Na mwandishi wetu
Yanga, Simba hazichekani, ndicho kilichotokea baada ya Yanga kugawana pointi moja moja na JKT Tanzania katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Jumatatu Februari 10, 2025.
Siku chache zilizopita, Yanga waliwacheka mno Simba wallpogawana pointi moja moja na Fountain Gate katika mechi ya ligi hiyo iliyoisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.
Yanga ingawa wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 46, kushindwa kunyakua pointi zote tatu katika mechi ya leo inaweza kuwa sababu ya kukaa kileleni kwa muda mfupi.
Hiyo ni kwa sababu Simba wanaoshika nafasi ya pili wana pointi 44 na wapo nyuma kwa mechi moja, Yanga wamecheza mechi 18 wakati Simba wamercheza mechi 17 na kesho Juamnne wataikabili Tanzania Prisons.
Matarajio makubwa waliyokuwa nayo Yanga hii leo ni timu yao kutoka na ushindi kwenye dimba la Meja Jenerali Isamhuyo, Mbweni, Dar es Salaam lakini JKT wamewakatalia na kujikuta wakiambulia pointi moja.
JKT wana kila sababu ya kujipongeza kwa matokeo hayo na zaidi kumpongeza beki wao Wilson Nangu ambaye alikuwa mwiba kwa Yanga na haikushangaza baada ya mechi alipotangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa leo, Ken Gold imetoka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Fountain Gate wakati KMC ikiichapa Singida BS mabao 2-0.
Soka Yanga yaambulia pointi moja kwa JKT
Yanga yaambulia pointi moja kwa JKT
Read also