Na mwandishi wetu
Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), imemteua mchambuzi wa soka, Jemedari Said Kazumari (pichani) kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania zitakazotolewa na Taswa.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumatano na Katibu Mkuu wa Taswa, Alfred Lucas alisema chama hicho kimerejesha tuzo zake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
“Sherehe ya kuzawadia wanamichezo wote waliofanya vizuri mwaka 2023/24 kwa michezo mbalimbali kadri Kamati ya Utendaji ya TASWA itakavyopanga kwa ushauri wa Kamati ya Tuzo,” ilieleza taarifa ya Alfred.
Alisema makamu mwenyekiti wa kamati hiyo ni Mbonile Burton na katibu atakuwa Ramadhan Mbwaduke huku wajumbe wakiwa ni Tullo Chambo, Wilson Oruma, Patrick Nyembera, Evance Mhando, Amry Masare, Aaron Mpanduka, Ramadhani Mwelondo, Cosmas Mlekani, Adam Lutta, Gift Macha, Charles Abel, Paschal Kabombe, Mussa Mwakisu na Anuary Binde.
Wengine ni Tagato James, Ezekiel Ombopo, Alex Luambano, Faustine Felician, Abisay Stephen Jr, Abdul Mkeyenge, Yusuph Badi, Omary Katanga, Irene Kilango, Athanas Kazige, Suleiman Jongo, Rahel Pallangyo, Fatma Chikawe na Abdallah Ibrahim.
Mapunda alifafanua kuwa dhamira ya Taswa ni kuhakikisha michezo yote inayotambuliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), inafuatiliwa na kwa wale watakaostahili kupewa tuzo wanafikiwa.