Nyon, Switzerland
Baada ya kubeba tuzo ya Ballon d’Or, Lionel Messi, kwa mara nyingine atachuana na washambuliaji wenzake, Erling Haaland na Kylian Mbappe katika tuzo za mwaka ya mchezaji bora wa Fifa mwaka 2023.
Wakati Messi akichauana na kina Mbappe na Haaland, kwa upande wa wanawake mchuano utakuwa kati ya Aitana Bonmati, Linda Caicedo na Jennifer Hermoso ambapo mshindi atatangazwa Januari 15 mwakani jijini London.
Kwa upande wa tuzo ya Puskas ambayo inahusisha goli bora la mwaka, mchuano utakuwa kati ya Julio Enciso, Guilherme Madruga na Nuno Santos.
Sarina Wiegman, Emma Hayes na Pep Guardiola wamo kwenye orodha ya tuzo ya kocha bora wakati kwenye tuzo ya kipa wamo Mary Earps na Ederson.
Gumzo kubwa litakuwa kati ya Haaland wa Man City, Mbappe wa PSG na Messi wa Inter Miami ya Marekani ambao wamo kwenye orodha ya wachezaji 12 wanaowania tuzo hiyo.
Orodha ya wachezaji wanaowania tuzo, timu wanazochezea na mataifa yao ni kama ifuatavyo…
Wanaume:
Erling Haaland (Norway-Man City)
Kylian Mbappe (Ufaransa-PSG)
Lionel Messi (Argentina-Inter Miami)
Wanawake:
Aitana Bonmati (Hispania-Barcelona)
Linda Caicedo (Colombia-Real Madrid)
Jenni Hermoso (Hispania-Pachuca)
Kimataifa Messi, Haaland, Mbappe wawania tuzo Fifa
Messi, Haaland, Mbappe wawania tuzo Fifa
Read also