Na mwandishi wetu
Timu ya wasichana chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu Serengeti Girls imekwama katika kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2025 baada ya kulala kwa bao 1-0 mbele ya Zambia.
Katika mechi hiyo iliyopigwa leo Jumamosi Machi 15, 20225 ambayo Serentgeti ilikuwa ugenini Zambia kwenye Uwanja wa levy Mwanawasa mjini Ndola bao pekee la washindi lilipatikana dakika ya 52 na Natsha Nkaka,
Kwa kipigo hicho ndoto za Serengeti Girls kucheza fainali za Kombe la Dunia zinakuwa zimeyeyuka rasmi timu hiyo ikiwa imefungwa jumla ya mabao 4-0 baada ya kulala kwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza iliyopigwa Jumapili iliyopita mjini Dar es Salaam.
Baada ya kupata ushindi huo timu ya Zambia maarufu Copper Princesses inakuwa imesonga mbele ikisubiri kuumana na mshindi wa mechi kati ya Benin na DR Congo.
Fainali za Kombe la Dunia kwa timu za wasichana chini ya miaka 17 zitafanyika nchini Morocco kuanzia Oktoba 17 mwaka huu.
Kimataifa Serengeti Girls yakwama Zambia
Serengeti Girls yakwama Zambia
Read also