Leverkusen, Ujerumani
Kocha Jose Mourinho ana kila sababu ya kuwa na furaha baada ya AS Roma kufuzu fainali ya Europa Ligi ikiwa ni mara ya pili mfululizo kuifikisha timu hiyo hatua ya fainali ya michuano ya klabu Ulaya.
Roma jana Ahamisi ilitoka sare ya bao 0-0 na Bayer Leverkusen ya Ujerumani na hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa bao 1-0, ushindi ambao iliupata katika mechi ya kwanza ikiwa nyumbani.
Msimu uliopita, Maurinho aliifikisha timu hiyo katika fainali ya Europa Conference Ligi na kubeba taji hilo na sasa anajiandaa kuipa timu hiyo taji jingine la pili la Ulaya yaani Europa Ligi.
Roma sasa itaumana na Sevilla katika mechi ya fainali itakayopigwa Mei 31. Sevilla imefuzu hatua hiyo baada ya kuichapa Juventus mabao 2-1 na hivyo kupata kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.
Katika mechi ya nusu fainali ya kwanza, Edoardo Bove aliipatia Roma bao pekee ambalo limetosha kuwa mtaji wa kuifanya timu hiyo iweke rekodi ya kufikia hatua ya fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu barani Ulaya.
Mourinho hapo Mei 31 atakuwa akiwania rekodi ya kushinda mechi ya sita ya fainali katika michuano ya klabu barani Ulaya akiwa tayari amefanikiwa kushinda fainali hizo mara tano, mara mbili akiwa FC Porto na nyingine alishinda akiwa, Man United, Inter Milan na AS Roma.
Kimataifa Mourinho kwa raha zake
Mourinho kwa raha zake
Read also