Na mwandishi wetu
Wachezaji 30 wa timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania maarufu ‘Twiga Stars’ wameitwa chini ya kocha Bakari Shime (pichani) wakiwamo 11 wanaocheza soka nje ya nchi.
Kikosi hicho kinajiandaa kwa mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Wanawake (Wafcon) 2026 dhidi ya Guinea ya Ikweta, mechi itakayopigwa Februari 20 mwaka huu.
Kati ya wachezaji wanaocheza soka nje yumo Aisha Masaka anayecheza katika klabu ya Brighton & Hove Albion inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake England.
Wachezaji wengine wanaocheza soka nje ya nchi walioitwa Twiga Stars ni Clara Luvanga wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Opa Clement na Juletha Singano ambao wote wanacheza katika timu ya FC Juarez ya Mexico.
Wengine ni Suzan Adam wa Tutankhamun ya Misri, Maimuna Kaimu wa Zed FC ya Misri, Noela Luhala wa Asa Tel Aviv ya Israel, Enekia Kasonga wa Mazatlan FC ya Mexico na Diana Lucas wa Trabzonspor ya Uturuki.
Katika kikosi hicho pia wamo Hasnath Ubamba wa FC Masar ya Misri pamoja na Malaika Meena wa Bristol City ya England.
Wachezaji wengine waliomo katika kikosi hicho ambao wanacheza soka nchini na timu zao katika mabano ni Najat Abbas (JKT Queens), Aisha Mrisho (Mashujaa Queens) na Janet Shija (Simba Queens).
Wengine ni Lydia Maximilian (JKT Queens), Donisia Minja (JKT Queens), Jamila Rajab (JTK Queens), Aisha Mnnuka (Simba Queens), Asha Ramadhan (Yanga Princess), Winfrida Gerarld (JKT Queens) na Winfrida Charles (Fountain Gate).
Katika orodha hiyo wengine ni Ester Maseke (Bunda Queens), Anastasia Katunzi (JKT Queens), Christer Bahera (JKT Queens), Ester Mayala (Simba Queens), Vaileth Nicholaus (Simba Queens) na Joyce Lema (Simba Queens).
Wengine ni Janeth Christopher (JKT Queens), Marry Siyame (Fountain Gate) na Stumai Abdallah (JKT Queens).
Kimataifa 11 wanaocheza nje waitwa Twiga Stars
11 wanaocheza nje waitwa Twiga Stars
Read also