Manchester, England
Katika kinachoonekana kuwa ni kukabiliana na janga la majeruhi na kusaka matokeo, Man City inadaiwa kuanza hesabu za kumsajili kiungo wa zamani wa Man United, Paul Pogba.
Mwenendo wa Man City kwa sasa si mzuri katika Ligi Kuu England (EPL) na moja ya matatizo yanayoikabili timu hiyo ni janga la wachezaji majeruhi ambalo wanataka kukabiliana nalo.
Mabingwa hao watetezi wa EPL wamepoteza ubora wao wa misimu michache iliyopita hali ambayo pia imeanza kuibua maswali kuhusu nafasi ya kocha wa timu hiyo, Pep Gurdiola kama vile ameanza kuishiwa mbinu.
Pogba hata hivyo kwa sasa anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kujihusiha na soka baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu, adhabu ambayo inafikia ukomo Machi mwakani.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hiyo Pogba hata hivyo huenda asiwe tayari kwa mpango huo utakaomrudisha kwa mara nyingine kwenye EPL.
Pogba ambaye mwaka 2018 aliiwakilisha vyema timu ya taifa ya Ufaransa hadi kubeba Kombe la Dunia, mambo yake hayakuwa kama ilivyotarajiwa mara baada ya kuhamia Man United.
Baada ya mambo kuwa magumu United, mchezaji huyo aliamua kurudi nchini Italia na kujiunga na Juventus na ndipo alipokutana na kashfa ya utumiaji dawa za kuongeza nguvu.
Kimataifa Man City yamtolea macho Pogba
Man City yamtolea macho Pogba
Read also