Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea na makali yake kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kuinyuka Azam FC mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa leo Alhamisi, Aprili 10, 2025 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Ushindi huo ni hatua muhimu kwa Yanga katika mbio zake za kulitetea taji la ligi hiyo kwa kuwa Azam ni moja ya timu ambazo zilizoaminika kuwa na ubora wa kuizua Yanga lakini imekwama.
Yanga walianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 10 mfungaji akiwa Pacome Zouzoua kabla ya kuongeza la pili dakika ya 34 lililofungwa na Prince Dube ambaye pia aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.
Juhudi za Azam kusawazisha mabao hayo hazikuweza kuzaa matunda badala yake timu hiyo iliishia kupata bao pekee la kufutia machozi lililofungwa na Lusajo Mwaikenda katika dakika ya 82.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 67 katika mechi 25.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizopigwa leo, Coastal Union ikiwa nyumbani Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani iliichapa Singida B kwa mabao 2-1.
Kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Tabora United baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Mashujaa wakati JKT Tanzania ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ilitoka sare ya mabao 2-2 na Namungo FC.
Kimataifa Yanga yaitandika Azam 2-1
Yanga yaitandika Azam 2-1
Read also