Zurich, Switzerland
Shirikisho la Soka Kimataifa (Fifa) limetangaza kuyafungia kushiriki mashindano ya soka ya kimataifa mashirikisho ya soka ya nchi za Pakistan na Congo Brazaville.
Taarifa ya Fifa iliyopatikana Alhamisi hii ilieleza kuwa Shirikisho la Soka Congo Brazzaville (Fecofoot) limefungiwa kwa kile kinachodaiwa kuwa shughuli za uendeshaji soka zimekuwa zikiingiliwa na makundi mengine.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uamuzi huo wa Fifa umefikiwa baada ya kuwashirikisha viongozi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) waliokwenda Congo kwa ajili ya suala hilo.
Uamuzi wa kuifungia Congo utasitishwa pale baadhi ya hatua zitakapochukuliwa ikiwamo uongozi kukabidhiwa majukumu ya usimamizi wa makao makuu ya shirikisho hilo.
Kwa upande wa Pakistan, shirikisho la soka nchini humo yaani PFF, nalo limefungiwa baada ya kutoifanyia mabadiliko katiba ya shirikisho hilo ili katiba hiyo itoe nafasi ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wa kidemokrasia.
Hii si mara ya kwanza kwa Fifa kuifungia Pakistan, iliwahi kufanya hivyo mwaka 2017 na 2021 sababu ikiwa hiyo hiyo ya masuala ya soka kuingiliwa na makundi mengine ingawa adhabu ya mwisho ilifutwa Juni 2022 baada ya kuundwa kwa tume ya usuluhishi ya PFF.
Kwa adhabu hiyo nchi za Pakistan na Congo hazitoshiriki mashindano yoyote ya kimataifa ya soka yanayotambuliwa au kusimamiwa na Fifa na washirika wake.
Kimataifa Fifa yazifungia Pakistan, Congo
Fifa yazifungia Pakistan, Congo
Read also