Milan, Italia
Waendesha mashtaka wa tume ya kudhibiti madawa ya yaliyopigwa marufuku michezoni wa nchini Italia wameomba kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba afungiwe miaka minne.
Pogba (pichani) ambaye alikuwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 2018, baada ya kufanyiwa vipimo alibainika kutumia madawa ya kusisimua misuli ambayo hayaruhusiwi kwa wanamichezo.
Baada ya kukutwa na tuhuma hizo, Pogba hakutaka suala hilo limalizwe kwa kufanya mazungumzo ya awali na waendesha mashtaka hao, na hiyo maana yake ni kwamba atapandishwa katika mahakama ya kupambana na madawa ya kuongeza nguvu ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Adhabu ya kufungiwa miaka minne pia inatambuliwa duniani katika kanuni zinazohusu makosa hayo lakini adhabu hiyo inaweza kupunguzwa iwapo mchezaji huyo ataweza kuthibitisha kwamba hakuwa amekusudia kufanya kosa analohusishwa nalo.
Vipimo vilivyobaini kwamba Pogba anatumia madawa hayo vilifanyika Agosti mwaka huu katika mechi kati ya Juventus na Udinese na kutangazwa mwezi mmoja baadaye ingawa katika mechi hiyo Pogba alikuwa benchi.
Pogba alirudi kwa mara nyingine katika klabu ya Juventus mwaka 2022 baada ya kuondoka Man United lakini alipitia kipindi kigumu akiandamwa na balaa la majeruhi.
Kimataifa Wataka Pogba afungiwe miaka minne
Wataka Pogba afungiwe miaka minne
Read also