London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta ameikumbuka Barca iliyokuwa bora eneo la kiungo chini ya Iniesta, Xavi na Sergio Bosquets na kujiaminisha kuwa Bukayo Saka na Martin Odegaard wanaweza kutengeneza safu bora ya kiungo kama hiyo.
Ødegaard aliyekuwa majeruhi akisumbuliwa na enka amerudi akiwa bora na kuifanya Arsenal iwe moto, ikishinda mechi tatu katika wiki huku Saka naye akitoa mchango mkubwa katika mafanikio hayo.
Msimu uliopita, Ødegaard aligawa pasi nyingi zaidi kwa Saka (320) hali ambayo imeonesha namna wachezaji hao wanavyojuana na wanavyokwenda vizuri katika mbio za kuipatia mafanikio Arsenal.
Alipoulizwa kuhusu wachezaji wawili wanavyocheza kwa kuelewana, Arteta aliwalinganisha na magwiji wa Barca, ambao mbali na mafanikio yaliyoonekana kwenye klabu pia waliisaidia timu yao ya taifa ya Hispania hadi kubeba Kombe la Dunia na Kombe la Ulaya au Euro.
“Wanaweza kuwa bora katika namna hiyo kwa sababu wao ni viungo washambuliaji na mawinga,” alisema Arteta kuhusu Saka na Ødegaard.
Arteta hata hivyo alisema kwamba pia aliwahi kuwaona mabeki wa kati wenye kucheza kwa maelewano, viungo wa kati lakini wakati wote amekuwa mwenye kuwafikiria Xavi, Iniesta na Busquets kwa kuwa walikuwa wa kipekee.
Katika siku za karibuni, kiungo mwingine wa Arsenal, Jorginho alisema kwamba Saka ana uwezo wa kuingia katika mbio za kuwania tuzo ya Ballon d’Or kama tu atakuwa mwenye kujiamini katika hilo.
Kimataifa Arteta aitaka Barca ya Iniesta, Xavi Arsenal
Arteta aitaka Barca ya Iniesta, Xavi Arsenal
Read also