Chicago, Marekani
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti anesema kwamba mshambuliaji wake, Endrick (pichani) mwenye umri wa miaka 18 ana vitu vya kipekee.
Ancelotti ametoa kauli hiyo baada ya mchezaji huyo wa Brazil kucheza mechi yake ya kwanza na kikosi cha Real Madrid dhidi ya AC Milan mapema wiki hii na Real Madrid kufungwa bao 1-0.
Endrick ambaye amejiunga na Real Madrid akitokea Palmeiras ya Brazil baada ya makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2022, alicheza katika kipindi cha kwanza kabla ya kufanyiwa mabadiliko katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Soldier.
“Ni mwepesi na hatari katika maeneo magumu, ana uwezo wa kugeuka kwa kasi katika eneo dogo, anajua namna ya kujiweka sehemu nzuri, zote hizi ni sifa alizonazo na hiyo maana yake ni kwamba ana kipaji cha kipekee, ni nadra kukuta mchezaji mwenye sifa za aina hii,” alisema Ancelotti.
Bao pekee la AC Milan katika mechi hiyo lilifungwa na mshambuliaji wa timu hiyo kutoka Nigeria, Samuel Chukwueze katika dakika ya 56 na hivyo kumpa ushindi wa pili kocha mpya wa timu hiyo, Paulo Fonseca.
Real Madrid ambayo kwa sasa ipo nchini Marekani kwa ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024-25. katika mechi hiyo haikuwa na wakali wake, Vinicius Jr. Jude Bellingham, Rodrygo na mshambuliaji mpya Kylian Mbappe.
Kimataifa Ancelotti: Endrick ana vitu vya kipekee
Ancelotti: Endrick ana vitu vya kipekee
Read also