Na mwandishi wetu
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Walace Karia ameahidi kuwapa ushirikiano viongozi wapya wa kamati ya utendaji ya Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA).
Hayo yamo katika taarifa ya TFF iliyopatikana leo Jumapili Aprili 6, 2025 na kusainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho hilo, Clliford Ndimbo.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliofanyika leo jijini Mbeya ni Elias Mwanjala aliyeshinda nafasi ya uenyekiti na Emmanuel Jacob aliyeibuka kidedea nafasi ya makamu mwenyekiti.
Wengine waliochaguliwa ni Geoofrey Mkumbwa aliyeshinda nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF, Elisia Mwaipopo na Mohamed Mashango ambao wameshinda nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.
Karia mbali na kuahidi kuipa ushirikiano kamati hiyo mpya, pia aliwataka wajumbe waliochaguliwa kuhakikisha wanasimamia maendeleo ya mpira wa miguu mkoani Mbeya.
Kimataifa Karia awaahidi ushirikiano MREFA
Karia awaahidi ushirikiano MREFA
Read also