Na mwandishi wetu
Simba imeendelea kuifukuzia Yanga katika Ligi Kuu NBC baada ya kuitandika Namungo FC mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa leo Jumatano, Februari 19, 2025 katika uwanja wa Majaliwa mjini Lindi.
Mabao yaliyoibeba Simba leo yalifungwa na Jean Ahoua ambaye alifunga mabao mawili likiwamo moja la mkwaju wa penalti na ndiye aliyeibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.
Bao la tatu lililohitimisha karamu ya mabao ya Simba kwa leo lilijazwa kimiani na Steven Mukwala.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 50 ikiwa imezidiwa pointi mbili na mahasimu wao Yanga wanaoshika usukani wa ligi.
Yanga ambayo hadi sasa imecheza mechi 20 pia imeizidi Simba kwa mechi moja, mechi ambayo mashabiki wa Simba wanaamini inaweza kuiengua Yanga kileleni.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa leo, Azam FC ikiwa kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid ilishindwa kutamba mbele ya Coastal Union baada ya kulazimishwa sare ya 0-0.
Nao Mashujaa Mashujaa FC wakiwa kwenye dimba la Lake Tanganyika waliitandika Pamba fc mabao 2-0.
Soka Simba yaitandika Namungo 3-0
Simba yaitandika Namungo 3-0
Read also