Addis Ababa, Ethiopia
Bao pekee la Prince Dube limeiwezesha Yanga kutamba ugenini leo Jumamosi ikitoka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Benki ya Biashara ya Ethiopia (CBE) katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mechi hiyo iliyochezwa mjini Addis Ababa, Ethiopia kwenye Uwanja wa Abebe Bikira, Yanga ilipata bao hilo pekee dakika ya 45 baada ya Dube kuinasa pasi ya Maxi Nzengeli iliyotokea upande wa kushoto wa uwanja.
Ushindi huo wa ugenini unakuwa hatua moja nzuri ya timu hiyo kusonga mbele katika michuano hiyo baada ya kuwa tayari imevuka hatua ya kwanza kwa kuitoa Vital’O ya Burundi.
Yanga sasa inasubiri kurudiana na CBE Jumamosi ijayo katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar ambapo timu hiyo itahitaji sare ya aina yoyote au ushindi wowote ili isonge mbele hatua ya makundi.
Kimataifa Yanga yatamba Ethiopia
Yanga yatamba Ethiopia
Read also