Napoli, Italia
Klabu ya soka ya Napoli ya Italia inadaiwa kuwa katika mpango wa kuwasilisha ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford.
Rashord, 27, kwa sasa anapitia kipindi kigumu katika kikosi cha kwanza cha Man United chini ya kocha Ruben Amorim ambaye amekuwa akimuondoa katika kikosi hicho kwenye mechi kadhaa za hivi karibuni.
Amorim anadaiwa kuchukua uamuzi huo kwa kile alichowahi kusema kwamba hajavutiwa na uwajibikaji wa mchezaji huyo kwenye mazoezi na zaidi ya hilo amesema hana tatizo iwapo mchezaji huyo atataka kuondoka Man United.
Rashford ambaye ni hivi karibuni tu ameanza kuitwa kwenye kikosi cha timu ya England chini ya kocha Thomas Tuchel, huenda akaikosa nafasi hiyo kama ataendelea kukosa nafasi ndani ya kikosi cha Man United.
Mpango wa mshambuliaji huyo kwenda Napoli huenda ukawa suluhisho lililobaki hasa kwa kuwa hata mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema angependa kuondoka kiungwana Man United.
Rashford aliwatolea mfano bila kuwataja majina wachezaji ambao kuondoka kwao katika klabu hiyo kuliandamana na kuibuka kwa kauli tata jambo ambalo alisema asingependa iwe hivyo kwake.
Katika siku za karibuni pia zimekuwapo habari kwamba Rashford amekataa ofa kadhaa nono nchini Saudi Arabi kwa kile kinachodaiwa kwamba angependa kuendelea kucheza barani Ulaya katika ligi zenye ushindani.
Wakati habari ya Rashford kwenda katika klabu hiyo ya Ligi Kuu Italia maarufu Serie A ikiwa hivyo, klabu hiyo pia inadaiwa kujiandaa kuachana na winga wake, Alexander Isak kutoka nchini Georgia.
Kimataifa Rashford atakiwa Napoli
Rashford atakiwa Napoli
Read also