Manchester, England
Winga wa Man United, Alejandro Garnacho amejitoa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kinachojiandaa kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuumia goti la mguu wa kushoto.
Argentina katika mbio za kufuzu fainali hizo itakuwa na mechi mbili dhidi ya Venezuela Alhamisi na dhidi ya Bolivia Jumanne ijayo, mechi ambazo, Garnacho mmoja wa wachezaji muhimu wa timu hiyo atazikosa.
Garnacho, 20, Jumapili alicheza kwa dakika 90 mechi ya Man United dhidi ya Aston Villa kwenye Ligi Kuu England, mechi ambayo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana ingawa ilibainika kuwa hali yake haikuwa nzuri.
Tayari Argentina imetambua kuumia kwa mchezaji huyo na nafasi yake amepewa nyota wa Leicester City, Facundo Buonanotte.
Argentina katika mbio za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 inashika usukani katika kundi lake kwa tofauti ya pointi mbili ikifuatiwa na Colombia inayoshika nafasi ya pili.
Garnacho hadi sasa ameichezea timu ya taifa ya Argentina mara saba na alitoa mchango mkubwa kwa timu hiyo kubeba taji la Copa America kwa mara ya 16 katika fainali zilizopigwa nchini Marekani Juni mwaka huu.
Kimataifa Goti lamtoa Garnacho kikosini Argentina
Goti lamtoa Garnacho kikosini Argentina
Read also