London, England
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na timu ya Taifa ya England, Harry Kane (pichani) ameamua kuweka wazi kwamba anataka kujiunga na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Awali Kane alikuwa akitajwa kuwindwa na timu nne za PSG, Man United, Real Madrid pamoja na Bayern ambayo mwenyewe ametangaza kuitaka ingawa Man United imeshatangaza kutomtaka tena.
Mpango wa Kane kwenda Bayern hata hivyo unatatizwa na ofa ya klabu hiyo ambayo ni ndogo na huenda ikakataliwa na Spurs ambayo inataka ilipwe kuanzia Dola 100 milioni.
Habari za ndani zinadai kwamba Bayern ipo tayari kutoa Dola 70 milioni kwa ajili ya kumpata mchezaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya England.
Kane ambaye mkataba wake na Spurs unafikia ukomo mwishoni mwa msimu ujao, amewahi kukiri kwamba yuko tayari kuihama timu hiyo na kwenda kusaka changamoto mpya kwingineko barani Ulaya.
Na ingawa Kane ametangaza kuitaka Bayern lakini hali hiyo haiwezi kuzitoa timu za PSG na Real Madrid katika mbio za kumsaka mchezaji huyo.
Kimataifa Kane aitaka Bayern Munich
Kane aitaka Bayern Munich
Read also