London, England
Mpango wa bilionea wa Uingereza, Sir Jim Ratcliffe kununua asilimia 25 ya hisa za klabu za Manchester United umepitishwa rasmi na mamlaka ya Ligi Kuu England (EPL).
Bilionea huyo amenunua hisa hizo kwa thamani ya Dola 1.3 bilioni na kwa sasa kinachosubiriwa ni baraka za Chama cha Soka England au FA ili aanze rasmi kuwajibika katika klabu hiyo.
Wamiliki kutoka Familia ya Glazer wataendelea kubaki na asilimia kubwa katika klabu hiyo ingawa Ratcliffe kupitia kampuni yake ya Ineos Group watakuwa na nguvu ya usimamizi na uendeshaji soka.
“Kwa sasa Ligi Kuu tunasubiri uthibitisho wa kukamilika kwa muamala,” ilieleza taarifa ya mamlaka ya Ligi Kuu ikithibitisha kwamba, Ractliffe mwenye umri wa miaka 71 amesaini na nyaraka nyingine husika.
Mpango wa Ratcliffe kununua hisa Man United ulikubaliwa mwaka jana mwishoni wakati wa Sikukuu ya Krismasi na miongoni mwa uwekezaji unaotarajiwa kufanya na bilionea huyo ni uboreshaji wa Uwanja wa Old Trafford.
Katika usimamizi wa mambo ya soka, Ineos sasa watakuwa na majukumu kwenye timu ya soka ya wanaume na ile ya wanawake pamoja na akademi zinazomilikiwa na klabu hiyo.
Sambamba na hilo pia Ineos watakuwa na nafasi mbili za ushiriki kwenye vikao vya bodi ya klabu ya Manchester United.
Bilionea Ratcliffe tayari ameshafanya ziara kwenye Uwanja wa Old Trafford pamoja na kufanya vikao na maofisa kadhaa wa Man United akiwamo kocha wa timu hiyo, Erik ten Hag.
Kimataifa EPL wampitisha Bilionea Ratcliffe Man Utd
EPL wampitisha Bilionea Ratcliffe Man Utd
Read also