Rio de Janeiro, Brazil
Beki wa zamanti wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Marcelo, ametangaza kustaafu soka leo Alhamisi Februari 6, 2025 akiwa amefikisha umri wa miaka 36.
Marcelo mmoja wa mabeki bora wa kushoto duniani, amecheza soka kwa mafanikio kwa miaka 19 akijivunia mataji matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengine sita ya Ligi Kuu Hispania au La Liga.
“Habari yangu katika maisha ya soka imeishia hapa lakini bado nina mambo mengi ya kuyafanya kwenye soka,” alisema Marcelo kupitia video inayohusu maisha yake ya kuvutia katika soka.
Mbali na klabu ya Real Madrid, Marcelo pia anajivunia kubeba mataji kadhaa wakati akicheza soka katika klabu ya Fluminense ya jijini Rio de Janeiro nchini Brazil.
Akiwa Fluminense aliiwezesha kubeba taji la Copa Libertadores mwaka 2023 baada ya kuachana na Real Madrid ambayo taji lake la mwisho lilikuwa lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2022.
Aliachana na Fluminense Novemba mwaka jana baada ya kujikuta katika mzozo na kocha mkuu wa timu hiyo, Mano Menezes wakati wa mechi yao dhidi ya Gremio.
Marcelo pia alicheza soka kwa muda mfupi nchini Ugiriki akiwa na klabu maarufu nchini humo ya Olympiacos.
Kwa mara ya kwanza Marcelo alijiunga na Real Madrid mwaka 2007 akiwa na miaka 18 na kucheza jumla ya mechi 546 katika misimu 15 na nusu na anatajwa kuwa mmoja wa wakongwe wenye rekodi ya kucheza kwa kipindi kirefu katika historia ya klabu hiyo.
Kwa upande wa timu ya taifa ya Brazil, Marcelo aliiwakilisha timu hiyo katika mechi 58 na hakuwahi kubeba taji lolote kubwa na timu hiyo.
Kimataifa Marcelo astaafu soka
Marcelo astaafu soka
Read also