Lyon, Ufaransa
Kiungo wa zamani wa Man United, Nemanja Matic (pichani) amemtaja kipa wa timu hiyo, Andre Onana kuwa ni mmoja wa makipa wa hovyo katika historia ya klabu hiyo.
Matic, 36, alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Onana ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa ya Cameroon ambaye alisema Man United ni bora kwa mbali kuizidi klabu ya Lyon ya Ufaransa.
Onana alitoa kauli hiyo siku kadhaa kabla ya timu hizo kuumana katika robo fainali ya Europa, mechi ambayo iliisha kwa sare ya 2-2 na sasa timu hizo zitarudiana Alhamisi ijayo.
Akizungumzia kauli hiyo, Matic ambaye aliichezea Man United kati ya mwaka 2017 hadi 2022, alisema anapenda kuheshimu kila mtu lakini inapotokea mtu kutoa kauli kama za Onana unatakiwa kuwa na majibu yake.
Matic aliongeza kwa kusema kwamba inapotokea wewe kuwa mmoja wa makipa wa hovyo katika historia ya Man United ni lazima uwe makini na kile unachokisema.
“Kama angekwua ni Van der Sar, (Peter) Schmeichel au (David) De Gea anayesema hayo ningejiuliza mimi mwenyewe lakini ni lazima uwe na sifa za kutoa kauli kama hizo,” alisema.
Matic ambaye akiwa Man United aliichezea timu hiyo mara 128, mwaka jana alijiunga na Lyon baada ya kuzichezea timu za Rennes pia ya Ufaransa na Roma ya Italia.
Akiwa Man United alibeba taji la Ligi Kuu England mara mbili pamoja na taji la FA na EFL kwa miaka minne aliyokuwa na klabu ya Chelsea.
Kwa upande wa Onana alijiunga na Man United mwaka 2023 akitokea Inter Milan ya Italia na hadi sasa taji pekee alilofanikiwa kulibeba ni lile la FA.
Kipa huyo hivi karibuni amejikuta akilaumiwa kwa kufanya makosa ya kizembe mojawapo ni kitendo chake cha kuchelewa kugawa mipira baada ya kuidaka.
Kimataifa Matic: Onana kipa wa hovyo
Matic: Onana kipa wa hovyo
Read also