Madrid, Hispania
Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe amelimwa kadi nyekundu (red card) Jumapili hii, Aprili 13, 2025 katika mechi ya La Liga dhidi ya Alaves ambayo Real Madrid imeshinda kwa bao 1-0.
Ushindi huo umeifanya timu hiyo kuendelea kuwafukuzia mahasimu wao Barcelona wanaoshika usukani wa La Liga kwa tofauti ya pointi nne.
Mbappe ambaye ataikosa mechi ya Jumapili ijayo dhidi ya Athletic Bilbao, awali alipewa kadi ya njano kwa kumkanyaga kwenye ugoko Antonio Blanco lakini baada ya VAR kutumika mwamuzi aliamua kumpa kadi nyekundu moja kwa moja.
Tukio la Mbappe lilitokea dakika ya 38 ikiwa ni dakika nne baada ya Real Madrid kupata bao hilo pekee lililofungwa na Eduardo Camavinga kwa shuti la mguu wa kushoto nje kidogo ya eneo la penalti.
Real Madrid iliyobaki na wachezaji 10 uwanjani ilikuwa na kazi nzito ya kujihami ambapo kipa Thibaut Courtois aliazimika kuokoa michomo sita iliyoelekezwa langoni mwake.
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alianza mchezo huo bila ya wachezaji wake nyota, Vinicius Junior na Jude Bellingham walioanzia kwenye benchi ikiwa ni siku chache baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-0 na Arsenal katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ancelotti ambaye Mei 11 atakuwa na mechi ngumu dhidi ya Barcelona, hata hivyo baadaye aliwapa nafasi wachezaji hao lakini kuwapo kwao hakukuweza kubadili matokeo.
Mbappe aomba radhi
Baada ya mechi hiyo, Mbappe aliwaomba radhi wachezaji wenzake wa Real Madrid pamoja na Blanco huku akionekana kuchukizwa na tukio hilo.
Kwa upande wake Blanco alikiri kuombwa radhi na kukubaliana na tukio hilo ambalo alisema mambo kama hayo hutokea kwenye soka.
“Ni rafu mbaya, nimezungumza na Kylian, ameomba radhi, matukio ya aina hii huto9kea kwenye soka,” alisema Blancxo mbele ya waandishi wa habari.
Kimataifa Mbappe alimwa red card, aomba radhi
Mbappe alimwa red card, aomba radhi
Read also