Na joseph shaluwa
Albamu mpya ya ‘It’ll All ya Make Sense Later’ ya staa wa muziki nchini Nigeria, Eric Bellinger (pichani) imewashirikisha mastaa kibao akiwemo Burna Boy ambaye anzo ya Muziki ya Grammy.
Mastaa wengine walioshirikishwa kwenye albamu hiyo ni mkali wa RnB kutoka Ghana, Gyakie na mastaa wengine wa Nigeria ambao wamepata kushinda Tuzo ya Grammy, Reekado, Banks, Oxlade, Tempoe na Taves.
Bellinger ambaye naye pia amewahi kushinda Tuzo ya Grammy, albamu yake hiyo mpya inapatikana katika mifumo mbalimbali ya kidigitali mitandaoni.
Albamu yake hiyo iliyotengenezwa Cape Town, Afrika Kusini, ndani yake ina mikong’osia ya aina yake yenye ladha za Kiafrika katika mitindo ya R&B, Afrobeats na Amapiano.
Akizungumzia albamu hiyo, Eric anasema: “Nilisafiri hadi Afrika Kusini kwa ajili ya kutengeneza hii albamu. Hii ni moja ya kazi iliyonipa uzoefu mkubwa sana katika utengenezaji wa muziki.
“Ni kazi nzuri hakika. Inanipa nguvu ya kusonga mbele, kujiamini katika kazi zijazo, ndiyo maana nimeiita hii albamu, ‘It’ll All Make Sense Later’ yaani ‘Italeta Maana Baadaye.
Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo na wasanii walioshirikishwa kwenye mabano ni Pure, Special (feat. Konshens), Feelings Never Die na Shooting Star (feat. Oxlade).
Nyingine ni Precision (feat. Reekado Banks), Backtrack (feat. Taves), Don’t Shut Off The Lights na For The Evening (feat. Burna Boy).
Vibao vingine ni Ms Africa (feat. Gyakie), Desire, Follow Her Lead, No Coincidence (feat. Geko), Top Dolla (feat. Vscript), Don’t Leave na Unfinished Business.
Wanamuziki wengine aliowahi kupiga nao kolabo ni Usher Raymond, Justin Bieber, Ne-Yo, bila kuwasahau Chris Brown na OG Parker.
Bellinger pia amepata kuandika mashairi ya nyimbo na kuwatayarishia wasanii mbalimbali maarufu duniani.
Burudani Albamu ya Bellinger mastaa kibao
Albamu ya Bellinger mastaa kibao
Related posts
Read also