Na mwandishi wetu
Nyota ya kiungo wa Simba, Fabrice Ngoma imeendelea kung’ara baada ya kufunga bao pekee na kuiwezesha timu yake kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Singida Black Stars mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Liti Jumamosi hii.
Bao hilo pekee la Ngoma lilipatikana dakika ya 42 kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Jean Ahoua na kuruka juu kuwazidi walinzi wa Singida kabla ya kuujaza wavuni.
Hii ni mara ya pili kwa Ngoma kufunga bao la kichwa, alifanya hivyo katika mechi nyingine ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Kagera Sugar ambayo Simba ilitoka uwanjani na ushindi wa mabao 5-2.
Dakika moja baada ya kuingia bao hilo, Simba walifanya shambulizi jingine kali ambalo lilitokana na krosi ya Mukwala na Kibu Dennis kuunganisha kwa staili ya tikitaka lakini mpira ulipaa nje ya lango.
Singida nao hawakufanya ajizi wakajibu kwa shambulizi kali baada ya Elvis Rupia kuunganisha kwa kichwa maridadi mpira wa krosi lakini kipa wa Simba, Musa Camara alikuwa makini na kuudaka mpira huo.
Kipindi cha pili timu ziliendelea kushambuliana na kufanya mabadiliko kadhaa lakini hadi mwamuzi Shomari Lawi anapulizi filimbi ya kumaliza mchezo, Simba walitoka na bao lao pekee.
Kwa ushindi huo Simba imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa wamefikisha pointi 40.
Kimataifa Ngoma aizamisha Singida Black
Ngoma aizamisha Singida Black
Read also