kugharamia kambi, chakula, posho za wachezaji na safari ya kuelekea Ghana kwenye mashindano hayo, akiamini mkono wao una faida kubwa.
Ngumi Ngumi za ridhaa waelekea Ghana
Ngumi za ridhaa waelekea Ghana
Read also