Turin, Italia
Kiungo wa Juventus, Paul Pogba huenda akajikuta anakuwa mchezaji huru baada ya habari kwamba mkataba wake umeanza kujadiliwa na klabu hiyo kwa kinachoaminika kuwa unataka kuvunjwa.
Pogba, 31, kwa sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi 18 ambayo imepunguzwa kutoka ya miaka minne ya awali baada ya kukata rufaa alipoadhibiwa kwa kosa la kutumia madawa ya kuongeza nguvu.
Mara baada ya kukutwa na hatia na kufungiwa miaka minne, Pogba alikata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo na ndipo adhabu hiyo ilipopunguzwa kutoka miaka minne hadi miezi 18.
Kwa hali ilivyo sasa Pogba anaweza kuanza mazoezi mapema Januari mwakani na atakuwa na haki ya kucheza soka la ushindani mwezi Machi mwakani.
Matarajio hayo hata hivyo huenda yakamfanya aendelee kucheza soka sehemu nyingine baada ya mabosi wa Juve kuanza mazungumzo lengo likiwa ni kumpa nafasi ya kwenda katika klabu nyingine.
Mkataba wa Pogba na Juve unafikia ukomo Juni 2026 lakini zipo habari kwamba makubaliano ya pande mbili yanaweza kumfanya asifikie wakati huo na kusaini mkataba na timu nyingine.
Tangu arudi kwa mara nyingine katika klabu ya Juve mwaka 2022 akitokea Man United, Pogba ameichezea timu hiyo mechi 12 tu na mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Napoli ambayo hakucheza yote ingawa Juve ilishinda kwa mabao 2-0.
Kimataifa Juve waujadili mkataba wa Pogba
Juve waujadili mkataba wa Pogba
Read also