Manchester, England
Kocha wa Man United, Ruben Amorim amesema kwamba hatomruhusu kiungo wake nyota, Bruno Fernandes kuihama timu hiyo wakati wa usajili wa dirisha kubwa la Majira ya Kiangazi.
Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na habari kwamba Amorim yuko katika mkakati mzito wa kukisuka kikosi chake akijiandaa kwa msimu ujao ambao anatarajia kuuanza tangu mwanzo.
Wakati Amorim akiwa na mpango huo, Fernandes amekuwa akitajwa katika mipango ya kuhamia Real Madrid lakini kocha wake amemwambia wazi kiungo huyo Mreno kuwa yumo katika mipango ya baadaye Man United.
Amorim alitoa kauli hiyo Jumatatu kwenye mkutano na waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu habari za Fernandes kuhama ambapo alijibu kwa kifupi, “Hapana, hicho kitu hakitatokea.”
Kocha huyo alifafanua kuwa Fernandes hatokwenda popote kwa sababu tayari ameshamwambia kuhusu jambo hilo.
Msimu huu umekuwa wa hovyo kwa Man United ikiwa nafasi ya 13 kwenye Ligi Kuu England (EPL) ngawa Fernandes ameendelea kuonesha ubora wake akiwa ameifungia timu hiyo mabao 16 na kutoa asisti 16 katika mashindano yote.
Fernandes, 30, alijiunga na Man United mwaka 2020 na kwa sasa mkataba wake na klabu hiyo unafikia ukomo mwaka 2027 ingawa kuna kipengele kinachompa nafasi ya kuongeza mwaka mmoja.
Kimataifa Amorim: Fernandes haondoki
Amorim: Fernandes haondoki
Read also