Liverpool, England
Klabu ya soka ya Everton imetangaza kumfuta kazi kocha Sean Dyche baada ya kuinoa timu hiyo ya Goodison Park kwa muda usiozidi miaka miwili.
Uamuzi huo umefikiwa saa chache kabla ya timu hiyo kujitupa uwanjani kuikabili timu ya Ligi One ya Peterborough katika mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la FA.
Sambamba na Dyche, 53, Everton pia imewafuta kazi wasaidizi wanne wa kocha huyo ambao ni Ian Woan, Steve Stone, Mark Howard na Billy Mercer.
Baada ya kutangaza kumtimua Dyche, klabu hiyo ilitangaza kuwa kocha wa timu yao ya vijana chini ya miaka 18, Leighton Baines na nahodha wa timu hiyo, Seamus Coleman ndio watakaokaimu nafasi ya kocha huyo.
Coleman ambaye ni beki wa kulia na Baines ambaye ni beki wa zamani wa kushoto, ni majina yenye heshima katika klabu hiyo na wenye uzeofu wa muda mrefu.
Uamuzi wa kumtimua Dyche umetokana na mwenendo mbaya wa Everton kwenye Ligi Kuu England ambapo Jumamosi ilichapwa bao 1-0 na Bournemouth na kwa sasa inashika nafasi ya 16 ikiwa imeshinda mechi tatu tu kati ya 19 za ligi hiyo.
Dyche amefutwa kazi kinyume na matarajio yake kwani alinukuliwa hivi karibuni akisema kwamba amefanya mazungumzo yenye mwelekeo chanya na wamiliki wa klabu na wote wameonesha kuwa na matarajio makubwa.
Kimataifa Everton yamtimua kocha Sean Dyche
Everton yamtimua kocha Sean Dyche
Read also