Na mwandishi wetu
Timu ya soka ya Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Star’s itatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuumana na wenyeji Zanzibar Heroes kesho Ijumaa, Januari 3, 2025.
Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa na Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF), leo Alhamisi, Kenya itacheza mechi yake ya kwanza keshokutwa Jumamosi kwa kuumana na Burkinafasso.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mechi zote za michuano hiyo zitachezwa kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba kuanzia saa mbili usiku ambapo siku ya Jumapili itakuwa ya mapumziko.
Baada ya hapo michuano hiyo itaendelea Jumatatu ya Januari 6, 2025 kwa mechi kati ya Burkinafasso na Zanzibar wakati siku inayofuata Kilimanjaro Stars itacheza na Kenya.
Januari 9 kutakuwa na mechi kati ya Burkinafasso na Zanzibar na Januari 10, Kenya itacheza na wenyeji Zanzibar Herous.
Michuano hiyo itasimama kwa siku mbili Januari 11 na 12 kabla ya kufikia tamati Januari 13 kwa mechi ya fainali.
Awali michuano hiyo ilikuwa ikishirikisha klabu ambapo Mlandege ndio waliokuwa mabingwa wa mwaka 2024 ambao pamoja na kombe walipewa kitita cha Sh milioni 100 lakini safari hii waandaaji ZFF wameamua kuzishirikisha timu za taifa.
Soka Kili Stars, Zanzibar Heroes kuliamsha Mapinduzi
Kili Stars, Zanzibar Heroes kuliamsha Mapinduzi
Read also