Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Yanga imeunda kamati mpya ya mashindano ambayo jukumu lake pamoja na mambo mengine ni kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mashindano inayoshiriki.
Kamati hiyo iliyotangazwa Alhamisi hii na rais wa klabu hiyo Injinia Hersi Said itaendelea kuwa chini ya uenyekiti wa Rodgers Gumbo ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo.
Wengine waliomo katika kamati hiyo ni pamoja na Lucas Mashauri ambaye anaendelea na nafasi yake ya makamu mwenyekiti ambao kwa pamoja watasaidiana na wajumbe wengine sita.
Wajumbe hao ni Seif Ahmed maarufu Seif Magari ambaye pia si jina geni ndani ya kamati hiyo kwani amewahi kuiongoza wakati wa uenyekiti wa Imani Madega na baadaye Yusuph Manji.
Wengine walio katika kamati hiyo ni Davis Mosha ambaye pia aliwahi kuwa makamu mwenyekiti miaka ya nyuma pamoja na Mustapha Himba, Majid Suleiman, Pelegriunis Rutayuga na Omar Kimosa.
Yanga kwa sasa inapambana kulitetea taji la Ligi Kuu NBC wakati huo huo ikiwa ni mtihani wa kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Jumamosi hii itakuwa ugenini Ethiopia kuumana na Commercial Bank of Ethiopia (CBE).
Soka Hersi ateua kamati ya ushindi Yanga
Hersi ateua kamati ya ushindi Yanga
Read also