Manchester, England
Habari ya mshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford kuihama timu hiyo imechukua sura mpya ikidaiwa kwamba sasa anataka kwenda Barcelona au Barca hata kwa mshahara pungufu.
Rashford kwa sasa hafurahii maisha Man United na tayari ameweka wazi nia yake ya kutaka kuhama kwa amani na asingependa kuhama kwake kukaandamana na kauli za kulaumiana.
Tayari timu za PSG ya Ufaransa na Napoli ya Italia zimekuwa zikihusishwa na mipango ya kumsajili mshambuliaji huyo wa England na sasa Barca inaongeza idadi ya timu hizo.
Chanzo kimoja cha habari kimearifu leo Jumapili, Januari 26 kwamba Rashford, 27, angependa mpango wa kuhama kwake ukamilike wakati wowote kipindi hiki cha Januari.
Habari kutoka Barca hata hivyo zinadai kwamba mpango wao wa kumsajili Rashford unaweza kukamilika iwapo beki wa timu hiyo, Andreas Christensen, 28, kutoka Denmark atakuwa tayari kuhama.
Rashford amejikuta katika wakati mgumu tangu kocha Ruben Amorim aanze kuinoa timu hiyo akichukua nafasi ya Erik ten Hag aliyetimuliwa kutokana na matokea mabaya.
Amorim ambaye naye bado hajawa na matokeo ya kuvutia, amewahi kunukuliwa akisema kwamba hana tatizo iwapo RAshford mwenyewe ataamua kuondoka Man United.
Kimataifa Rashford aitaka Barca
Rashford aitaka Barca
Read also