Na mwandishi wetu
Yanga Princess imewatambia mahasimu wake, Simba Queens kwa kuwachapa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Wanawake (TWPL) iliyopigwa leo Jumanne, Machi 18, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam.
Baada ya mpambano mkali, dakika 45 za kwanza zilimalizika bila timu kupata bao kabla ya Yanga kupata bao hilo pekee dakika nne baada ya mapumziko lililofungwa na Jeannine Mukandayisenga.
Jeannine ambaye ni mchezaji kutoka nchini Rwanda alimchambua vyema kipa wa Simba Queens, Winfrida Ouko kutoka Kenya na kuihakikishia timu yake pointi tatu muhimu.
Yanga Princess pamoja na ushindi huo, inaendelea kushika nafasi ya tatu hivyo bado ina kazi ya kufanya ili kuwaengua kileleni Simba Queens ambao ndio mabingwa watetezi.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo yenye timu 10 zilizochezwa leo, matokeo ni kama ifuatavyo: Ceasiaa Queens iliichapa Mlandizi Queens mabao 5-2, Allance Queens ilipata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Gets Program wakati kesho Mashujaa Queens watacheza na JKT Queens.
Soka Yanga Princess yaipiga Simba Queens
Yanga Princess yaipiga Simba Queens
Read also