Na mwandishi wetu
Mabao ya Clement Mzize na Prince Dube yameiwezesha Yanga kutoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars na kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Katika mechi hiyo iliyopigwa leo Jumatatu, Februari 17, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam, wenyeji Yanga waliandika bao lao la kwanza dakika ya 14 kupitia kwa Mzize.
Dakika mbili kabla ya timu kwenda mapumziko, Dube aliipatia Yanga bao la pili na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko Yanga wakiwa mbele kwa mabao 2-0.
Juhudi za Singida BS kusaka bao zilizaa matunda katika dakika ya pili ya nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika mfungaji akiwa nyota wa timu hiyo kutoka Ghana, Jonathan Sowah.
Kwa ushindi huo Yanga sasa imefikisha pointi 52 katika michezo 20 wakati mahasimu wao Simba wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 47 ingawa Yanga wamecheza mechi 20 wakati Simba wamecheza 18.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa mjini Manyara, wenyeji Fountain Gate walitoka sare ya 0-0 na Tabora United.
Soka Yanga yajiimarisha kileleni
Yanga yajiimarisha kileleni
Read also