London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amethibitisha kwamba nyota wake, Bukayo Saka aliyekuwa majeruhi yuko tayari kwa kazi wakati wakisubiri kuikabili Fulham Jumanne hii, Aprili Mosi 2025.
Saka ambaye alipata majeraha ya misuli na kufanyiwa upasuaji Desemba mwaka jana, amekuwa nje ya kikosi cha Arsenal lakini kwa sasa yuko fiti na anatarajia kuikabili Fulham.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, aliumia misuli ya mguu wa kulia katika kipindi cha kwanza wakati wa mechi na Crystal Palace, mechi ambayo Arsena ilitoka na ushindi wa mabao 5-1.
Kikosi cha Arsenal licha ya kuonesha makali yake msimu huu lakini kimekuwa kikiandamwa na janga la wachezaji majeruhi wakiwamo Kai Havert, Gabriel Martinelli na Gabriel Jesus ambao wamekuwa nje ya kikosi hicho kwa muda sasa.
Mchezaji mwingine ambaye naye ni majeruhi ni Riccardo Calafiori ambaye atakuwa nje kwa wiki kadhaa baada ya kuumia wakati akiiwakilishi timu ya taifa ya Italia.
Arsenal kwa sasa inapambana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na Ligi Kuu England (EPL) ikiwa nafasi ya pili, imeachwa na vinara Liverpool kwa tofauti ya pointi 12.
Kupona kwa Saka kunakuwa faraja kubwa kwa timu hiyo kwenye EPL pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Aprili 8 timu hiyo itaumana na Real Madrid katika mechi ya pili ya hatua ya robo fainali.
Kimataifa Saka yuko fiti kuikabili Fulham
Saka yuko fiti kuikabili Fulham
Read also