Rio de Janeiro, Brazil
Neymar da Silva Santos Sr ambaye ni baba na wakala wa Neymar Jr amesema mtoto wake anataka kuwa na mkataba utakaomfanya aendelee kuichezea Santos hata baada ya Majira ya Kiangazi.
Neymar Jr ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil, alijiunga na klabu ya Santos mwezi uliopita akitokea Al Hilal ya Saudi Arabia kwa makubaliano ya pande mbili na kusaini mkataba utakaofikia mwisho Juni mwaka huu.
Janga la kuwa majeruhi limemuandama Neymar na kujikuta akiichezea mechi saba tu Al Hilal tangu kujiunga na timu hiyo Agosti 2023 kwa ada ya Dola 94 milioni akitokea PSG ya Ufaransa.
“Mpango wetu si kwa miezi mitano tu, ni mkataba ambao tunafikiria kuuongeza, hatujaja hapa kushindana kwa miezi mitano, tupo hapa kuipa Santos nafasi ya kujiweka vizuri kutafuta wadau wa kuijenga klabu,” alisema Neymar Sr.
Jumapili iliyopita Neymar aliifungia Santos bao katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Agua Santa na hilo kuwa bao lake la kwanza tangu arudi kwa mara nyingine katika timu hiyo aliyowahi kuichezea utotoni.
Baada ya kufunga bao hilo, Neymar ambaye kwa sasa ana miaka 33 alifurahia kwa kuibusu nembo ya klabu hiyo kwenye jezi.
Furaha ya Neymar haikuishia uwanjani kwani baada ya hapo aligeukia kwenye mtandao wa Instagram ambapo aliandika, “Ushindi muhimu, twende mbele Santos.